Ili upinzani Nchini uwe na nguvu ya ushawishi kisiasa ni sharti waachane kabisa na kujiongoza kwa hisia, ghadhabu, mihemko na matamko ya bila maono

Tlaatlaah

JF-Expert Member
May 18, 2023
16,550
18,564
Ni muhimu sana wakafanya tafiti za kutosha na kuibua sera, mipango mikakati, na uelekeo mahususi utakao washawishi wananchi wengi zaidi na kukonga nyoyo zao, na hapo ndipo watakua na maana, uhalali na nguvu ya kupambania wananchi.

Na sio kukurupuka kama ilivyo sasa kwa mfano kama Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA na mwenyekiti wake walivyo kurupuka tangu majuzi.

Kwa ujumla, mathalan hapa Tanzania upinzani unatumia hisia, ghadhabu na mihemko kuendesha shughuli zao za kisiasa kitu ambacho sio sahii, badala ya kua na sera mbdala dhidi ya zile za serikali, na zenye mwangaza na kuleta matumaini kwa wananchi waliokata tamaa, na kua na mipango mbdala inayotekelezaka na isiyohatarisha umoja wa kitaifa, bali kuwaleta wanainchi pamoja na kua na uelekeo mahususi wa pamoja..

Kamati za kitaalamu na kibobevu ni muhimu sana kuwamo kwenye vyama vya siasa hususani upinzani ili kusaidia kutathmini athari na faida ya matamko ya kukurupuka na mipango yenye mihemko..

Vyama vya siasa kujiendesha kwa kuvizia mistakes za Taasisi za umma au kutegemea huruma za wananchi na ndipo wanaibuka na matamko ya kukurupuka kama tamko la chadema, ni kujidumaza kisiasa kwasabb hakusaidii kukua kwa demokrasia nchini..🐒

una maoni gani?

Soma Pia: Iko haja ya upinzani nchini kubadilika mtindo na falsafa ya ushawishi kutoka kulalamika tu, hadi kuja na fikra mpya na mipango mbadala ya maendeleo

Mungu Ibariki Tanzania
 
Back
Top Bottom