Habari, kumekua na malalamiko kwamba wakazi walio karibu na hifadhi/mapori wanavamiwa marakwamara na wanyama tembo. Ifuatayo ni njia rahisi zaidi kuwafukuza tembo kukukaribia!
Kwa kawaida mnyama tembo maisha yake anatumia kunusa mazingira yanayo mzunguka, chakula, adui, jinsia n.k.
Pilipili iliosagwa anaisikia harufu akiwa mbali hivo inamsumbua sana sababu inaharibu uwezo wa kunusa vyanzo vingine.
Tembo hasogei eneo lenye mmea wa pilipili!
Saga unga wa pilipili changanya na kinyesi cha ng'ombe kibichi tengeneza tonge au shepu unayotaka acha ikauke vizuri, kwa matokea mazuri inapochomwa. Au panda miche kadhaa kuzunguka uzio /shamba umevunja urafiki na tembo.