Msomi Livelu
Member
- Jun 21, 2024
- 24
- 30
Kashfa kwenye Jeshi la Polisi imekuwa ni Jambo la kawaida, na ukifanya utafiti utagundua ni chombo kisichoaminika na inatuhumiwa kwa rushwa, ubakaji na ulawiti. Kila baya polisi.
Je, sababu ni nini?
Pamoja na ukosefu wa maadili, lakini masilahi ya polisi ni duni mno, mishahara kidogo, tena walio wengi malipo yao hayafanyiki hazina, yanalipwa halmashauri. Hawakopesheki kwenye taasisi za kifedha kama ilivyo jeshi la wananchi. Motisha za kazi ni chache.
Kutokutambulika kazi yao huko hazina kunawafanya kazi yao iwe kama temporary, na bosi anaweza kukufukuza muda wowote. Hii inapelekea wasijimini na kupokea amri za kijuha za mabosi wao, mishahara isiyo na uhakika inawafanya waingie kwenye rushwa na kushiriki kwenye magenge ya uhalifu.
Mazingira magumu ya kazi, hamna kota mbovu Tanzania Kama wanazoishi polisi. Tumewapa majukumu mazito ya kulinda raia na Mali zao, lakini tukawadharau kwenye masilahi yao.
Mimi napendekeza jeshi la polisi malipo yao yatoke moja kwa moja hazina Kama jeshi la wananchi. Masilahi yataongeza ufanisi, pia bila kusahau katumizi ya technology, wafungwe ving'amuzi kwenye sare zao. Akienda field bila sare liwe ni kosa linaloweza kumuondosha kazini.