Mshindi wa Shindano la Big Brother Africa
Idris Sultan ameamua kukiri wazi kuwa
kipindi yupo kwenye mahusiano na Miss
Tanzania 2006 Wema Sepetu alikumbwa na
ukata.
Kupitia kipindi cha Clouds e cha Clouds Tv
Idris Sultan amesema wakati yupo kwenye
mahusiano yake yaliyopita na mrembo
Wema Sepetu alikuwa kwenye Ukata hivyo
nilijikuta sifanyi vitu vya maana kuliko
kipindi hiki ambapo yupo Single.
“ Wakati nipo kwenye mahusiano yangu
yaliyopita niliyumba kidogo kiuchumi kwani
sikuwa nafanya mambo mengi ya muhimu
kuliko sasa hivi kwani hata watu wangu wa
karibu watakueleza hivyo,nafurahi niko
single na naendelea kupambana“Alisema
Idris.
Ikumbukwe idris alishinda tsh milioni 500 za kitanzania kwenye shindano la big brother Africa.
Idris sasahivi ni mtangazaji wa choice FM