Ilikuchukua muda gani mpaka kuunganishiwa Umeme na Tanesco?

Jumanne Mwita

JF-Expert Member
Nov 18, 2014
509
1,341
Mtaa ninamoishi una makazi mengi sana, tena watu hujenga kama vile wamavamia, ila ukweli ni kwamba watu wamejenga, siyo siri.

Nikifikiria siku ninunua hapa, miji haikuwepo kabisa. Ilikuwa ni wazi, unaweza sema kwamba uwezekano wa watu kuja eneo lile haukuwepo, au isingechukua muda mfupi wawe wameisha maliza maeneo yote kujenga.

Lakini cha kushangaza, baada ya mwaka mmoja, eneo lote, yaani kiujumla kijiji hiki nilipo, kimetapakaa nyumba. Huwezi kuona hata mita mia ya uwazi; ni nyumba mwanzo mwisho.

Kibaya zaidi, baada ya nyumba kuwa nyingi, barabara nazo zimeharibika. Hivyo, uwezekano wa kupita gari ni mdogo. Labda Halmashauri ya mji ipitishe Kijigo na mitambo yao ili kulekebisha barabara.

Swali langu linarudi palepale:
  1. Kama mada inavyosema, ni muda gani huchukua mpaka kuletewa Umeme na Tanesco?
  2. Au sheria za Serikali yetu zinasemaje pamoja na kanuni zake pindi makazi kama haya yanapojaa au kukaliwa na watu kwa muda mfupi?
  3. Huduma za haraka kama umeme, maji n.k huja kwa kuzingatia nini au wanataka watu wawapigie kelele ndio waone kwamba hapa kuna watu wanaishi?
  4. Hivi sasa ninavyoandika makala hii miundombini imekufa hata hao Tanesco wakija hawapitishi hata gari unaona sasa, Mpaka miundombinu inaharibika, hawahusiki kwa chochote, raia ndio hukomaa kivyao huku wanaserikali kabisa!!
Hii ni haki kweli?
Kanuni zinasemaje na sheria ya nyumba na makazi inazungumziaje suala kama langu hili?
 
Mwaka Jana nilituma maombi kwa Njia ya Niconect ilikuwa siku ya Jumatatu, siku hiyo hiyo akaja Surveyor.. Kesho yake siku ya Jumanne asubuhi nikatumiwa Control number nikalipia. Siku inayofuata yani Jumatano wakaja Mafundi wakaniwekea Umeme...
 
Aisee wengine mnabahati sana
Mwaka Jana nilituma maombi kwa Njia ya Niconect ilikuwa siku ya Jumatatu, siku hiyo hiyo akaja Surveyor.. Kesho yake siku ya Jumanne asubuhi nikatumiwa Control number nikalipia. Siku inayofuata yani Jumatano wakaja Mafundi wakaniwekea Umeme...
 
Back
Top Bottom