Imani za kishirikina kwa wachimbaji madini ni hatarishi kwa usalama wa jamii

ZALEMDA

JF-Expert Member
Aug 15, 2017
1,899
2,154
Mimi ni mchimbaji wa madini.namshukuru Mungu kuwa nimeokoka na ni mwanasayansi.
Wachimbaji wadogo ambao wanajiita wanachama au mafadhagora na wengine wanashift hawaamini kuwa wanaweza kupata madini bila kutoa kafara ya mnyama au hata ya mtu kabisa.Hii ni shida kubwa

Ndiyo maana utasikia mtoto kapotea kama yule wa Arusha ,kumbe Kuna mchimbaji wa madini kaenda kwa mganga kumwombe apate dawa apate madini.Mganga anamwambia eti atoe kafara ya mnyama au binadamu achanganye na dawa ndipo atapata madini.

Namba Serikali ingilie Kati kwa kutoa elimu na pia ikiwa mchimbaji atabainika anajihusisha na Imani za kishirikina afukuzwe maeneo ya uchimbaji.shida itakuja eti Serikali haiamini ushirikina.sawa Serikali haiamini ushirikina lakini watu wake wanauawa kwa Imani za kishirikina.

View: https://youtu.be/fy1Rck34Fe8?si=adXclR9rDhItCwhd
 
Nje ya mada mkuu unajua soko la uhakika la blue saphire au una deal na nn zaidi??

Kuna sehem naambiwa ni kwenda kuchota ila najistukia wasije kunibakiza huko. Plus mambo ya kuonana na chief wa hapo kupewa free pass najua kuna mambo ya jadi nakua mzito.
 
Migodini kama hakuna sheria , kesi za watu kuuliwa ni kawaida na wahusika wanadunda na pesa zao ...Migodoni ni dunia nyingine mbele ya pesa unauliwa nje kweupe.
 
Nje ya mada mkuu unajua soko la uhakika la blue saphire au una deal na nn zaidi??

Kuna sehem naambiwa ni kwenda kuchota ila najistukia wasije kunibakiza huko. Plus mambo ya kuonana na chief wa hapo kupewa free pass najua kuna mambo ya jadi nakua mzito.
Duuu.wapi hapo mzee
 
Ushirikina umetawala sana machimboni.

Mkiwa mnachimba shimo la ku-share then ukachukua ile koleo ukailaza chini kwa kuifunika, wenzako wakakuona unaweza kujikuta matatizoni.
 
Ushirikina umetawala sana machimboni.

Mkiwa mnachimba shimo la ku-share then ukachukua ile koleo ukailaza chini kwa kuifunika, wenzako wakakuona unaweza kujikuta matatizoni.
Wanaabudu sana uchawi...
 
Wanaabudu sana uchawi...
Kuna mtu hapo kasema hawa manabii na mitume waende huko kuhubiri asijue hawa nao wanasababisha sana kuenea kwa imani za ushirikina. BTW kuna wauaji wengine mtu unajisemea bora wanyongwe kihalisia, hawa ni mojawapo.
 
Tena huenda washirikina waliobobea ni hao wanaojiita manabii aisee....
 
Back
Top Bottom