Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 52,223
- 118,246
Wanabodi,
Kama kawa, hii ni makala yangu kwenye gazeti la Nipashe la leo, Ili kupata maendeleo ya kweli, Je Watanzania tujifunze kuukubali ukweli wa tatizo, tutafute ufumbuzi wa kudumu wa tatizo husika, au tuendelee na huu mtindo wetu wa kufunika tuu kombe mwanaharamu apite?. Tutakuwa tunayafumbia macho matatizo hadi lini?. Kama uwepo wa idadi kubwa ya Wamasai Ngorongoro, unatishia ecolojia ya uhai wa uwepo wa mbuga yenyewe, na kama the solution to the problem, ni lazima Wamasai waondoke, then Wamasai lazima waambiwe ukweli kuwa ni lazima waondoke Ngorongoro kwa kupungua wabaki idadi himilivu pekee!.
Ili Tanzania tuweze kupata maendeleo ya kweli, ambayo ni maendeleo endelevu, ni lazima tujifunze kuukubali ukweli halisi jinsi ulivyo, na kukitokea tatizo, tukabiliane nalo kwa kutafuta ufumbuzi wa kudumu, wa tatizo hilo na sio kufunika kombe mwanaharamu apite!. Ngorongoro kuna tatizo, serikali ilitaka kulitatua kibabe, Wamasai wakagoma, alichofanya Rais Samia ni kufunika tuu kombe, lakini tatizo bado lipo na linahitaji ufumbuzi wa kudumu ili tuendelee kuwa na Ngorongoro yenye maendeleo endelevu.
Kufuatia hali ya Ngorongoro ilivyokuwa tense, jambo la kwanza ni pongezi kwa Rais Samia to defuse the tense na kunusuru Ngorongora kwa kuepusha shari kwa mtindo wa funika kombe mwanaharamu apite, kwa kupooza tuu, lakini ukweli unabaki pale pale, Ngorongoro kuna tatizo, Tutafute suluhisho la kudumu kwa kuwatendea haki wana Ngorongoro kwa mujibu wa katiba, sheria, taratibu na kanuni.
Rais Samia ameupooza mtanziko wa Ngorongoro kupitia tamko la Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge na Uratibu), William Lukuvi akizungumza na wananchi wa kata 11 zilizopo Tarafa ya Ngorongoro, akiwasilisha maagizo ya Rais aliyewatuma kuwasilikiza wananchi hao waliokuwa wamekusanyika na kukesha kwa siku 5 wakitaka kujua hatima ya malalamiko yao.
Waziri Lukuvi pia amesema Rais ameagiza uchaguzi katika tarafa hiyo kwa kutumia mipaka ya zamani, ufanyike kama unavyofanyika maeneo mengine nchini.
Eneo la Hifadhi la Ngorongoro (NCA) lilianzishwa mwaka 1959 kwa Wamasai kutoka mbuga ya Serengeti kuhamishiwa Ngorongoro kama eneo la kipekee la matumizi ya mseto, ambapo uhifadhi, utalii, na maisha ya jadi ya jamii ya Wamasai vingeweza kuishi kwa pamoja.
Lengo lilikuwa ni kulinda na kuhifadhi wanyamapori huku Wamasai wakiendelea na maisha yao ya ufugaji wa kiasili. Hata hivyo, kwa miongo kadhaa, usawa huo mwembamba kati ya makazi ya binadamu na uhifadhi wa mazingira ulianza kudhoofika.
Wamasai hao wanapewa huduma zote afya, elimu na chakula cha kujikimu bure, hali iliyopelekea Wamasai kutoka maeneo mbalimbali kujisogeza Ngorongora, ukijumlisha na kuzaliana, kukapelekea idadi ya watu ndani ya NCA kuongezeka sana, sambamba na kuongezeka kwa idadi mifugo na kutishia ecolojia ya eneo hilo.
Idadi ya Wamasai, ambayo ilikuja mwanzo kutoka Serengeti ni takriban 8,000 katika miaka ya 1959, sasa eneo hilo lina watu zaidi ya 100,000.
Ongezeko hili la watu limeleta mzigo mkubwa kwenye rasilimali za eneo hilo, hali iliyopelekea uharibifu wa mazingira, ulishaji wa mifugo kupita kiasi, na migogoro kati ya uhifadhi wa wanyamapori na shughuli za binadamu.
Serikali ya Tanzania, kwa kutambua hitaji muhimu la kuhifadhi ikolojia ya NCA, ilianzisha mpango wa uhamisho wa hiari kwa jamii ya Wamasai.
Mpango huu uliratibiwa kwa kuzingatia ustawi wa Wamasai, kuhakikisha kuwa wale waliokubali kuhamia kwa hiyari, wanapatiwa ardhi ya kutosha, huduma za kisasa, na msaada wa kuhamia kwenye maisha endelevu zaidi.
Uhamisho huu sio wa kulazimishwa, bali ni mchakato uliyopangwa kwa uangalifu bila yoyote kushinikizwa.
