ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 58,628
- 69,254
Mbunge wa Bukene Selemani Zedi (CCM), ameonesha kutoridhishwa na kupunguzwa kwa bajeti ya maji na kuishauri serikali kuongeza bajeti hiyo kwa kuwa ni sekta muhimu kwa wananchi.
Akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Maji, Zedi amesema kuna tatizo lingine pia pamoja na bajeti ya maji kupungua hata hiyo iliyopangwa maeneo mengi haiendi kikamilifu kama ilivyopangwa,kwa mfano katika halmashauri ya wilaya ya Nzega huu mwaka unaoisha mwezi ujao tulitarajia kupata bilioni 10 za maji lakini mpaka sasa umebaki mwezi mmoja wamepata sh.bilioni tano tu.
"Ushauri wangu kwa serikali maji ni muhimu mno na fedha zote zinazopangwa kwa ajili ya maji zinapaswa kwenda kwa asilimia 100,”amesema Zedi.
Katika bajeti hiyo, Wizara imeidhinishiwa kiasi cha Sh.Bilioni 627.7 katika mwaka 2024/25 ambapo katika bajeti iliyopo ya mwaka 2023/2024,wizara hiyo iliidhinishiwa Sh.Bilioni 756.2.
My Take
Licha ya vilio na adha kubwa ya ukosefu wa Maji ya matumizi Kwa binadamu na maendeleo, Serikali imepunguza Fedha ilizotenga kwenye Bajeti ya Wizara ya Maji Kwa zaidi ya 17% kutoka Bilioni 750 Hadi Bilioni 627.
Kwa sekta nyeti kama ya Maji harafu unapunguza Bajeti ni jambo la kushangaza.Ni vyema wabunge wasikubliane na huu utaratibu.
Ilianza Wizara ya Nishati na Sasa ni Wizara ya Maji,zote Mbili ni Wizara Nyeti ila Zimepunguziwa Bajeti zake.
Utaratibu huu Haukubaliki,punguzeni Bajeti kwenye Wizara za Madini,Maliasili na Utawala sio kwenye Wizara Zenye maslahi na Wananchi.
Pia soma Serikali imetumia busara gani kupunguza Bajeti ya Wizara ya Nishati wakati kuna Maombi Mengi ya Kuunganisha wateja wapya?
Source: Nipashe, Mwananchi News