johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 93,961
- 164,208
Rais Magufuli leo anawaapisha wateule wake aliowateuwa hivi karibuni wakiwemo makatibu wakuu na mkuu wa mkoa wa Njombe Ikulu Chamwino jijini Dodoma.
Viongozi Wateule watakaoapishwa Chamwino Dodoma
1. Mhandisi Marwa Mwita Bubirya Kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe
2. Dkt. Aloyce Nzuki, kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii
3. Mhandisi Anthony Sanga,kuwa katibu Mkuu, Wizara ya Maji
4. Dkt. Seif Shekilage, kuwa katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe
5. Dkt. Allan Kijazi, Kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii
6. Mhandisi Nadhifa Kemikimba, kuwa Naibu katibu Mkuu, Wizara ya Maji
7. Dkt. Mwinyi Talib Haji, kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
*Kushuhudia Uapisho wa Wakuu wa Wilaya za Ilala, Maswa, Kalambo,Rombo na Geita
*Kushuhudia Viapo vya Maadili vya Viongozi walioapishwa pamoja na Wakurugenzi watendaji wa Halmashauri walioteuliwa
Eneo: Viwanja vya Ikulu Chamwino- Dodoma Ratiba inaanza saa 4:00 Asubuhi.
Updates:
- Rais Magufuli ameshafika katika viwanja hivi kwa ajili ya kuapisha.
- Zoezi la kuwaapisha Viongozi mbalimbali walioteuliwa limeanza kwa sasa kimeanza kiapo cha Wakuu wa Mikoa na na Manaibu Katibu Wakuu.
- Baada ya tukio la kuapa Wakuu wa Mikoa kwa sasa wanaapa Wakuu wa Wilaya walioteuliwa.
- Zoezi la kuapa kwa Kiongozi mmoja mmoja limekamilika. kwa sasa Viongozi Wateuliwa watatoa ahadi ya Uadilifu ya Viongozi wa Umma ambapo viongozi wote Walioteuliwa wanaapa kwa pamoja.
- Utoaji wa ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa Umma imekamilika zoezi linalofuata ni salamu kutoka kwa viongozi mbalimbali.
Salamu kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Mahenge
Amewapongeza Viongozi wote walioteuliwa katika nafasi mbalimbali na kuwasisitiza kufanya kazi kwa bidii ili kuendana na kasi ya utendaji wa Rais Magufuli.
Sambamba na hilo, Dkt. Mahenge amewaomba wana Dodoma waebdelee kumuunga mkono Rais Magufuli.
Salamu kutoka kwa Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan
Ameanza kwa kuwapongeza viongozi wote walioteuliwa katika nafasi mbalimbali sambamba na kuwasisitiza kwenda kufanya kazi kwa bidii kazi zao kwa bidii.
Katika kuwasisitiza viongozi hao kwenda kuwa wachapa kazi Mama Samia Suluhu amesema "Leo tunaendeleza ile hadithi ya paukwa pakawa, yaani anayeondoka basi mwingine anakaa. Lakini paukuwa pakawa hii si ya bure kwamba anaondoka mtu anakaa mtu. Kaondoka mtu anakaa mtu kuendeleza ile kasi ya maendeleo. Kama uliikuta ilikuwa ndogo wewe unakwenda kuikoleza, kama umeikuta hairidhishi wewe unaenda kuifanya iridhishe."
Salamu na Hotuba ya Rais Magufuli
Rais Magufuli amewapongeza viongozi wote walioapishwa siku ya leo pamoja na kueleza imani yake juu ya viongozi wote aliowateuwa. ameeleza uteuzi huo umetokana kutokana na nafasi zilizopatikana.
Akieleza kuhusu suala la uchukuaji fomu Rais Magufuli amesema Nimepata taarifa kuwa jumla ya watu waliochukua fomu katika kiti cha Ubunge na Uwakilishi kupitia Chama cha Mapinduzi walikuwa 10367 na katika hao ambao wamekamilisha fomu zao zikiwa kamili ni 10321 kwa hiyo wale ambao hawakuzirudisha ni 46 katika nchi nzima. Kwahiyo unaweza kuona kuna watu wengi walijitokeza, haijawahi kutokea.
Akieleza kuhusu Uchaguzi ndani ya Chama cha Mapinduzi katika uteuzi wa wagombea, Rais Magufuli amesisitiza haki itendeke kila mtu apewe haki anayostahili. katika hili Rais Magufuli ametoa rai kuwa anatamani mchakato huo ufanyike wazi kama ambavyo ilifanyika wakati wakiteua Wagombea Urais katika chama hicho. Rais Magufuli amesema "Natamani sana kura zikimalizika zihesabiwe hadharani kama kwenye Mkutano Mkuu"
Akimuelezea Dokta Seif Rais Magufuli amesema Dkt. Seif ni Dokta 'By Profession'. Amesoma akamaliza akapata PhD Uholanzi akaenda kwenye kituo cha Utafiti Ifakara. Miaka ya nyuma aliomba Ubunge Korongwe, hakuwa na hela wala nini alitaka kuwatumikia wanaKorogwe, akapigwa chini.
