Ifahamu Sekta ya Mafuta na Gesi Tanzania- Sehemu ya Kwanza (Utangulizi)

Chige

JF-Expert Member
Dec 20, 2008
13,495
29,859
Ili niweze kugusia kila eneo, basi makala hii itakuwa na sehemu angalau tatu ambazo ni Utangulizi, Sera, Sheria na Kanuni zinazoongoza sekta hii, na sehemu ya mwisho fursa zilizopo.

Kwa kuanza, naweza kuiweka Gesi ya Tanzania kwenye makundi makuu mawili. Kundi la kwanza ni ile ambayo ugunduzi wake ulitokea wakati wa Awamu ya Kwanza, na kundi la pili ni ile ambayo ilianza kugundulika kwa wingi kuanzia Mwaka 2010.

Gesi ya Kundi la Kwanza inajumuisha gesi Gesi ya Songosongo kutoka mkoani Lindi, na ya Msimbati, mkoani Mtwara.

Hii Gesi ya Msimbati ndo ile ambayo ilizua kizaa zaa wakati wa JK..

Jumla ya gesi YOTE, yaani iliyogundulika Awamu ya Mwalimu na ile iliyogundulika awamu ya JK ni zaidi ya Futi za Ujazo TRILIONI 57; yaani 57 Trillion Cubic Feet (TCF).

Kati ya hizo, 7.5 Trillion Cubic Feet ziligunduliwa wakati wa Mwalimu na takribani 50 Trillion Cubic Feet ziligunduliwa wakati wa JK.

Aidha, ifahamike kwamba, kati ya zaidi ya 57.5 TCF ya gesi iliyogundulika, hadi sasa iliyoanza kuchimbwa ni ile TU ambayo Iligundulika wakati wa Mwalimu. Kwa maana nyingine, gesi ambayo ipo kwenye mzunguko wa kuzalisha umeme hivi sasa inatokana na zile 7.5 TCF, na zaidi ya 50TCF zilizogundulika wakati wa JK bado HAIJAANZA KUCHIMBWA!

Pia ifahamike kwamba, kiwango kikubwa cha gesi hii imegundulika kwenye Kina Kirefu cha Bahari. Na nikisema kina kirefu, ni kirefu hasa. Kwa ujumla, kati ya 57.5TCF ya gesi iliyogundulika, takribani 47 TCF inapatikana kwenye kina kirefu cha bahari ya Pwani ya Lindi na Mtwara.

Kwa mfano, ripoti zinaonesha kwamba Kitalu No. 1 kipo zaidi ya 100Km kutoka ufukweni na Kitalu No. 4 kipo takribani 200Km kutoka ufukweni.

Aidha, gesi yenyewe ipo takribani 1Km chini ya uso wa bahari (yaani, below water surface).

Pengine, hiyo ndio sababu hata gharama za ujenzi wa Kiwanda cha Kuchakata Gesi Asilia (LNG) pale Lindi ni KUBWA MNO kwa sababu, gesi inatarajiwa kuchimbwa angalau 1 Km chini ya uso wa bahari kisha kusafirishwa kwa mabomba kwa zaidi ya 100km hadi nchi kavu kitakapojengwa kiwanda cha uchakataji.

Pia, si mbaya tukifahamu vitalu vyetu vipo chini ya akina nani.

Kitalu No. 1 na No. 4 vipo chini ya Shell (exploration concession 60%), Kampuni ya Pavilion Energy (20%), na PT Medco Daya Abadi Lestari (20%).

Shell Tanzania ndie Operator wa Kitalu husika.

Ifahamike kwamba, Shell Tanzania ni Kampuni ya Kidachi, Pavilioni Energy ni kampuni tanzu ya Temasek Holdings Limited, na Temasek Holdings Limited ni kampuni ya Serikali ya Singapore!

Aidha, PT Medco Daya Abadi Lestari ni kampuni ya Kiindonesia inayomilikiwa na Familia ya The Panigoro, na mwanzilishi wa kampuni hiyo ni Arifin Panigoro ambae amefariki February 2022.

