Ifahamu vyema mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro (Ngorongoro conservation area authority NCAA)

Steven mushi mushi

JF-Expert Member
Jul 25, 2016
533
739
Inawezekana kwa namna moja au nyingine unaifahamu hifadhi lakini kuna baadhi ya vitu hivijui kuhusu hii hifadhi au ikawa unaiskia tu lakini huijui kiungani hebu tiririka nami nikuelezee kinagaubaga kuhusiana na hifadhi hii ya ngorongoro. Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro (Ngorongoro conservation area NCAA) ilianzishwa mwaka 1959 na ina ukubwa wa kilometa za mraba 8300sqkms, hapo awali kabla ya kuanzishwa kwake ilikuwa imeungana na hifadhi ya taifa ya Serengeti na ilikuwa ikifahamika kama great Serengeti na baadaye zikatenganishwa moja ikawa national park ambayo ni Serengeti na nyingine ikawa hifadhi mseto(Conservation) ambayo ni ngorongoro. Mamlaka ya hifadhi ya ngorongoro pia ni moja kati ya maeneo ya urithi wa dunia na pia ni moja kati ya maajabu saba ya dunia na hii ni kutokana na upekee wake iliyokuwa nayo ambapo ni pamoja na upatikanaji wa fuvu la kwanza la binadamu wa kale ambaye aliishi ndani ya ngorongoro kipindi cha miaka million 1.7 iliyopita na fuvu hili linapatikana Olduvai george, pia sababu nyingine iliyopelekea ngorongoro kuwa maajabu saba ya dunia ni pamoja na bonde la ngorongoro ( Ngorongoro crater ) pamoja na ile hali ya wanyama pori kuishi na binadamu kwa wakati mmoja bila kuthuriana, sababu nyingine ni uwayo wa binadamu wa kale ( Laetoli footprint ) ambao unapatikana ndani ya Olduvai george na kutokana na sababu hizi UNESCO ikaifanya ngorongoro kuwa moja kati ya maeneo ya urithi wa dunia mnamo mwaka 1979. Pia mamlaka ya hifadhi ya ngorongoro ni hifadhi inayojitegemea yenyewe haipo chini ya national park na sababu kubwa inayopelekea ngorongoro isiwe national park ni uwepo wa binadamu wanaoishi ndani ya hifadhi na mifugo wao pamoja na wanyama pori kwa wakati mmoja tofauti na national park ambapo ni wanyama pori pekee wanaoruhusiwa kuishi pia ndani ya mamlaka ya hifadhi ya ngorongoro shughuli zote za kijamii zinafanyika tuna shule, makanisa, misikiti, maduka, baa, grosery pamoja na hospital na ni shughuli moja pekee ya kilimo ambayo hairuhusiwi ndani ya hifadhi lakini shughuli nyingine zote zinafanyika. Kabila la wamasai ndo kabila pekee linaloishi ndani ya hifadhi na kabila hili limeishi ndani ya ngorongoro kwa zaidi ya miaka 150 iliyopita na kabila hili limerihusiwa kuishi ndani ya hifadhi kutokana na wao kutokula nyama pori pia wamekuwa moja kati ya kivutio cha utalii ukiachana na crater kwa sababu wageni huja kutizama jinsi binadamu anavyoishi na wanyama pori kwa wakati mmoja bila kuthuriana yaani wanaishi peacefully maana dunia nzima ni ngorongoro pekee binadamu anaishi na mnyama pori. Tuje kwenye asili ya neno ngorongoro, Neno ngorongoro ni neno la kimasai engorongoro na kuna sababu nyingi iliyopelekea eneo hili kuitwa ngorongoro, sababu ya kwanza kuna wajerumani wawili Bernad na Michael Bismark ambao walikuwa ni Baba na mtoto hawa walikuwa wanafanya research za milima na vipepeo kutoka Serengeti kuja ngorongoro na walipofika ngorongoro walikuta wenyeji ambao ni wamasai na hawa wajerumani walikuwa na mkalimani wao baada ya kufika yule mkalimani akawauliza wale wamasai eneo hili linaitwaje wakamwambia linaitwa engorongoro wakimaanisha bonde (wamasai wanaita bonde engorongoro) yule mkalimani akawaambia wale wajerumani wamesema hapa panaitwa engorongoro maana yake bonde wale wazungu wakashindwa kutamka engorongoro wakatamka ngorongoro na hapo ndipo neno ngorongoro lilipoanzia pia kuna sababu nyingine nyingi silizopelekea eneo hili kuitwa ngorongoro nyingine ikiwa ni zile kengele wanazofungiwa ng'ombe wa kimasai ambazo zinatoa mlio wa ngoro ngoro wakati wa kutembea ndiposa hili eneo likaitwa ngorongoro. Pia zamani wamasai walikuwa wanaishi ndani ya crater baadaye wakaja wakahamishwa na leo hii wanapatikana nje ya crater ingawa kule huruhusiwa kushusha mifugo wao kuwalisha na kuwanywesha maji hasahasa kipindi cha kiangazi kwenye ziwa linalopatikana ndani ya crater ambalo linaitwa ziwa makati (Alkaline lake ). Kwa upande wa vifutio vya utalii ndani ya ngorongoro vipo vingi ikiwemo ngorongoro crater ambayo kwa kawaida ni caldera na sio crater, ngoja nikupe tofauti kati ya crater na caldera. Kuna tofauti kati ya crater na caldera tofauti ya kwanza ni kuwa crater