Serikali imesema imepokea ombi la chuo cha usimamizi wa Fedha cha (IFM) la kutaka kupandishwa hadi kuwa chuo kikuu kutokana na kukidhi vigezo
Aidha, Serikali imeahidi kulifanyia kazi ombi hilo kwa kushirikiana na wadau wengine ili kufanikisha jambo hilo bila kupindisha utaratibu wa Serikali
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Vijana Dk. Anthony Mavunde wakati akizindua Baraza la Tisa la wafanyakazi wa chuo hicho
"Sishangazwi na ombi letu la kuwa chuo kikuu, nimelichukua na naahidi kuwasiliana na wadau wengine wa Serikali tuone njia bora ya kuliendeleza bila kupindisha taratibu"alisema Mavunde
Pia alitaka Baraza hilo jipya kufanya kazi kwa bidii na kuhakikisha wanatekeleza mipango waliojiwekea ambayo inaendana na mipango ya Serikali
Chanzo: HabariLeo