Ijue Pumu ya Ngozi (eczema)

Aug 22, 2015
26
46
Pumu ya Ngozi ni nini ?

Pumu ya Ngozi ni ugonjwa wa ngozi unaosababisha kuvimba kwa ngozi (inflammation). Hii huambatana na ngozi kuwasha, kuwa nyekundu, kavu, vipele na mabaka.

Ugonjwa huu ni wa muda mrefu (chronic).
27447tn.jpg

Nini husababisha Pumu ya Ngozi ?

Pumu ya ngozi husababishwa na mshituko wa kinga ya mwili (hypersensitivity) na ngozi ya mwili. Kuna uhusiano wa pumu ya ngozi na magonjwa kama asthma, mafua, msongo (stress) na kurithi (vinasaba).

Dalili za Pumu ya Ngozi :

Dalili kuu tatu wa Pumu ya Ngozi ni ngozi kuwa nyekundu, kuvimba na kupasuka. Pia huambatana na muwasho na kukauka kwa ngozi.

Hii huambatana na magonjwa ya njia ya hewa kama asthma (atopic dermatitis) au baada ya kukutana na kitu kinachosababisha mshituko wa kinga ya mwili na ngozi mfano kipodozi au kemikali nk (contact dermatitis).

Pumu ya ngozi kwa watoto :

Asilimia 8 mpaka 18 ya watoto wote uhathiriwa na ugonjwa huu. Hii huambatana na mabadiliko ya hewa na magonjwa ya mfumo wa hewa mfano mafua na asthma. Mara nyingi ugonjwa huu hupotea ukubwani baada ya matibabu.

Tiba ya Pumu ya ngozi:

-Tiba kuu ya ugonjwa wa pumu ya ngozi ni kuondoa ukavu kwa kuiweka ngozi na unyevu nyevu. Madaktari hushauri kutumia mafuta ya Vaseline yasiyo na manukato. Pia mgonjwa hushauriwa kuogea sabuni isiyo na manukato mfano sabuni ya kipande B-29.

-Daktari pia anaweza kutoa dawa ya kupunguza uvimbe (antiiflammation drug) ya kupaka kama ataona inafaa.

-Daktari pia anaweza kutoa dawa ya kuzuia kinga ya mwili isishambulie ngozi (immunosuppresors drugs).

-Mgonjwa hushauriwa kuchunguza vitu au dawa zinazosababisha ugonjwa huu na kuviepuka mfano aina za vipodozi na kadhalika.

Inashauriwa kupata ushauri wa daktari kila unapopata dalili za ugonjwa wa ngozi.

Dr Luhaja Nginila, MD.
 
Mimi pia nina tatizo linalofanana na hili. Mwanzoni nilikuwa naambiwa ni allergy and kuna baadhi ya vyakula nikaambiwa nisile lakini tatizo halikuisha coz huwa linakuja kwa muda baadae tena linapotea ila haliishi.

But kuna dr mwingine tena akaja nambia ni pumu ya ngozi na haiponi so niwe natumia tu dawa za kutuliza. Huwa nawashwa ngozi natokewa na vipele vidogo vidogo yaani vikichachamaa ni shida.
Nilishatumia dawa mpaka nikachoka! Kama kuna mtu alishawahi kuwa na tatizo la hivi then akapona anijuze basi!
 
Pole sana Hulida
 
Nani alie pata dawa ya pumu ya ngozi anisaidie
pole sana mkuu,
FANYA HIVI,
Tafuta mafuta ya nazi(coconut oil) yapo maduka ya viungo/ya vipodozi mimi kwa Dodoma nayapata maduka ya wapemba.

Osha kwanza sehemu iliyoathirika,acha pakauke, pakaa mafuta ya nazi asubuhi na jioni
MAELEZO YA TIBA;
Mafuta ya nazi yana nguvu kubwa ktk kurejeshea ngozi fat yake asili iliyoondolewa na pumu ya ngozi.