Kwa ujumla, Kitalu No.1 na Kitalu No. 4 vina takaribani 17 TCF of natural gas reserve.

Kwa upande mwingine, Kitalu No. 2 kinaendeshwa na kampuni ya Equinor na ExxonMobil.

Equinor, ambayo zamani ilikuwa inafahamika kama Statoil ni kampuni kutoka Norway huku shareholder mkubwa akiwa Serikali ya Norway yenye hisa 67%, huku ExxonMobil ikiwa ni kampuni kutoka Texas, Marekani.

Kitalu hiki No. 2 kinakadiriwa kuna na zaidi ya 20 TCF. Na kama ilivyo kwa vitalu vingine, Kitalu No. 2 kipo umbali wa takribani 100Km kutoka Pwani ya Lindi, na gesi inapatikana takribani 2Km kutoka uso wa bahari (2km below water surface)

REMEMBER: Umiliki huo hapo ni Umiliki uliotokana na leseni ya Utafutaji wa Gesi lakini kwa Mujibu wa Sheria ya Mafuta na Gesi ya Mwaka 2015, Mmiliki HALISI wa Vitalu husika ni National Oil Company (For now, TPDC).

Jambo lingine ambalo watu wanatakiwa kulifahamu ni kwamba, hadi kufikia sasa, kiwango kikubwa cha gesi kimegundulika Mkoani Lindi na sio Mtwara kama ambavyo wengi wanadhani.

Aidha, tumepata kusikia hapa na pale kwamba Gesi YOTE ameuziwa Mchina! Na kama nilivyosema hapo juu, hizo kampuni za kigeni zilipewa leseni ya Utafutaji na sio UCHIMBAJI.

Hadi hivi sasa, HAKUNA kitalu chochote KILICHOUZWA kwa ajili ya uchimbaji. Endapo utaratibu utafuatwa, Vitalu husika vitapaswa kupigwa mnada na wale watakaoshinda ndio watapewa leseni za UCHIMBAJI.

Kuhusu nani atapata nini kati ya Serikali na Mwekezaji, hilo tutajadili kwenye Sehemu ya Pili ya mada hii ambapo tutaangazia Sera, Sheria, Kanuni na Model Production Sharing Agreement.

Hapo kwenye Model Production Sharing Agreement ndo hasa patakapotoa au kuua maslahi yetu. Kwa sasa, MPSA iliyopo ni ya 2013 ambayo kuna taarifa zinadai kwamba Wawekezaji HAWAITAKI!
 
Umeanza vizuri Ila umepuyanga mwishoni Kama kawaida yako.
Kufanya exploration ni gharama kubwa, yaani ufanye expolaration alafu kwenye uchimbaji usihusike? Uchimbaji akipewa mwingine, wewe zile cost za expolaration unazirudishaje? Ukielewa kwa nn anayefanya tafiti atafaidika na uchimbaji pia ndio hasa utarudi kwenye ukweli wa uzi wako
 
Wapi nimesema ukifanya exploration kwenye uchimbaji huusiki?!

Na kama unahoji gharama za exploration anarudishaje basi inaonesha unatakiwa kujifunza mengi kwa sababu hata leo, kampuni iliyofanya exploration, inaweza kuuza haki zake kwa kampuni nyingine kama ambavyo BG au Ophir walifanya.

Halafu eti kama kawaida yako! Juzi nilikuuliza ni wapi nimesema uongo lakini ukakimbia lakini kwa hoja yako hiyo inaonekana una matatizo ya kuelewa kinachoandikwa!
 
Unaona sasa ulivyo umeanza kwa kusema wamepewa tafiti tu na sio uchimbaji, alafu hapo unakuja tena kusema hakuna sehemu umesema kwenye uchimbaji hawahusiki, Kama ukimpa mtu exploration na uchimbaji akahusika. Akachimba gesi alafu akakuuzia, hapo utasemaje gesi haijauzwa?