inafomdiwa juu ya mlima tofauti na caldera na kwenye crater hakuna viumbe hai vinavyoishi tofauti na kwenye caldera ambapo viumbe hai Wanaishi kwa hiyo ngorongoro crater iko misnamed ile ni caldera na ndio maana hata wageni wakija ngorongoro tunawafafanulia na kuwaelimisha tofauti kati ya crater na caldera kwa hiyo ilipaswa kuwa ngorongoro caldera na sio ngorongoro crater Kama inavyoitwa, pia ukiachana na ngorongoro caldera tunavifutio vingine vya utalii ambavyo ni pamoja na Olduvai George ambapo linapatikana fuvu la kwanza la binadamu wa kale, laetoli footprint (uwayo wa binadamu wa kale), shifting sand (mchanga unaohama na inakadiriwa kuwa huu mchanga unahama mita 17 kila mwaka ) pamoja na oldonyo lengai ambo ndio mlima pekee wenye volkano iliyo hai Tanzania pia ukiachana na ngorongoro caldera ngorongoro kuna takribani crater sita ambazo kiuhalisia ni crater sita na caldera tatu ambazo ni ngorongoro caldera, olmoti caldera na empakai caldera na pia ndani ya ngorongoro caldera pekee ambapo kuna fanyika shughuli ya game drive( kutumia gari kuzunguka ndani ya crater na kutizama wanyama ) lakini kwa upande wa hizi zilizobaki tunafanya shughuli za matembezi kwa njia ya miguu (Walking Safari ) lakini kwa kawaida kwenye walking Safari unakuwa chini ya askari wa wanyama pori(park ranger ) na tunafanya walking kwenye hizi nyingine zimezungukwa na maji kwa hiyo hakuna sehemu ya gari kupita kama ndani ya caldera ambayo wengi wanaita crater. Na hii ngorongoro crater ilitokea zaidi ya miaka million 2 iliyopita baada ya mlima uliokuwa mrefu ndani ya eneo hili kulipuka na kutitia kutokana na volkano na kutengeneza kitu chenye shape kama garai ambacho ndio ngorongoro crater na ukubwa wa crater ni km260 kwa ile flow ya chini ambapo ndipo wanyama wanapoishi, urefu wake kutoka juu hadi chini ni 610 meters na mzunguko wa juu (crater rim size ni km 310) kwa hiyo hii crater ina shepu kama garai ndo maana juu ni kubwa kuliko chini kama ilivyo garai. Na kwa upande wa wanyama tunasema ngorongoro is home of big five (wanyama wakubwa watano Africa ) ambao ni simba, nyati(mbogo), faru (rhino ) tembo na chui na hawa wanyama waliitwa big five na walewawindaji wa wazami kutokana na kupata wakati mgumu pindi walipokuwa wakiwawinda hawa wanyama na sababu nyingine iliyopelekea kuitwa big five ni kutokana na trophy zao kuwa na thamani kubwa mfano meno kwa upande wa tembo, pembe kwa faru na ngozi kwa simba na chui pia ukiachana na hawa wanyama ambao ni big five ngorongoro kuna aina nyingine nyingi za wanyama ikiwemo nyumbu, pundamlia, swala tomi, fisi, mbweha, na aina nyingi za wanyama ambao utabahatika kiwaona pindi ukitembelea hifadhi hii na pia kuna baadhi ya wanyama ambao hawapatikani ngorongoro ni pamoja na impala pia Topi ambao wanapatikana Serengeti pia kuna baadhi ya wanyama ambao wapo ndani ya ngorongoro lakini hawapatikani ndani ya crater kama twiga na majike wa tembo pamoja na watoto wao ambao wao unawapata kwenye ukingo wa bonde kutokana na mazingira yao kitowaruhusu kuishi ndani ya crater vile vile tuna aina nyingi za ndege ikiwemo mbuni, tandawala, ndege John na wengine wengi pia kwa wale wageni watakaopenda kulala ndani ya hifadhi ndani ya hifadhi tuna lodge nyingi kama ngorongoro crater lodge, Serena hotel rhino lodge na nyinginezo pia tuna sehemu za camping Kama simba na nyati kwa wale watakaohitaji. Hiyo ndo ngorongoro mzazi moja kati ya maajabu saba ya dunia pia kama hujawahi fika ngorongoro unaweza ukaanza kujipanga na kuweka akiba kidogokidogo kwa ajili ya kuja kutembea siku moja na kwa upande wa watalii wa ndani kuingia hifadhini unalipia tu1500 just imagine ila kingine utakachopaswa kulipia ni gari lako iwapo utaamua kutumia gari lako binafsi pia kuna gari maalamu kwa ajili ya watalii wa ndani kwa hiyo mnaweza mkaungana kikundi cha watu kadhaa mkachangisha kwa ajili ya kuja kutembelea hifadhi ya ngorongoro ila kwa upande wa gari la watalii wa ndani mnafanya booking kwanza ndio muende. Ni sehemu nzuri sana kwa ajili ya kutembea na kujifunza mambo mengi kuhisiana na nchi yetu Tanzania!!!!!!!!
 
Asante sana mtoa mada,nilistaajabu sana nilvyoona jinsi barchan(shifting sand) inavyo ama uku ikimaintain shape yake.
 
Angekuja kujibu maswali uzi ungenoga sana sasa hapa ni kama amecopy kitabu akapaste na ndio udhaifu wa fasihi andishi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…