KAMA KUNA MTU MWENYE PUMU/ASTHMA YA MWILI(KUBANA KIFUA NA KUPUMUA KWA SHIDA ANITAFUTE NINAYO DAWA ASILI YA KUMPONYA KABISA 0656 871878. (50,000/dozi ya wiki mbili)
 
Mimi pia nina tatizo linalofanana na hili. Mwanzoni nilikuwa naambiwa ni allergy and kuna baadhi ya vyakula nikaambiwa nisile lakini tatizo halikuisha coz huwa linakuja kwa muda baadae tena linapotea ila haliishi.

But kuna dr mwingine tena akaja nambia ni pumu ya ngozi na haiponi so niwe natumia tu dawa za kutuliza. Huwa nawashwa ngozi natokewa na vipele vidogo vidogo yaani vikichachamaa ni shida.
Nilishatumia dawa mpaka nikachoka! Kama kuna mtu alishawahi kuwa na tatizo la hivi then akapona anijuze basi!
Pole sana hali kama hiyo ilinitesa sanaa nilihangaika kila kona na ikafika cku nikashangaa nikapona kabisaa hadi leo haijarudi ila sijui nilipona na dawa gani maana nilitumia dawa za hospital ikashindikana nikaanza za kienyeji tofaut tofaut na huko ndiko nilipo ponea
 
Binafsi mwanangu anasumbuliwa sana vinakuja na kupotea nipo nae chini ya dokta mbokomu pale tangi bovu mbezi beach
 
Pole sana hali kama hiyo ilinitesa sanaa nilihangaika kila kona na ikafika cku nikashangaa nikapona kabisaa hadi leo haijarudi ila sijui nilipona na dawa gani maana nilitumia dawa za hospital ikashindikana nikaanza za kienyeji tofaut tofaut na huko ndiko nilipo ponea

Hongera sana, mi bado tatizo halijaisha mpaka leo
 
Unaweza kutuambia dawa za kienyeji ulizotumia?
 
Mtoto wangu mdogo mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi mitatu,Naye anatatizo kama hilo (Eczema),Ngozi inakauka na kuwasha sambamba na vipele vidogovidogo sana usoni.Mwanzo hakuwa na tatizo hilo mpaka alipofikisha miezi nane ndipo likaanza tena ni baada ya kuhama kutoka eneo tulilokuwa tunaishi hapo mwanzo kabla hajazaliwa mpk alipozaliwa tukahama akiwa na miezi name na tatizo likaanzia hapo.,Inavyoonekana ni allergy inayosabishwa kubadili mazingira.Mwanangu anatumia mafuta ya (Baby Johnson) yanaonekana kumsaidia sana pale anapotumia bila kuacha,Nimefuatilia na advices mbalimbali kuhusu mafuta ya nazi (Coconut Oil) pia nitayajaribu.Wito wangu kwa wale wenye tatizo kama hili ambapo huwa wanadai linakuja kisha kutoweka wajaribu kaungalia mazingira wanayoishi maana inasemekana zipo allergy za namna nyingi mno,Ikiwemo allergy ya maua ya miti ama asili ya miti na mimea fulani hivyo kama unaweza kubadili mazingira fanya hivyo ili kuepusha madhara yatokanayo na tatizo kama hili ambalo tiba yake inaonekana ni bahati nasibu.
 
Hongera sana, mi bado tatizo halijaisha mpaka leo
Inasemekana pia tatizo huwa linaisha lenyewe baada muda fulani,Hivyo kutumia dawa sio kwamba ni kumaliza tatizo bali ni kupunguza athari zinazosababishwa na tatizo lenyewe kama vile muwasho,kukauka ngozi na vipele.Hivyo usikate tamaa kama ulishawahi kuonana na wataalamu wa afya wakakupatia dawa itumie kama ulivyoelekezwa tatizo litaisha tu.
 
Back
Top Bottom