Ofcourse haijauzwa kama vile watu wanavyodhani mkate unavyouzwa, Ila kwa kuwa hatuna uwezo wa kufanya yote hayo hatuna budi kuwaacha wafanye tafiti, wachimbe na watuuzie( sijui sasa Kama hii ni tafsiri ya gesi Kuuzwa).

Katika hili eneo hakuna kitu utaniongopea, amini hivyo kwanza. Alafu ukija kuleta hoja ziwe na mashiko.

Mada ya juzi, sikutaka tu kufanya mjadala uwe mkubwa na kuweka mambo ya watu wengine in public kwa watu wote nawapenda na kuwaheshimu Ila hiyo isiwe sababu ya nyie wachache kuujua ukweli na kuusema alafu humo humo kwenye ukweli mnachomekea na propaganda zenu Kama unavyotaka kufanya hapa.
 
Unaona sasa ulivyo umeanza kwa kusema wamepewa tafiti tu na sio uchimbaji, alafu hapo unakuja tena kusema hakuna sehemu umesema kwenye uchimbaji hawahusiki, Kama ukimpa mtu exploration na uchimbaji akahusika. Akachimba gesi alafu akakuuzia, hapo utasemaje gesi haijauzwa?
HUELEWI....

Nimekuambia leseni zilizotolewa ni za UTAFUTAJI. Zipo kampuni ambazo zili-invest kufanya UTAFUTAJI na ZIKAGUNDUA gesi.

Baada ya hapo, kwa sababu wanazojua wenyewe, wakauza ile haki walizokuwa nazo kwenye leseni za UTAFUTAJI, na haki hizo zikanunuliwa na wengine kwa matarajio, endapo watapata fursa ya uchimbaji waendelee na shughili husika, lakini pia hata wao wakiona kwenye uchimbaji hakuna maslahi, wanaweza kuuza hizo haki zao!
Ofcourse haijauzwa kama vile watu wanavyodhani mkate unavyouzwa, Ila kwa kuwa hatuna uwezo wa kufanya yote hayo hatuna budi kuwaacha wafanye tafiti, wachimbe na watuuzie( sijui sasa Kama hii ni tafsiri ya gesi Kuuzwa).
Mbona Hueleweki!

Hapo juu umeona suala la kuuza haki ya leseni ya utafutaji ni sawa na kuuza gesi yenyewe halafu hapa tena unasema "of course, haijauzwa"!

Acha kufanya assumptions.
Katika hili eneo hakuna kitu utaniongopea, amini hivyo kwanza. Alafu ukija kuleta hoja ziwe na mashiko
Mtu anayejua hawezi kuongea ulichoongea...
.Mada ya juzi, sikutaka tu kufanya mjadala uwe mkubwa na kuweka mambo ya watu wengine in public kwa watu wote nawapenda na kuwaheshimu Ila hiyo isiwe sababu ya nyie wachache kuujua ukweli na kuusema alafu humo humo kwenye ukweli
Kuna mtu yeyote ambae alikashifiwa kwenye ile mada hadi useme "huwezi kuweka mambo public kwa sababu unawaheshimu na kuwapenda"?
mnachomekea na propaganda zenu Kama unavyotaka kufanya hapa.
Unaweza kutaja hizo propaganda nilizotaja hapa ni zipi au ni ipi?!
 
Umiliki huo hapo ni Umiliki uliotokana na leseni ya Utafutaji wa Gesi lakini kwa Mujibu wa Sheria ya Mafuta na Gesi ya Mwaka 2015, Mmiliki HALISI wa Vitalu husika ni National Oil Company (For now, TPDC).

***hi Nchi Wabunge kazi yao kupiga makofi,hivi huyo TPDC atakuwaje mmliki huku hana capital yoyote aliyo contribute???
TPDC tukubali tu ni msimamizi.
 
Hilo litajibika kwenye mada itakayojadili Sheria ya Mafuta na Gesi pamoja na kanuni zake!
 
