In Love and Money Tour ya Vanessa Mdee na Jux yawakosha wana Mtwara

Apr 16, 2018
19
7
V.MONEY & BARNABA 3.JPG

Vanessa Mdee na Barnaba wakitumbuiza jukwaani.
JUX & VANESSA &.JPG

Vanessa na Jux wakiperform
BEN POL 4.JPG

JUX & BEN POL.JPG

VANESSA.JPG

Mtwara
. Ni rasmi kuwa wasanii wa Tanzania, Vanessa Mdee na Juma Jux wanakua mfano wa kuigwa katika safari ya maisha yao ya kimuziki baada ya kuzindua rasmi ziara yao iliyopewa jina la “In Love and Money Tour” jijini Mwanza hivi karibuni. Uhusiano wao ulioanza takribani miaka 3 iliyopita umebadilika na sasa kuwa wa kibiashara zaidi baada ya wawili hao kuja na Ziara yao binafsi ya mwezi mzima ambayo itapita kwenye mikoa 5 nchini.

Tamasha la pili la ziara hiyo mkoani Mtwara ambalo lilifanyika mwishoni mwa wiki, lilihudhuriwa na mashabiki wa muziki zaidi ya 10,000 katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona ikiambatana na shoo ya kuvutia. Uwepo wa wasanii wakubwa na maarufu, muziki mzuri, steji ya kuvutia na shoo za kusisimua kutoka kwa wasanii wote vililifanya tamasha hilo kuwa la kufana huku likikata kiu na matarajio ya mashabiki waliofurika katika uwanja huo.

Tamasha hilo lilianza kufunguliwa na wasanii wapya na chipikuzi kwenye tasnia ya Bongo Fleva ikiwa ni pamoja na Brian Simba ambaye yupo chini ya lebo ya Mdee Music. Pia Nancy Namtero Mdee almaarufu ‘Nancy Hebron’ ambaye aliimba nyimbo zake pendwa za injili kisha akafuata 'Marioo' ambaye aliwaamsha mashabiki na nyimbo zake za 'Dar Kugumu' na 'Yale'.

Baadhi ya wasanii wengine waliofanya vizuri kwenye Shoo hiyo ya kuvutia ni pamoja na Mister Kreest, Mimi Mars, Barnaba, na Ben Pol. Lakini Msanii Chege Chigunda alionekana kuwa na shoo nzuri zaidi amabapo aliamsaha ari ya uwanja na kushangiliwa vilivyo na maelfu ya mashabiki.

Vanessa na Jux walipanda kwa pamoja jukwaani mida ya saa saba usiku na kuwaburudisha mashabiki wao kwa takribani saa mbili mfululizo kwa kuimba nyimbo zao zilizowahi kutamba tangu waingie rasmi kwenye tasnia ya muziki. Wapenzi hao pia waliimba wimbo waliofanya pamoja wa ‘Juu’ na kuthibitisha kwa mashabiki jinsi walivyoshibana.

Meneja wa ziara hiyo, Fred Ngimba alisema, "Tunafuraha kubwa kwa mapokezi ambayo mashabiki wetu wa Mtwara wametuonyesha usiku wa leo. Hatukutarajia kuwapata zaidi ya watu 10,000, kwenye shoo hii, huu ni upendo wa dhati ambao wana Mtwara wameonyesha kwa wasanii wangu."

Baada ya Mtwara, 'In Love and Money tour' itaelekea Dodoma tarehe 14 Julai na inatarajia kutoa burudani kwa mashabiki wengi zaidi kama ilivyokua kwa mikoa iliyopita.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom