Ili udumu kazini au kwenye nafasi uliopo lazima uwe na nidhamu ya uwoga au unafiki kwa Mabosi zako

Equation x

JF-Expert Member
Sep 3, 2017
32,565
47,678
Nimejaribu kufanya utafiti mdogo tu, nikagundua ni rahisi waajiriwa kuwaonea au kuwakemea wale wote waliopo chini yao, lakini hawa waajiriwa kwa mabosi zao wanakuwa na nidhamu ya woga au unafiki; wakiogopa kufukuzwa kazi au kuondolewa kwenye nafasi/ cheo walicho nacho.

Na hawana ujasiri wa kupingana na mabosi zao, ata kama atatakiwa kufanya kazi ambayo haiendani na fani yake; yeye atakachofanya ni kutekeleza tu, kutokana na nidhamu ya woga au unafiki aliyojijengea kwa mabosi zake.

Ni wachache sana, ambao hawana nidhamu ya woga au unafiki kwa mabosi zao; ambao wanaweza kuwa tayari kuacha kazi, cheo/ nafasi, kutokutekeleza maagizo ya bosi wake, kutokana na misimamo yao, taaluma yao, na kusimamia kile wanacho kiamini.

Kwa mfano, bosi wako akakupa maelekezo, mfanyie w mizengwe ili aondolewe kwenye ile nafasi, alafu hiyo nafasi upewe wewe; Je utakuwa na uwezo wa kukataa au kupinga?​

Je, wewe huna nidhamu ya woga au unafiki kwa mabosi zako?
 
Back
Top Bottom