Hadi hivi sasa, HAKUNA kitalu chochote KILICHOUZWA kwa ajili ya uchimbaji. Endapo utaratibu utafuatwa, Vitalu husika vitapaswa kupigwa mnada na wale watakaoshinda ndio watapewa leseni za UCHIMBAJI

*** Mkuu sijui ulikiwa una manisha nini kwenye hiyo statement hapo juu-maana hadi sasa tunatumia gas na ina chimbwa au una manisha vitalu vilivyohunduliwa wakati wa Kikwete?
 
Umeanza vizuri Ila umepuyanga mwishoni Kama kawaida yako.
Kufanya exploration ni gharama kubwa, yaani ufanye expolaration alafu kwenye uchimbaji usihusike? Uchimbaji akipewa mwingine, wewe zile cost za expolaration unazirudishaje? Ukielewa kwa nn anayefanya tafiti atafaidika na uchimbaji pia ndio hasa utarudi kwenye ukweli wa uzi wako
Mkuu ni sahihi kwenye mafuta,gas na Madini utafiti wa uwepo wa rasilimali unaweza ukafanywa na Kampuni X na uchimbaji ukafanywa na Kampuni Y.
 
Hadi hivi sasa, HAKUNA kitalu chochote KILICHOUZWA kwa ajili ya uchimbaji. Endapo utaratibu utafuatwa, Vitalu husika vitapaswa kupigwa mnada na wale watakaoshinda ndio watapewa leseni za UCHIMBAJI

*** Mkuu sijui ulikiwa una manisha nini kwenye hiyo statement hapo juu-maana hadi sasa tunatumia gas na ina chimbwa au una manisha vitalu vilivyohunduliwa wakati wa Kikwete?
Ndo JIBU, kwa sababu ile ya Songosongo na Msimbati tayari inachimbwa!
 
HUELEWI....

Nimekuambia leseni zilizotolewa ni za UTAFUTAJI. Zipo kampuni ambazo zili-invest kufanya UTAFUTAJI na ZIKAGUNDUA gesi.

Baada ya hapo, kwa sababu wanazojua wenyewe, wakauza ile haki walizokuwa nazo kwenye leseni za UTAFUTAJI, na haki hizo zikanunuliwa na wengine kwa matarajio, endapo watapata fursa ya uchimbaji waendelee na shughili husika, lakini pia hata wao wakiona kwenye uchimbaji hakuna maslahi, wanaweza kuuza hizo haki zao!

Mbona Hueleweki!

Hapo juu umeona suala la kuuza haki ya leseni ya utafutaji ni sawa na kuuza gesi yenyewe halafu hapa tena unasema "of course, haijauzwa"!

Acha kufanya assumptions.

Mtu anayejua hawezi kuongea ulichoongea...

Kuna mtu yeyote ambae alikashifiwa kwenye ile mada hadi useme "huwezi kuweka mambo public kwa sababu unawaheshimu na kuwapenda"?

Unaweza kutaja hizo propaganda nilizotaja hapa ni zipi au ni ipi?!
Wewe ndio hutaki kuelewa kitu ambacho kipo straight. Kama unaweza kutoa haki za makampuni kufanya tafiti, kipi kinashindwa kuwapa kuchimba?

Au unataka kusema wao wamepewa haki ya kufanya utaifit alafu uchimbaj tunafanya wenyewe? Ukishatoa haki ya kuchimba ni lazima ukubali warudishe mitaji yao, hapo ndio years za sisi kusubiri mpaka mitaji irudi. Mitaji wanarudisha lini au wamepewa miaka mingapi, hapa ndio kuna hizi conspiracies zinaingia kuwa imeuzwa.

Soma na uelewe, umepingana na waliosema imeuzwa kwa kwa tafsiri ya kwamba kilichofanyika ni utafiti tu. Mimi ndio nikaja kukuuliza utafanya utafiti alafu uchimbaji hutatoa hiyo haki? Ndio maana nikakuambia mm siwezi kuita hii ni kuuza gesi, wataoamua kuita hivyo sawa. kwa kuwa hata tusingewapa hao bado hatuna uwezo wa kufanya tafiti na kuchimba
 
Hilo litajibika kwenye mada itakayojadili Sheria ya Mafuta na Gesi pamoja na kanuni zake!
Mkuu ninaelewa vizuri kuhusu hizo sheria ndio maana nilisema baado ni kiini mamcho na wizi kuficha udhaifu wa Serikali yetu.huwezi kuwa mmliki kwa kitu ambacho huna 51 % ya shares.
 
