Inaelekea maana ya neno 'fake' ilipotoshwa ktk uhakiki wa vyeti feki na hiki ndicho kimezaa kizaazaa

Dr Akili

JF-Expert Member
Aug 21, 2011
5,060
4,500
Neno feki linatokana na neno la kiingereza 'fake'. Lina maana 'An object or situation that is made to look real or valuable in order to deceive people'. For a example fake passport, fake money notes, fake smile, fake accident and so forth. Yaani kama ni cheti feki ni karatasi iliyotengenezwa ionekane kama cheti halisi, wakati sivyo, kwa madhumuni ya kudanganya watu au mamlaka fulani.

Zoezi la uhakiki wa vyeti vya watumishi wa umma lilijikita kwenye uhakiki wa vyeti vyao vya kidato cha 4 na 6 tu na wala siyo uhakiki wa vyeti vyao vya kitaaluma. Hii ni kwa sababu data base tulizonazo ni za kidato cha 4 na 6 tu ambazo ziko NECTA, nazo ni za kuanzia miaka ya 1990s; nyuma ya hapo haziko maana hata computer za kuhifadhia hatukuwa nazo. Vyeti vya elimu ya juu na vya kitaaluma hatuna database ya kutosha kufanya uhakiki.

Baada ya uhakiki huo wa vyeti vya elimu ya sekondari waliyonayo watumishi hao wa serikali makundi makubwa mawili (ya the so called wenye vyeti feki) yalitokea kama ifuatavyo:

1. Kundi A (inaelekea ndiyo kubwa):

Hawa ni watumishi wenye taaluma zao ambao vyeti vya taaluma zao hazikuhakikiwa na bila shaka hazina utata kwani wamekuwa wakifanya kazi zao za kitaaluma kwa ufanisi hadi kupanda vyeo kwenye ngazi za utumishi wa umma. Tuwesikia wauguzi na waalimu waandamizi, madaktari bingwa, wahadhiri wa vyuo vikuu na hata baadhi ya waliokuwa kwenye tume ya uhakiki yenyewe.
Kundi hili vyeti vyao vya kidato cha 4 au 6 ni halisi (real) lakini havikuwa vya viwango vya kuwawezesha kujiunga na elimu ya vyuo walivyosomea taaluma zao (kwa vigezo vya sasa nadhani). Unakuta kwa mfano muuguzi mwandamizi lakini ana cheti tu cha form 4 ambacho ni halisi lakini alipata F kwenye masomo yote ya PCB ya kidato cha 4. Daktari bingwa ambaye hakusoma kidato cha sita na ufaulu wake wa form 4 ni wa divission IV. Alijiunga na chuo kikuu kwa alternative qualifications hususani mature age, remedial studies au tu chuo kikuu husika (hasa vyuo vikuu vya nje hususani vya Urusi na China) viliona anatosha kujiunga navyo. Wimbi la wanafunzi waliomaliza form 4 au 6 wenye ufaulu pungufu uliongezeka sana baada hasa ya kuongezeka kwa vyuo vya tasisi binafisi ikwemo vyuo vikuu binafsi. Walidahiliwa kihalali wakati huo kwani serikali ya wakati huo ilijua au ilipaswa kujua na wengi wao iliwapa hadi mkopo wa masomo yao hayo ya elimu ya juu. TCU haikuweka objection. Kama TCU (ama mamlaka nyingine husika) ya wakati huo ilikuwa imelala na hivyo kutotimiza wajibu wake, haliwahusu watumishi hawa.

Vyeti vya form 4 au 6 vya watumishi hawa si feki by definition. Hawana kosa lo lote la jinai. Hawakufanya udanganyifu wo wote kujiunga na vyuo hivyo. Serikali kama mwajiri ina hiari kama inaona watu wa aina hiyo (waliojiunga na vyuo vya taaluma kwa ufaulu usioridhisha wa kidato cha 4 na 6) haiwataki kwenye ajira yake kuwaondoa / kuwapunguza kwa utaratibu uliowekwa wa kisheria ambao ni pamoja na kuwapa notisi ya mwezi mmoja na kuwalipa haki zao. Serikali inapaswa kumwandikia barua kila mhusika ikimjulisha kwa nini imeamua kumpunguza kwenye utumishi wa umma (elimu yake ya kidato cha 4 au 6 haitoshelezi kuendelea naye katika utumishi wa umma kwa cheo alichonacho) baada ya notisi ya mwezi mmoja kumalizika. Barua hiyo pia ieleze kuwa atalipwa stahili zake zote baada ya kuachishwa kazi ikiwamo akiba yake ya uzeeni/ pension.

2. Kundi B:
Hawa ni wale waliotengeneza au kununua vyeti bandia (vyeti feki) au waliiba vyeti halisi vya watu wengine na kujifanya ni vyao ( hawa ni wezi wa vyeti, vyeti siyo feki lakini waliziiba na kumdanganya muajiri au mdahili wa chuo) au walichakachua vyeti vyao halali kwa kubadilisha alama halisi zilizokuwamo kwenye vyeti vyao halisi kwa mfano alama D isomeke B ( hawa ni wachakachua vyeti).
Hivyo kundi hili la watumishi wa serikali ni la watumishi wa serikali ambao wana vyeti halali vya taaluma zao na wana sifa za kitaaluma zinazokubalika kwenye kazi zao na ndiyo maana wamekuwa wakipanda vyeo kwenye utumishi wa umma, ila huko nyuma wakiwa kidato cha 4 au 6 walifanya makosa ya jinai aidha kwa kuiba vyeti, kutengeneza/ kutumia vyeti feki au kuchakachua vyeti hivyo.
Watumishi hawa waliweza kukwepa mkono wa sheria kipindi hiko. Makosa ya jinai huwa hayana time bar. Hivyo ni halali serikali kuwashughulikia inavyopaswa kwa mjibu wa sheria. Kuwafukuza kazi ni sawa kabisa ila kila muhusika aandikiwe barua yake inayobainisha kosa lake (kukutwa na cheti cha kugushi/ feki, cha wizi au kuchakachua matokeo ya cheti chake) na pia barua hiyo ibainishe adhabu aliyopewa (eg kufukuzwa kazi na kupoteza mafao yake yote ya uzeeni/ pension).

