IGP Mangu asema Lugumi alitekeleza Mkataba

Fabian the Jr

JF-Expert Member
Aug 4, 2012
756
743
IGP ERNEST MANGU:LUGUMI ILITEKELEZA MKATABA WAKE NA JESHI LA POLISI.

Mkuu wa Jeshi la Polisi – Inspekta Jenerali (IGP), Ernest Mangu amekanusha madai ya wabunge na hata taarifa zinazosambaa mitandaoni na kwenye vyombo vya habari kuhusu kampuni ya Lugumi kushindwa kufunga mashine kwenye vituo vya Polisi 108 kama mkataba wake ulivyomtaka.

Akizungumza mwishoni mwa wiki, IGP Mangu alisema anashangazwa na habari hizo na kueleza kuwa kampuni ya Lugumi ilitekeleza mradi wa kufunga mashine hizo kama ilivyokubaliana na serikali. “Siyo kweli, watu wana ugomvi wao, lakini nakueleza wazi kwamba, tembelea vituo vyote tulivyokubaliana, utakuta mashine zipo. Inawezekana zingine hazifanyi kazi kwa sababu ya kukosekana kwa intaneti,” aliongeza mkuu huyo wa polisi.

Alipoulizwa mwenye jukumu la kufunga mtandao wa intaneti ni nani, IGP alijibu, “...ni TTCL (Kamuni ya Simu) ingawa sehemu nyingi ofisi zetu zimekatiwa huduma hiyo kwa kuwa jeshi halijalipa.”
 
Hakuna raia atakae comments hapa wanaogopa kuwekwa rupango.Magufuli na ukali wake wote hapo kakwama na hata bunge nalo bado linachemka na Lugumi.
 
Kwa hiyo CAG Prof Asad alitoa taarifa ya uongo. Basi kuna haja ya kuanika nani anastahili kufutwa kazi, Asad au Mangu kwa sababu mmoja wao anasema uongo na JPM hataki uongo hasa katika ofisi nyeti kama IGP na CAG.
 
!
!
Hii selikali ni ya viwanda. Hayo ya Lugumi sijui mashine sijui nini subirini uchaguzi ujao.
Selikali ya Magufuli ni ya viwandaa haki ya Mungu nasema kweli, naomba mniombee.
 
Kwanini jeshi halijalipa internet?

Wanafanyaje kazi zao? Uchunguzi unafanyikaje?
 
Najaribu kukumbuka habari ya Jana ya Mwananchi juu kufungwa sasa kwa hizo Machine na hii kauli ya IGP, nnasikia kizunguzungu!
 
Huyu IGP anatakiw awe mwangalifu hii Lugumigate italamba watu wengi sana. Imeshaanza na kitwanga pamoja na kelele zake. Huwezi ukatetea Lugumi na kubaki salama.
 
LUGUMI Ilitekeleza au Inatekeleza?
Uzi huu ni kaa la moto kwa nyumbu wote na vyura wa ukawa wamepoteana
IGP amezungumzia nini kuhusu haya madai kwamba mashine hizo ndio bado zinafungwa kimyakimya?
Link Sinema sakata la LUGUMI: Mashine za utambuzi wa alama za vidole zaanza kufungwa kimya kimya
Najaribu kukumbuka habari ya Jana ya Mwananchi juu kufungwa sasa kwa hizo Machine na hii kauli ya IGP, nnasikia kizunguzungu!

Ipo kitu inafichwa au "mashine hizo zinazofungwa Dodoma na Geita" ziliharibika na zinafanyiwa matengenezo?

Link Sarakasi ya sakata la Lugumi yaendelea

Link KASHFA NDANI YA JESHI LA POLISI: Waziri Kitwanga aikana Lugumi
 
Najaribu kukumbuka habari ya Jana ya Mwananchi juu kufungwa sasa kwa hizo Machine na hii kauli ya IGP, nnasikia kizunguzungu!

tusubiri kauli ya rais na taarifa kutoka kamati ya bunge...

na wasiwasi na baadhi ya wajumbe wa kamati za bunge. wengine ni bado ni waumini wa rushwa na ufisadi...
 
Wabunge wa kamati ya Bunge ambao wameanzia Morogoro wamesema kwamba Moro hakuna hata mashine moja iliyofungwa kule. Kwa hiyo Mangu kudai kwamba vituo vyote 108 mashine zilifungwa aliudanganya umma wa Watanzania.


Hivi igp naye kawa mwana siasa?

Angetoa taarifa na orodha ya kila kituo na idadi ya mashine zilizofungwa....
 
Uzi huu ni kaa la moto kwa nyumbu wote na vyura wa ukawa wamepoteana

Hapa wahanga no wote, haijalishi uko chama gani. Hata hivyo huu Uzi ni kaa la moto kwa CCM na IGP mwenyewe, haihitaji kuumiza kichwa kujua kwamba kadanganya umma.

Kama mkataba ulitekelezwa kwa wakati, kigugumizi cha kuutoa huo mkataba kwa kamati ya bunge kilitoka wapi? Taratibu za manunuzi zilifuatwa? Mambo mengine jaribu kuweka ushabiki wa vyama pembeni mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…