Mkuu ni sahihi kwenye mafuta,gas na Madini utafiti wa uwepo wa rasilimali unaweza ukafanywa na Kampuni X na uchimbaji ukafanywa na Kampuni Y.
Elewa basi nilichomaanisha, nawajua waliofaanya tafiti. Huyo amesema imetolewa ya utafiti tu na sio uchimbaji, Sasa Kama tafiti tumetoa, kipi kinafanya tusitoe kwenye uchimbaji? Yeye aliweka nukta kuwa ni tafiti Wala sio uchimbaji, huku akijua kabisa hata uchimbaji tunatoa kwa kuwa hatuna uwezo wa kuchimba
 
Wewe ndio hutaki kuelewa kitu ambacho kipo straight. Kama unaweza kutoa haki za makampuni kufanya tafiti, kipi kinashindwa kuwapa kuchimba?
Hivi nimesema hawawezi kupewa haki ya kuchimba au nimesema Vitalu Vitapigwa Mnada ili kutoa haki ya kuchimba?!

Maana yake, hata hizo kampuni zilizofanya exploration zitashiriki kwenye huo mnada! Lakini ikitokea aliyeshinda ni Kampuni nyingine basi hiyo kampuni nyingine itakaa chini na kampuni iliyofanya exploration ili kufidiwa gharama zake!

Lakini kwa kuwa kampuni za utafiti ndo hizo hizo za uchimbaji basi kuna uwezekano mkubwa bado haki ya kuchimba ikarudi tena kwao lakini sio GUARANTEE
Au unataka kusema wao wamepewa haki ya kufanya utaifit alafu uchimbaj tunafanya wenyewe? Ukishatoa haki ya kuchimba ni lazima ukubali warudishe mitaji yao, hapo ndio years za sisi kusubiri mpaka mitaji irudi. Mitaji wanarudisha lini au wamepewa miaka mingapi, hapa ndio kuna hizi conspiracies zinaingia kuwa imeuzwa.
Unaongea mambo kwa kutoa kichwani. Kasome Sheria, Kanuni na Production Sharing Agreement
Soma na uelewe, umepingana na waliosema imeuzwa kwa kwa tafsiri ya kwamba kilichofanyika ni utafiti tu. Mimi ndio nikaja kukuuliza utafanya utafiti alafu uchimbaji hutatoa hiyo haki? Ndio maana nikakuambia mm siwezi kuita hii ni kuuza gesi, wataoamua kuita hivyo sawa. kwa kuwa hata tusingewapa hao bado hatuna uwezo wa kufanya tafiti na kuchimba
Wewe ndie usietaka kuelewa kwa sababu unaongea maneno ya mitaani na wanasiasa wakati sheria zipo wazi.
 
Ndo JIBU, kwa sababu ile ya Songosongo na Msimbati tayari inachimbwa!

Elewa basi nilichomaanisha, nawajua waliofaanya tafiti. Huyo amesema imetolewa ya utafiti tu na sio uchimbaji, Sasa Kama tafiti tumetoa, kipi kinafanya tusitoe kwenye uchimbaji? Yeye aliweka nukta kuwa ni tafiti Wala sio uchimbaji, huku akijua kabisa hata uchimbaji tunatoa kwa kuwa hatuna uwezo wa kuchimba
Mie nilikiwa na support ile ya kuwa unaweza ukawa na leseni ya kutafuta na uchimbaji akapewa mwingine ni vitu vinawezakana.Hata hivyo,mara nyingi inayepewa leseni UA utafutaji ndio Huyo huyo hupewa na ya uchimbaji badaye akisha kamilisha kutafiti.
 
Hivi nimesema hawawezi kupewa haki ya kuchimba au nimesema Vitalu Vitapigwa Mnada ili kutoa haki ya kuchimba?!