Ombi: Maafisa utumishi wa wizara na taasisi mbalimbali za umma wakiongozwa na wenzao wa Utumishi wa Umma wafanye zoezi hili la kuhitimisha zoezi la uhakiki wa vyeti, kitaalamu wala wasichanganywe na mihemuko ya kisiasa. Lisipofanyika na kuhitimishwa kitaalamu kwa mjjbu wa Standing Orders na sheria za utumishi wa umma hiki kizaazaa kinaweza kuligharimu fedha nyingi serikali yetu.

Pia ni vyema sasa vyeti vya elimu ya juu na za kitaaluma za watumishi hawa wa umma nazo zikafanyiwa uhakiki. Vyeti hivi ni vya muhimu sana kuliko hivyo vya shule za sekondari. Kama hizo za shule waliweza kuzigushi watashindwaje kugushi vyeti vya digrii na taaluma mbali mbali. Utakuta mtu ana cheti feki cha udaktari wa binadamu ( vile vya form 4 na 6 viko safi) na hivyo unakuta kaajiliwa kama daktari akitibu watu kwa elimu yake ya hapa na pale ya uganga. Ni hatari.

Makosa yaliyopatikana kwa watumishi wa umma niliyoyaorodhesha kwenye kundi B ni ya jinai. Hivyo hata watumishj walioko sekta binafsi vyeti vyao vihakikiwe. Kosa la jinai linakata sehemu zote. Halihalalishwi kwa kuwa umeajiriwa sekta binafsi. Hata kama hukuajiriwa ukikutwa na vyeti vya bandia unapaswa ushughulikiwe kwa mjibu wa sheria. Vinginevyo hata hawa watumishi watahamia sekta binafsi.
 
Nani alokwambia hukukua na database miaka hyo?!! database ni nini? database ilikuepo sema haikua fresh km ya saiv,mbna kwenye vitabu yaan hardcopies yapo tu ya miaka yote ni suala tu la kuyacapture .
 
Nani alokwambia hukukua na database miaka hyo?!! database ni nini? database ilikuepo sema haikua fresh km ya saiv,mbna kwenye vitabu yaan hardcopies yapo tu ya miaka yote ni suala tu la kuyacapture .
Kwa taarifa yako hata hiyo NACTE na NECTA hazikuwapo. Vyeti vya kidato cha 4 na 6 vilitolewa na University of Cambridge Local Examination Syndicate ambalo ndilo lilikuwa likitahini wahitimu hao kutokea London. Jukumu hilo lilichukuliwa na wizara ya elimu (Tanzania bara) na wizara ya elimu (Zanzibar) mwaka 1972. Mkurugenzi wa wizara ya elimu ndiye alikuwa akitoa vyeti hivyo. Vyeti havikuwa na picha wala biometric identification yo yote ya mhusika wa cheti. Wizara haikubaki na nakala yo yote ya cheti. Sana sana ni matokeo ya ujumla ya mtihani wa mwaka huo iliyokuwa inachapishwa kwenye gazeti la The Standard. Huwezi kufanya uhakiki kwa documents za aina hiyo.

NACTE (The National Council for Technical Education) na NECTA (The National Examination Council of Tanzania) zilianza miaka ya 1990s kama tasisi zinazojitegemea. Mfumo wa database ya vyeti vilivyokuwa vinatolewa uliwekwa baadaye wa kijidijitali na taasisi hizi. Mfumo huu ndiyo uliotumika kufanya uhakiki huu wa watumishi. Hizo rekodi za magazeti ya standard au kumbukumbu zilizoko kwenye museum ya Cambridge University hakuna aliyejisumbua kuzitafuta kwani hata kama zingepatikana hizo hard copies hazingesaidia.
 
Kwa taarifa yako hata hiyo NACTE haikuwapo. Vyeti vya kidato cha 4 na 6 vilitolewa na University of Cambridge Local Examination Syndicate ambalo ndilo lilikuwa likitahini wahitimu hao kutokea London. Jukumu hilo lilichukuliwa na wizara ya elimu (Tanzania bara) na wizara ya elimu (Zanzibar) mwaka 1972. Mkurugenzi wa wizara ya elimu ndiye alikuwa akitoa vyeti hivyo. Vyeti havikuwa na picha wala biometric identification yo yote ya mhusika wa cheti. Wizara haikubaki na nakala yo yote ya cheti. Sana sana ni matokeo ya ujumla ya mtihani wa mwaka huo iliyokuwa inachapishwa kwenye gazeti la The Standard. Huwezi kufanya uhakiki kwa documents za aina hiyo.

NACTE ( The National Council for Technical Education) ilianza miaka ya 1990s kama tasisi. Mfumo wa database ya vyeti vilivyokuwa vinatolewa uliwekwa baadaye kijitali. Mfumo huu ndiyo uliotumika kufanya uhakiki huu wa watumishi. Hizo rekodi za magazeti ya standard au kumbukumbu zilizoko kwenye museum ya Cambridge University hakuna aliyejisumbua kuzitafuta kwani hata kama zingepatikana hizo hard copies hazingesaidia.
Sorry,siyo NACTE,bali ni NECTA.NACTE ni National Council for Technical Education as Opposed na NECTA.
 
Back
Top Bottom