View attachment 453623
Source TBC
Waziri Mkuu achangisha takribani Bil 1.4 kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi Kagera - TBC.go.tz
Jumla ya Shilingi Bilioni Moja na Milioni 396 zimeweza kukusanywa ikiwa ni mchango wa kusaidia tetemeko la Ardhi lililotokea September 10,2016 .
Waziri Mkuu KASSIM MAJALIWA amesema taifa limepata hasara kutokana na tetemeko kubwa lililotokea mkoani KAGERA mwishoni mwa wiki iliyopita.
Katika mkutano uliofanyika jijini DSM na mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini na Jumuiya ya wafanyabiashara nchini kwa lengo la kuchangia waliokumbwa na tetemeko Waziri Mkuu MAJALIWA amesema serikali inahangaika kuendelea kutoa misaada kwa waliokumbwa na tetemeko.
Amesema shule nne za sekondari zimeharibika na shule mbili zimefungwa kwa muda ili kuzifanyia marekebisho.
Waziri Mkuu MAJALIWA amesema Kamati ya maafa kwa kushirikiana na mkoa wa KAGERA wanaendelea kupitia maeneo mbalimbali kufanya tathmini ili kubaini kiwango cha hasara.
Amesema Rais JOHN MAGUFULI na serikali kwa ujumla inawashukuru waliojitokeza kutoa misaada mbalimbali na wale walio tayari kuendelea kutoa michango ya hali na mali kwa waliokumbwa na tetemeko.
Waziri Mkuu ulikuwa mstari wa mbele kutuchangisha kwa ajili ya kuwasadia wahanga wa tetemeko la Kagera,ukaongea kwa unyenyekevu ukilengwa na chozi huku kwa kutumia kitambaa ukijifuta manyunyu ya machozi, leo hii tunakashifiwa umekaa kimya.
Tukumbushe waziri mkuu ni lini uliwahi kusema tunaichangia serikali kwa ajili ya kujenga miundombinu yake
Mungu nakukabidhi hili jambo utahukumu kwa mapenzi yako kwa wana Kagera
Asubuhi jema