Serikali imetoa ardhi mbadala za malisho, shule, vituo vya afya, na huduma nyingine muhimu za jamii zikiwemo afya na elimu katika maeneo ambako Wamasai wanapelekwa kwa kuanzia na Msomera.
Njia hii inalenga kuboresha hali yao ya maisha duni ya Wamasai kupata maisha bora nay a kisasa, nyumba bore zenye huduma za maji na umeme huku uhifadhi NCA ukiboreshwa kwa ajili ya vizazi vijavyo.
Serikali imekuwa wazi kuhusu nia yake na imeendelea na mazungumzo endelevu na jamii ya Wamasai, viongozi wa eneo, na wadau wengine kujibu wasiwasi wao.
Lengo kuu ni kuhakikisha kuwa watu wa jamii ya Wamasai sio tu wanahama kwa hiari kwenda katika hali bora zaidi za maisha, bali pia wanawezeshwa kustawi katika mazingira yao mapya.
Mamlaka zimekuwa makini katika jitihada zao za kuepuka aina yoyote ya ukiukwaji wa haki za binadamu wakati wa mchakato wa uhamisho, kuhakikisha kuwa urithi wa kitamaduni wa jamii ya Wamasai unaheshimiwa na kuhifadhiwa.
Pamoja na juhudi na nia njema za Serikali, kumekuwepo na makundi mbalimbali yanayopokea fedha za nje ili kufitinisha Wamasai na wananchi dhidi ya serikali.
Kwa sasa, mchakato wa uhamisho unaendelea, huku idadi kubwa ya familia za Wamasai zikiwa zimehamia maeneo mapya kwa hiari.
Serikali inaendelea kufuatilia hali hiyo kwa karibu, ikitoa msaada unaohitajika kwa wale waliohamia na kudumisha njia za wazi za mawasiliano na wale waliobaki.
Uhamisho wa Wamasai kutoka Ngorongoro ni ushahidi wa kujitolea kwa serikali ya Tanzania kwa maendeleo endelevu tukubali tukatae utekelezaji una mushleli baadhi ya maeneo.
Kwa kuweka kipaumbele uhifadhi na ustawi wa Wamasai, serikali inafanya kazi kuhakikisha kuwa Eneo la Hifadhi la Ngorongoro linabaki kuwa urithi wa dunia unaotambulika, huku pia ikiunda mustakabali mzuri kwa watu wa jamii ya Wamasai.
Malengo ya serikali kuwahamisha Wamasai Ngorongoro ni jambo jema lakini utekelezaji wake umekumbana na changamoto kadhaa wa kadhaa ikiwemo kutumia shinikizo kuwalazimisha waliogoma kuhama, kutaka kuwahamisha kikuku kwa kutaka kutumia nguvu kwa kuvifuta vijiji, na kuzuia vyakula.
Alichofanya Rais Samia ni kutuliza tuu mtanziko wa tatizo kwa kulipooza, ila tatizo bado lipo.
Mapendekezo yangu.
1. Katika utekelezaji wa zoezi hili, katiba, sheria, taratibu na kanuni za uhamishaji zifuatwe.
2. Ushirikishwa wa wahusika kwa kuwatumia viongozi wa Wamasai wenyewe kwa kuanza na ma Laigwanani wao.
3. Kufanya tathmini mpya ya kuwatambua Wamasai kama Indigenous people, na kufanya upembuzi yakinifu nini kina faida zaidi kati ya binadamu na wanyama, binadamu wakiwa na faida zaidi kiutalii, wanyama ndio wapishe na Tanzania tuanzishe indigenous people tourism kama Marekani Red Indians, Australia Aborigines , News Zealand Maori etc.
4. Jamii zote indigenous za Tanzania, wakiwemo Wahadzabe, Wamang’ati, Watindiga, Wababaig, Wabalungi, na jamii asili za makabila mbalimbali zitambuliwe zilindwe na zitunzwe kama kivutio cha utalii.
5. Kitu muhimu number moja kwenye taifa lolote ni watu, haiwezekani mnyama akathaminiwa kuliko binadamu, ila huyu huyu binadamu akizidi kuzaliana na kutishia ecolojia, ni lazima adhibitiwe, Marekani walitumia Depo Provera, sisi tusifike huko.
Namalizia kwa hili swali, baada ya Rais Samia kuepusha shari kwa kupooza tuu kwa mtindo wa funika kombe, Je Watanzania tujifunze kuukubali ukweli wa tatizo, tutafute ufumbuzi wa kudumu wa tatizo husika, au tuendelee na huu mtindo wetu wa sasa wa kufunika tuu kombe mwanaharamu apite? huku ukweli unabaki pale pale kuwa Ngorongoro kuna tatizo, jee tufunike tuu kombe au sasa tutafute suluhisho la kweli la kudumu kwa kuwatendea haki wana Ngorongoro kwa mujibu wa katiba, sheria, taratibu na kanuni?.
Mungu Ibariki Tanzania
Paskali.