GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,024
- 119,543
Kila Siku za Ibada hapo za Jumapili, Jumatatu, Jumanne na zile za Matamasha Watu / Waumini huibiwa Simu au Pochi kwa Kuporwa huku Wakijeruhiwa na Vibaka Maarufu ambao baadhi yao Mchana huwa ni Madereva Bodaboda katika Ukanda huo.
GENTAMYCINE niliwahi Kumtaarifu hili ( hapa hapa JamiiForums ) aliyekuwa IGP Sirro ( Mzanaki ) Mwenzangu huku nikimtaka amuondoe hapo Mkuu wa Kituo cha Polisi Kawe na awahamishe Polisi Wote kwani hakuna Wakifanyacho na kuna baadhi yao wanashirikiana na hao Vibaka ila hakuna alichokifanya.
Haya na leo tena kwakuwa Wazanaki tuna bahati ya kuwa Viongozi na kupata Vyeo vya Taasisi Nyeti za Ulinzi na Usalama kutokana na Akili, Uweledi, Kujiamini, Uaminifu, Ukwel, Uthubutu na kutokuwa Wanafiki namtaarifu tena IGP Wambura ( Mzanaki Mwenzangu Mwingine ) kuwa Pori la Tanganyika Packers Kawe ( Msitu ule Mkubwa ) sasa ni Eneo HATARISHI na hali imekuwa ni Mbaya kwa Waumini na Beach Goers ( Waenda Baharini Kuburudika ) hivyo hatua za Kudhibiti UHALIFU HATARI wa hapo zichukuliwe haraka.
IGP Wambura sijajua kama Ulitaarifiwa hili ila Miezi kadhaa kuna Maiti Mbili za Mwanaume na Mwanamke ziliokotwa hilo Eneo kwa kinachoaminika kuwa walikuwa wakitoka Baharini ( Beach Kawe ) na wakiwa wanarejea njia ya nyuma ulipo Ukuta wa Tanganyika Packers wakavamiwa huku Mwanamke Akibakwa na Vibaka Wengi Waliokuwa na Mwanaume alipojaribu Kumtetea ( Kumpambania ) huku Mwanamke nae akijaribu Kujinasua Wakajeruhiwa vibaya hadi Kufa.
Pia IGP Wambura hilo Pori ( Msitu huo ) wa Tanganyika Packers Kawe sasa umekuwa ni sehemu ya Watu Kujiua kwa Kujinyonga lakini pia Wahalifu huwauwa Watu maeneo mengine na kuja Kuwatupa hapo.
IGP Wambura hilo Eneo Hatarishi la Msitu huo wa Tanganyiika Packers Kawe kuna mpaka Mahandaki ya Dharula ya Wahalifu ( Vibaka hao ) kuficha Vitu vyao na pia kuwa ni Gesti / Loji zao kwa Wanawake ambao huwa Wanawateka na Kuwatapeli hasa Nyakati za Usiku wa Siku hizo tajwa za Ibada.
Kinachonishangaza zaidi GENTAMYCINE ni kuona Mtume Mmoja wa Eneo hilo amekaa Kimya na hailisemi Kwenu wakati 85% ya yanayowakuta ni Waumini wake mpaka Mimi PATRIOTIC AND CONCERNED CITIZEN GENTAMYCINE nije kulisema hapa ili mjue.
Halafu IGP Wambura kinachonishangaza na hadi kunitia HASIRA zangu Kali na Tukuka za Kizanaki + Kimakuwa ni kuona Askari wako wa Kawe Police Station na Gari yao Land Cruiser wakiwa busy Kugombania hadi Kurogana ili tu wawepo katika Mkeka ( List ) ya kwenda Kumsindikiza ( Escort ) Mtume wa Tanganyiika Packers Kawe kwa Maagizo ya Mkuu wao wa Kituo ili wapewe Pesa za Asantee Tsh 150,000/= kila Mmoja na Mkuu wao akipewa yake Tsh 300,000/= ila Kupanbana na hawa Wahalifu ( Vibaka ) HATARI wa Msitu ( Pori hilo ) la Tanganyiika Packers Kawe wanashindwa na wala hawana muda huo.
Kama vipi IGP Wambura kama mmewashindwa hawa Wahalifu ( Vibaka ) HATARI katika hilo Pori ( Msitu wa Tanganyiika Packers Kawe ) basi wapeni Watoto wa Komando CDF Gen. Mkunda ( JWTZ ) ili Wawafyagie ndani ya Siku Moja mpaka Tatu ili hilo Eneo liwe Salama kwa kila Mtu tofauti na lilivyo sasa ambako inawalazimu Watu kupita njia za mbali sana ili waweze Kufika Makwao.
Ninachopendea hasa Patrols za JWTZ ( hasa walioko Jirani na Makazi ya Watu ) ni kwamba ama Wakiibiwa Wao au Wakiombwa Kuwadhibiti huwa hawaangalii Wewe ni sijui GENTAMYCINE wa JamiiForums au Mama au Bibi au Baba au Babu au Kijana bali hutembeza Msako na Kichapo Kitakatifu ( cha Kishalubela ) kiasi nyie Wenyewe ( Raia ) mnaenda Kuwahamisha hao Vibaka ( Wahalifu ) na kupelekea Eneo zima kuwa Salama na Adabu juu.
IGP Wambura lifanyie hili Kazi sawa?
Pia soma:
- Dar: Wahalifu wadaiwa kutumia jina la ‘Ulinzi Shirikishi’ kufanya uhalifu maeneo ya Tanganyika Packers
- Serikali ya Mtaa Kawe: Kweli kuna kundi la Wahalifu wanatumia kivuli cha Ulinzi Shirikishi, wanatuchanganya sana