A
Anonymous
Guest
Mimi ni kijana ambaye ninajishughulisha na shughuli halali za kawaida na ninajipatia kipato halali, ninaomba niwasilishe kilichotokea mtaani kwetu Mkoa wa Katavi, Kitongoji cha Makanyagio Mjini Mpanda mnamo tarehe 3 Aprili 2024.
Tukiwa mtaani hatuna hili wala lile, watu wakiwa wanaendelea na Maisha kama kawaida, majira ya saa mbili usiku, ghafla gari mbili za Polisi ambao baadaye tulijua kuwa walikuwa Askari wa Doria, moja ikiwa imeandikwa OCD na nyingine imeandikwa POLICE MPANDA, ziliwasili kwa kasi eneo hilo.
Baada ya gari kupaki, Askari kadhaa walishuka na kuanza kuwapiga Wananchi kwa fimbo, marungu na waya bila sababu yoyote.
Kibaya zaidi waliwavami hadi Wanawake ambao walikuwa wanapita na 50 zao, wakavamia kijiwe flani cha Mama Lishe waliokuwa jirani hapo na kuanza kutembeza kichapo.
Ilibidi kuibuke kama sekeseke flani maana hamna taarifa ghafla mnaanza kuchapwa tena na waya, hata wale ambao tulikuwa kwenye vibalaza vyetu vya nyumbani tukaanza kuchapwa, kilichokuwa kinakuokoa ni mbio zako.
Moja ya jeraha lililotokana na kichapo cha waya
Baada ya kuona watu wamesambaa na wamewaumiza wengine wengi tu Askari hao bila maelezo wakaingia kwenye magari yao na kuondoka.
Huku nyumba asilimia kubwa ya waliochapwa walikuwa na hali mbaya kutokana na majeraha, kichapo cha waya kisikie tu ndugu, mimi nilipichapwa fimbo mbili, nikaona nyotanyota.
Baada ya kuondoka Wananchi tukajikusanya na kuanza kuhojiana kulikoni, hatukupata jibu, baadhi wakaondoka zao hawakutka shida zaidi, wengine wakenda kuripoti Kituo cha Polisi Kati, kufika huko maelezo yakatolewa na Wananchi wakaomba PF3 ili waende hospitali.
Mkuu wa kituo aliyekutwa akasema yeye amekaimu tu, alioombwa PF3 akagoma kutoa.
Wananchi wakarejea hadi kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mtaa wa Makanyagio ya Pinda ambao pia ni maarufu kwa jina la Fimbo ya Mnyonge, kumjuza, mimi sikwenda kwa kuwa niliona isiwe tabu ngoja nisikilize wenzangu.
Waliporudi tukaongozana hadi kwa Mwenyekiti kumjulisha kila kilichotokea, baada ya hapo Polisi Kituo cha Mpanda hakijawahi kutupa PF3 wala huduma yoyote, kibaya zaidi ni kuwa Askari waliotuchapa Wananchi bila sababu wapo kituoni hapo na tukienda tunawakuta, Mkuu wa Kituo ameoneshwa kuwa ni fulani na fulani lakini hakuna kilichofanyika, wanalindana.
Tulichokuaja kusikia baadaye ni kuwa kuna kitongoji ambacho sio hapa kwetu kuna mauaji yakitokea, sasa katika kufuatilia hasira zao wakaja kuzibalizia kwa Wananchi tusiokuwa na hatia.
Hii sio sawa, Kamanda Mkuu wa Polisi Katavi na IGP huu uonevu unatakiwa kuchukuliwa hatua vinginevyo hao Askari wenu watarejea tena kufanya unyanyasaji mkubwa zaidi ya huu.
Viongozi wa Kituo cha Polisi Kati Mpanda wanawalinda Askari wao wa chini wanaofanya upuuzi.