Naomba kutoa kero yangu juu ya adha kubwa ya maji eneo la Nyegezi na viunga vyake!
Kimekuwa na kero kubwa sana ya maji Nyegezi kiasi kwamba tunajiuliza watendaji wa Idara ya Maji eneo la Nyegezi wanawajibika au la!
Nyegezi ni eneo lililoko mjini lakini mnaweza kaa hata takribani wiki tatu bila maji na kila kukicha tatizo linajirudia!
Tukiuliza majibu ni marahisi kunahitilafu ya mfumo!
Lo! Shida Nini? Inaonekana Watendaji wa Idara ya maji eneo la Nyegezi hawawajibiki ipasavyo na inapelekea adha kubwa kwa watu walio hili eneo.
Tunaomba viongozi wa Mwauwasa muingilie kati swala hili Ili muweze kutatua.
Maji yakitoka speed haieleweki na baadhi ya maeneo hayafikiwi na maji!
Jitafakarini na mtambue kuwa hili suala limekuwa sugu na halina ufumbuzi.
Majibu na ufafanuzi wa Mamlaka ya Maji soma hapa ~ MWAUWASA: Tunafahamu changamoto ya Maji katika baadhi ya maeneo Nyegezi, tunaifanyia kazi