Inachukua muda gani kuitwa kazini?

mliverpool

JF-Expert Member
Jan 6, 2015
1,558
2,937
Ndugu zangu naomba kuuliza, hivi inachukua muda gani toka mtu anapopigiwa simu ya kufaulu usaili mpaka anapoenda kuanza kazi??

Kuna ndugu yangu alipigiwa mwishoni mwa mwezi Wa 5 kuwa amefaulu usaili aliofanya kwenye shirika la serikali uliosimamiwa na utumishi, ikabidi atoke mkoani kuja Dar akijua anakuja kuanza kazi, akaenda ofisini akapewa barua na kuna fomu akajaza ,akapeleka na vitu alivyoambiwa apeleke akaambiwa asubiri asianze kazi mpaka aingizwe kwenye system.

Sasa ni wiki ya pili inaisha naye ameganda tu, anasubiri hajui hiyo system inamuapprove lini, kuna vitu vyake aliacha pending mkoani kuondoka anashindwa.

Wenye uzoefu hebu tusaidieni, sometime anakuwa na wasiwasi isije kuwa wamebadili maamuzi n.k
 
duuuh! hapo ss n utata sn! maan mtu ushapelekka kila kitu bt bado tuu wanakwmbia usubiro kwl? hii c sawa!
 
Kuna uwezekano ukaitwa ,ukapewa barua halafu wakabadili maamuzi ya kukuchukua wakamweka mtu mwingine??
 
Pole. Avumilie tu. Tena ikibidi, arudi tu mkoani, wakimuita ndo aje mjini. Kuna watu nawafahamu walikaa miezi 4 bila kuingia kwa system, bahati njema kwao ni kwamba taasisi waliyokuwa waifanyie kazi iliamua kuwalipa, wakaanza wakazirudisha baada ya kuwekewa arrears. Mimi mwenyewe nilikaa miezi sita baada ya kuhama toka taasisi moja kwenda nyingine, na kila mwezi issue ilikuwa ni hiyo hiyo kwamba system bado.
 
Arudi home hadi mshahara ukishaingia

Ukishasajiliwa tayari ushakuwa mtumishi unachosubiri mshahara tuuu ukisoma wakiona uko kimya wenyewe wanapiga simu
 
Kwahiyo ni jambo la kawaida,,asiogope ,maana hata mm nilikuwa napata wasiwasi ,si unajua bongo hii ,unaweza kwenda siku nyingine ukakuta mtu tofauti kakalia nafasi uliyoitwa wewe
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…