Inachukua muda gani kubadilisha jina kwenye passport?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2023
6,972
9,928
Msaada wa haraka tafadhali!

Kuna mtu anahitaji kubadilisha majina kwenye nyaraka zake za muhimu: PASSPORT, DRIVING LICENSE, NIDA, KITAMBULISHO CHA MPIGA KURA, n.k.

Majina yanayobadilishwa ni mawili: la kwanza na la kati. La mwisho (la ukoo) litabaki kama lilivyokuwa. Utaratibu ukoje?

1. Itawezekana kubadilisha majina kwenye pasi ya kusafiria?

2. Gharama ya kurekebisha majina kwenye nyaraka zote muhimu ni shilingi ngapi?

3. Hilo zoezi linaweza kuchukua muda gani?

4. Wapi pa kuanzia katika kushughulikia hiyo changamoto?

5. Inaweza inachukua muda gani hilo zoezi kukamilika?

Asanteni sana wakuu!
 
Sababu za kubadili jina..?
Ni kwa ajili ya kuiridhisha nafasi yake!

1. Katika majina anayoyatumia kwa sasa, jina la katikati na la mwisho yote ni ya baba yake

2. Japo jina la kwanza ambalo ndilo lake ni zuri, anataka abaki nalo lakini litanguliwe na jina lake lingine jipya alilojichagulia mwenyewe ukubwani. Kwa mfano, kama alikuwa akiitwa JOSEPH TREKTA JUMA ambapo Trekta na Juma ni majina ya baba yake (Trekta lilikuwa jina la utani la baba yake na Juma ndilo jina halisi la baba yake), majina yake mapya yatakuwa JAMES JOSEPH JUMA ambapo JAMES na JOSEPH ni majina yake (la James amejipa mwenyewe ukubwani) na Juma ni la baba yake, kwa hiyo jina la babu/ukoo wake halitatumika kwenye utambulisho wake

3. Ili kuwemo na mfanano wa majina yake na ya watoto wake. Watoto wake wanatumia majina 2: JOSEPH JUMA kama majina ya ubin. Kwa mfano, mwanawe wa kiume, tumpe jina la ALMASI, anaitwa ALMASI JOSEPH JUMA.

NB. Majina yote hapo juu ni ya kutungwa lakini yanaakisi hitaji la mwenye hitaji tajwa hapo juu.
 
Unaweza ukajiandikiasha upya tu.

Kwa nini ubadili? Si unaenda unachukua cheti cha kuzaliwa. NIDA Kisha passport?
Kivipi mkuu? Tayari ana passport. Unamaanisha:
1. Akaombe upya BIRTH CERTIFICATE, NIDA, DRIVING LICENSE, n.k.
2. Akaombe upya pasi ya kusafiria na huku aliyo nayo kwa sasa bado "mpya"?
 
Ni kwa ajili ya kuiridhisha nafasi yake!

1. Katika majina anayoyatumia kwa sasa, jina la katikati na la mwisho yote ni ya baba yake

2. Japo jina la kwanza ambalo ndilo lake ni zuri, anataka abaki nalo lakini litanguliwe na jina lake lingine jipya alilojichagulia mwenyewe ukubwani. Kwa mfano, kama alikuwa akiitwa JOSEPH TREKTA JUMA ambapo Trekta na Juma ni majina ya baba yake (Trekta lilikuwa jina la utani la baba yake na Juma ndilo jina halisi la baba yake), majina yake mapya yatakuwa JAMES JOSEPH JUMA ambapo JAMES na JOSEPH ni majina yake (la James amejipa mwenyewe ukubwani) na Juma ni la baba yake, kwa hiyo jina la babu/ukoo wake halitatumika kwenye utambulisho wake

3. Ili kuwemo na mfanano wa majina yake na ya watoto wake. Watoto wake wanatumia majina 2: JOSEPH JUMA kama majina ya ubin. Kwa mfano, mwanawe wa kiume, tumpe jina la ALMASI, anaitwa ALMASI JOSEPH JUMA.

NB. Majina yote hapo juu ni ya kutungwa lakini yanaakisi hitaji la mwenye hitaji tajwa hapo juu.
Kaka sababu ni hii achana nayo.

Fanya mambo mengine upate hela.

Ukijichanganya sana utaharibu mwishoe uanze tena kubadili majina ya vyeti vya shule.
 
Msaada wa haraka tafadhali!

Kuna mtu anahitaji kubadilisha majina kwenye nyaraka zake za muhimu: PASSPORT, DRIVING LICENSE, NIDA, KITAMBULISHO CHA MPIGA KURA, n.k.

Majina yanayobadilishwa ni mawili: la kwanza na la kati. La mwisho (la ukoo) litabaki kama lilivyokuwa. Utaratibu ukoje?

1. Itawezekana kubadilisha majina kwenye pasi ya kusafiria?

2. Gharama ya kurekebisha majina kwenye nyaraka zote muhimu ni shilingi ngapi?

3. Hilo zoezi linaweza kuchukua muda gani?

4. Wapi pa kuanzia katika kushughulikia hiyo changamoto?

5. Inaweza inachukua muda gani hilo zoezi kukamilika?

Asanteni sana wakuu!
Inaweza kuchukua siku, wiki hata miaka. Nchi yenye kudharau katiba na sheria zake, kila mtumishi anafanya kazi anavyojisikia!
 
Ilikuwaje mpaka yakakosewa au jamaa unabadilisha majina?

Maana kukosea sio rahisi kwa sababu ya viambatisho ambavyo hutumika wakati wa kuiomba.
 
Kivipi mkuu? Tayari ana passport. Unamaanisha:
1. Akaombe upya BIRTH CERTIFICATE, NIDA, DRIVING LICENSE, n.k.
2. Akaombe upya pasi ya kusafiria na huku aliyo nayo kwa sasa bado "mpya"?
Unadhani kuomba upya ni njia sahihi??? Je dole gumba alilochukuliwa na NIDA atakapoweka tena unadhani hatajulikana??? Je dole gumba alilochukuliwa na Immigration nalo je???
 
Back
Top Bottom