- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Wakuu
Nimeona vyanzo mbalimbali vimepost hii taarifa huko YouTube. Je, ni kweli Ibrahim Traoré, Rais wa Burkina Faso, amewasili nchini kuhudhuria mkutano wa nishati ambao unaendelea leo kwa siku ya pili?
Nimeona vyanzo mbalimbali vimepost hii taarifa huko YouTube. Je, ni kweli Ibrahim Traoré, Rais wa Burkina Faso, amewasili nchini kuhudhuria mkutano wa nishati ambao unaendelea leo kwa siku ya pili?
- Tunachokijua
- Captain Ibrahim TRAORÉ ni Rais wa kijeshi chini Burkina Faso aliyefanya mapinduzi ya kumtoa Rais wa wa mpito wa wakati huo ambaye alikuwa ni mwanajeshi pia Paul-Henri Sandaogo Damiba September 2022. Aidha Captain Ibrahim anatajwa kuwa miongoni mwa marais wenye umri mdogo zaidi barani Afrika na duniani.
Mkutano wa nishati Afika ni mkutano unaowakutanisha viongozi wa mataifa mbalimbali barani Afrika kujadili kuhusu nishati, mkutano huo unafanyika jijini Dar es salaam, Tanzania ukiwa na jina la Mission 300.
Baada ya mkutano huu kutangazwa na kwa kuwa unashirikisha viongozi wa mataifa ya Afrika ziliibuka taarifa nyingi kuhusu uwepo wa Rais wa Burkina faso, Captain Ibrahim tazama hapa na hapa. Wengi wamekuwa wakionesha shauku yao ya kutaka kumuona akiwa nchini Tanzania.
Madai
Baadhi ya chaneli za mtandao wa Youtube siku ya tarehe 27 januari, 2025 waliandika vichwa vya habari kuashiria kuwa Captain Ibrahim amewasili nchini tanzania na amekutana uso kwa uso na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan. Tazama hapa na hapa.
Uhalisia wa madai hayo upoje?
JamiiCheck imefuatilia madai hayo na kubaini kuwa si ya kweli. Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck umebaini kuwa Taarifa hizo ni za upotoshaji wa kichwa dhidi ya maudhui kwani vichwa vya habari vilivyotumika ni tofauti na maudhui yaliyomo ndani kwani hamna hata mmoja aliyeonesha kuhusu tukio hilo.
Aidha kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mahmoud Thabit Kombo alitaja nchi ambazo Marais wake wamethibitisha ushiriki wao katika mkutano huo ambapo Burkina Faso haikuwa miongoni. Nchi zilizotajwa ni Algeria, Comoro, Liberia, Lesotho, Botswana, Kenya, Ghana, Gabon, Sierra Leone, Ethiopia, Sudan, Malawi, Zambia, Somalia, Guine Bisau, Burundi, Mauritania, Kongo Brazzaville, Madagascar, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Libya, Nigeria, Djibouti na Gabon.
Idara ya mawasiliano ya Rais wa Burkina Faso walitoa taarifa kuwa kwa siku ya jana tarehe 27 January, 2025 Rais wa Burkina Faso Captain Ibrahim alikuwa na kikao na mawaziri wa mambo ya nje wa Shirikisho la Nchi za Sahel, walioko Ouagadougou kwa ajili ya mkutano wa kubadilishana mawazo kuhusu mwelekeo wa ushirikiano wa baadaye na kujitoa ECOWAS. Mawaziri hao waliwasilisha ripoti ya kazi yao kuhusu kujitoa ECOWAS.