Ukisikiliza kwa makini hoja za baadhi ya wabunge wa ccm utagundua kwamba kuna grievances na masononeko moyoni. Kuna hali fulani ya kutoikubali serikali ya Magufuli. Wanajitahidi kuficha hizo grievances au sonono lakini wanashindwa wanajikuta wanazibwaga hsdharani.
Mosi. Kamati ya budget inayoongozwa na Hawa Ghasia imeiponda serikali na waziri wake kwa kutochukua wazo hata moja kutoka kwenye kamati.
Pili. Mchango wa Aeshy Hilal, Kangi Lugola na wengineo wakati wanachangia bajeti, wamesikika wakimwambia waziri wa fedha kwamba hajui uchungu wa kuwa mbunge wa jimbo ndio maana anataka kuweka kodi kwenye kiinua
mgongo chao. Hii imekuwa kama kebehi kwa waziri Mpango sio kwa Mpango tu bali kwa wale wateule wa rais km Tulia na wengineo.
Inaonekana kama wabunge waccm hawakufurahishwa na Magufuli kwenda kutafuta waziri wa fedha nje ya wabunge wakuchaguliwa wa ccm. Imeonekana km rais hawaamini wabunge wa chama chake. Sasa hasira zote wameamua kumwangushia waziri Mpango.
Kina mpango wanaonekana kama outsiders. Hivyo wanachapwa kwelikweli!
Wabunge wengi wa ccm kwa nje wanaonekana wapo na serikali yao lakini mioyoni mwao wanatamani ishindwe. Inaonekana utumbuaji umewagusa wengi marafiki au ndugu zao labda ndio pia chanzo cha hizi grievances za chini chini zinazojitokeza unconsciously kwenye kauli zao!
Sikiliza kwa makini video clips za kina Bashe Kangi Lugola, Aeshi Hilaly Hawa Ghasis na wengineo wakichangia kwenye bajeti hii, utagundua nilisemalo. Aeshi Hilaly kwa mfano anamuuliza Mpango kama serikali ina chuki binafsi na CAG!!! There is something fishy indeed!