Maana yake, hata hizo kampuni zilizofanya exploration zitashiriki kwenye huo mnada! Lakini ikitokea aliyeshinda ni Kampuni nyingine basi hiyo kampuni nyingine itakaa chini na kampuni iliyofanya exploration ili kufidiwa gharama zake!

Lakini kwa kuwa kampuni za utafiti ndo hizo hizo za uchimbaji basi kuna uwezekano mkubwa bado haki ya kuchimba ikarudi tena kwao lakini sio GUARANTEE

Unaongea mambo kwa kutoa kichwani. Kasome Sheria, Kanuni na Production Sharing Agreement

Wewe ndie usietaka kuelewa kwa sababu unaongea maneno ya mitaani na wanasiasa wakati sheria zipo wazi.
Ulichoanza kukitakaa ndio unakubali sasa hivi, Kama unajua haki ya uchimbaji inatolewa hakukua na sababu ya kusema tumetoa ya utafiti tu. Ndio maana ninakuuliza huyo aliyefanya tafiti pesa yake anarudishaje? Uzuri umekuja kujibu sasa hivi swali ambalo umelikwepa mwanzoni.

Unasema nikasome kanuni na Sheria? Kwamba unamaanisha sisi tutaanza kufaidika kabla ya aliyewekeza? Hii inahitaji hata kubishana?

Wao wamekuja huku kutufaidisha sisi ambao hata mtaji tulikua hatuna? Stupid kabisa wewe
 
Mie nilikiwa na support ile ya kuwa unaweza ukawa na leseni ya kutafuta na uchimbaji akapewa mwingine ni vitu vinawezakana.Hata hivyo,mara nyingi inayepewa leseni UA utafutaji ndio Huyo huyo hupewa na ya uchimbaji badaye akisha kamilisha kutafiti.
Hilo ndio nililomaanisha na uzuri huyo jamaa kaja kalijibu wakati mwanzo alilikwepa. Unafikiri wanaokuja kufanya tafiti watatumia gharama zao alafu uchimbaji umpe mwingine, then wao gharama zao za utafiti zinarudishwaje? Hapo ndio nilipomuuliza mwanzo

Hizi kampuni zote zinazokujaa kuwekeza kwenye industry Kama hii hawaji kwa kukurupuka ndio maana unaona hata majadiliano ya LNG mwaka huu tulitafuta kampuni ya nje kusaidia Kushauri
 
Mie nilikiwa na support ile ya kuwa unaweza ukawa na leseni ya kutafuta na uchimbaji akapewa mwingine ni vitu vinawezakana.Hata hivyo,mara nyingi inayepewa leseni UA utafutaji ndio Huyo huyo hupewa na ya uchimbaji badaye akisha kamilisha kutafiti.
EXACTLY, na ndo maana
Ulichoanza kukitakaa ndio unakubali sasa hivi, Kama unajua haki ya uchimbaji inatolewa hakukua na sababu ya kusema tumetoa ya utafiti tu. Ndio maana ninakuuliza huyo aliyefanya tafiti pesa yake anarudishaje? Uzuri umekuja kujibu sasa hivi swali ambalo umelikwepa mwanzoni.
Duh!

Hivi huoni hoja yako ni kana kwamba aliefanya utafiti anakuwa guaranteed kuwa LAZIMA ndie atafanya shughuli za uchimbaji?
Unasema nikasome kanuni na Sheria? Kwamba unamaanisha sisi tutaanza kufaidika kabla ya aliyewekeza? Hii inahitaji hata kubishana?
Basi kumbe unabisha vitu ambavyo hata utaratibu wake HUFAHAMU...

Kwa kukusaidia, achana na kanuni pamoja na sheria lakini tafuta Model Production Sharing Agreement ambayo kwa mujibu wa sheria, wakati PURA wanafanya majadiliano, wanatakiwa kuangalia hiyo MPSA!
Wao wamekuja huku kutufaidisha sisi ambao hata mtaji tulikua hatuna? Stupid kabisa wewe
Kasome!
 
Back
Top Bottom