Alipoondoka nikasema mbona huyu anapenda Siasa nikaenda sema acha nimjaribu kidogo. Nikampa Ukuu wa Wilaya ya Maswa, hakukataa akaenda kufanya kazi vizuri. Maswa ni miongoni wa Wilaya zilizoanzisha Viwanda vya Mkakati. Ndio maana tukasema tumpandishe
Ndio maana ilipopatikana nafasi Songwe Mkoa ambao una Potential nyingi kitaifa nikaona nimteue Dkt. Seif ili akasaidiane na Brigedia Jenerali aende akaendeleze Mkoa wa Songe.
Aidha, Rais Magufuli akimuongelea Naibu Katibu Mkuu Kijazi, amesema "Naibu Katibu Mkuu Kijazi, sikumteua kwasababu Kaka yake ni Katibu Mkuu Kiongozi. Naliweka wazi maana hata Katibu Mkuu Kiongozi sikumwambia" Rais Magufuli amesisitiza kuwa Kijazi alifanya kazi kubwa akiwa TANAPA na kuweka rekodi nzuri ndio maana ilipopatikana nafasi akaona amteue katika Unaibu Katibu Mkuu lakini pia TANAPA aendelee kuisimamia.
Rais Magufuli akifafanua kuhusu kutokuangalia ndugu wala sehemu katika uteuzi wake amesema "Tatizo hili nililipata pia kwa Wateuzi wawili wako hapa, Ndugu Aswege anatoka Mbalali na mwingine anatoka Moshi - Wote wanatoka Ileje, na inawezekana wanatoka Tarafa moja. Ilikuwa ngumu, unajikuta wote wanaofanya vizuri wapo sehemu moja"
Akimuongelea Aswege, Rais Magufuli amesema "Aswege amekuwa Afisa Utumishi Mbalali na mara nyingi amekuwa akikaimu Ukurugenzi na amekuwa akiletewa mizengwe na TAKUKURU. Ile mizengwe ikaisha na TAKUKURU wakamsafisha. Sasa mimi nikaona kama TAKUKURU wamesafisha kwanini mimi nimsafishe kwa kumteua."
Mwenzake alikuwa Municipal Tresuary ya Moshi, jina lake ni gumu gumu ila na yeye anatoka Ileje. Tukampa Ukurugenzi wa Kilolo kwa maana aliyekuwepo pale amepata fursa nyingine. Kuwa ndugu au kutoka sehemu moja sio jambo, unafanyaje kazi ndio muhimu
Katika hili Rais Magufuli amesisitiza kwake watu kutoka sehemu moja au kuwa ndugu sio jambo la msinhgi kwake kitu kikubwa anachoangalia ni uwezo wa utendaji wa watu husika (Perfomance).
"Akimuongelea Chogelo, Rais Magufuli Ndugu Chogelo katika maeneo yote aliyopangwa amefanya kazi vizuri. Tukaona anafaa kwenda Ilala - Unapopeleka DC kwenye Makao Makuu ya Nchi au sehemu kama Dar lazima aende yule aliyefanya kazi sehemu nyingine. Anafanya kazi vizuri sana."
"Na nataka niwaambie Ilala panamfaa sana (Mussa Chigelo) tena zaidi ya Ilala. Ana miaka 56 au 58 kama sikosei, lazima upeleke Ilala mtu 'mature' sio wale 'mature' kacharwa wa Chuo Kikuu. 'Mature' wa kufanya kazi."
Aidha, kuhusu Fadhili Rais Magufuli amesema "Huyu aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Lindi. Enhe! CCM lazima iwemo ndio inatekeleza ilani ya Uchaguzi - Huyu ni mwalimu, amekuwa mwalimu wa shule ya msingi Nanyumbu. Alifanya kazi kaenda kusoma, akapata 'degree' ya kwanza na ya pili Aliposoma akaenda kugombea Uenyekiti wa CCM akashinda, akacha Ualimu na kufanya kazi ya bure. - Amejitolea na Uenyekiti wake amefanya vizuri sana Lindi. Ndiyo maana tumempa Ukuu wa Wilaya Geita. Ndugu Fadhili, hivyo amefadhiliwa kwenda Geita"
Rais Magufuli akidokeza kuhusu Gonjwa la Corona amesema Tuko salama, hata hapa ungekuta tumevaa barakoa Kwani sisi hatuogopi kufa? Lakini Corona iko mbali kule, ilimalizwa kabisa. Tulimuomba Mungu, tukamtanguliza Mungu na Mungu akatusikia. Kila mtalii anakayekuja atakuja na kuangalia Wanyama na kuondoka salama.
"Nakushukuru Jaji Mihayo na Wizara ya Maliasili, nimeanza kuona Watalii wanakuja wengi na ndege zinaleta Watalii wengi - Watu wameanza kuangalia na kuuona ukweli kuwa hapa Tanzania tuko salama. Endeleeni kulitangaza hili. Maadui zetu watazungumza mengi"
Mwisho, Rais Magufuli ameshukuru wote waliohudhuria katika tukio hilo. Rais Magufuli amesema "Katika mwezi huu tumekuwa tukikutana sana hapa katika kuapisha. Inawezekana tusikutane tena hapa - Matumaini yangu tumemaliza labda baada ya kampeni na kadhalika. Ninyi nafasi mmezijaza na sidhani kama mmoja wetu ataenda kutia nia".
Baada ya hotuba ya Rais tukio lililofata ni kupiga picha za kumbukumbu.