Daudi Kempu
Member
- Dec 6, 2024
- 26
- 56
Pengine hadi sasa hujui, wala hujawahi kufikiria kuwa; wewe ndo hayo mabadiliko unayotamani sana kuyaona duniani.
Kwa namna moja ama nyingine, umekuwa ukijichukulia kuwa mfinyu na usiye na nafasi kabisa ya kuibadilisha dunia hii.
Swali ni! KWANINI ULIUMBWA? Kwanini ulikuja katika hii dunia? Tena ukiwa kama mwanadamu na si kiumbe kingine chochote?
Ukipata jibu, ama majibu ya swali hili; niamini mimi utakuwa umeanza rasmi kujiwajibibisha na utakuwa na kila nafasi ya kutumikia kusudi la kuumbwa kwako, kwakuwa utalijua.
Kusudi, si jambo jepesi, na huzidi ugumu pale ambapo, kusudi lako limebeba majibu ya watu wengine; ama limebeba nuru ya kizazi husika.
Usiogope. Kusudi si mali yako, na sio wewe utakayelifanikisha. Kusudi ni mali ya Mungu aliyekuumba, ukijinyenyekeza na kuwa mtiifu na mwaminifu, atanyanyua jeshi la kuungana nawe katika kubadilisha ama kuunda jambo jipya duniani.
Wewe ni wapekee, wewe ni wa thamani, wewe ni wa maana na zaidi sana; wewe ni mabadiliko unayopaswa uyafanye.
Kwa nafasi yoyote uliyonayo, nathubutu kukuhusia na kuihusia nafsi yangu kuwajibika kwa ukubwa na kwa uaminifu. Iwe ni katika familia ama katika utafutaji; wajibika, na uwe mwaminifu.