Habari za jumapili wana MMU, natumai wazima, ambao hamko sawa jaribuni kujiweka karibu zaidi na Mungu na kutafutta suluhisho la matatizo yenu
Leo nimeona nije kivingine sio kila siku watu wanaleta mada za kuumizwa tuu hapa, kuambikizwa UKIMWI na kupigwa mizinga. Tuambie una watoto wangapi umezaa, changamoto gani umekumbana nazo kuwalea.
Ambao bado hawajazaa wanategemea kuwa na watoto wangapi? Mimi binafsi sijazaa naomba Mungu anijalie watatu, wote wa kiume, mimi sio mbaguzi ila kulea mtoto wa kike akue kwenye maadili mema asiharibiwe huko shuleni n.k ni ushujaa uliotukuka wenye uwezo naomba msini jadili vibaya ni hisia zangu.
Najiandaa katika mazingira ya kuwa baba, najifunza zaidi zaidi ili niweze kutengeneza stable family changamoto yangu kubwa kwa sasa ni mke bomba wa kuoa, kwa kweli naona chenga tuu ila namtegemea Mungu anipe kifaa cha maana.