Habari great thinkers.
Nimekuwa msomaji kwa muda mrefu sana humu, ila imenilazimu nijiunge ili nitoe nilichonacho maana ninahisi kuzidiwa moyoni sipati kulala usiku. Nahitaji ushauri.
Mimi ni mama wa mtoto mmoja wa miaka 6, nimeolewa miaka 8 iliyopita, nyumba tunayoishi tumepewa na mama mkwe kwa hiyo hatujajenga na wala hatulipi kodi. Najua unajiuliza hizi information za nini leta hoja, sawa nakuja na hoja.
Ni hivi mume wangu ana kipato cha kawaida tu kwa mwezi labda laki 8 take home. Binafsi nina kipato kwa mwezi kama 2.3m take home. baada tu ya kufunga ndo mume wangu alipoteza kazi kwahiyo alikaa nyumbani kuanzia 2017 akaja kupata kazi 2021 lakini tuliiishi bila shida.
Yeye kwao ni last born ana kaka na dada. Mimi kwetu ni wa pili kuzaliwa ila nahudumia wazazi pia. Kipindi yupo nyumbani ni kamwambia aongee na kaka yake amuazime mtaji wa kufanya biashara lakini mwenzangu alikuwa akikaa kimya, so miaka ikaenda mpaka alivyokuja kupata kazi.
Mwaka jana mwishoni nikagusia tena na kumpa idea ya biashara na alionekana kuipenda sana akasema sawa, na hiyo mwaka jana nilimwambia kwa kuwa mtoto anaingia darasa la kwanza hatuwezi kutegemea mshahara pekee. Ingawa mimi nimefungua biashara ila bado changa na pia ninafanyaga tender za kuprint, kufunga zawadi na kadhalika.
Mtoto tumemtafutia shule kwa pamoja na ada alikuwa anaijua tangu Novemba, nikamwmabia ngoja nikupunguzie mzigo nitalipia usafiri na uniform akasema sawa.
Nikawa namkumbusha kulipa ada anasema anakumbuka. juzi jumapili anasema hiyo ada kubwa sana hatoweza hiyo shule, imagine bado wiki shule zifunguliwe.
Baadae nikamuuliza kuhusu ile idea ya biashara vipi? mana haijalishi mtoto anasoma wapi jinsi anavyozidi kukua madarasa ndivyo gharama zinazidi, akasema mi mambo ya biashara siyawezi wala sijawahi kuyawaza, duuh nikabaki nimetoa macho, nikamuuliza mbona ile idea uliipenda na ukasema utaifanya utamuazima kaka yako mtaji akasema mi siwezi hayo mambo.
Haa, moyo wangu uliinama sana tangu hiyo siku nina mawazo sipati usingizi. Najiuliza niongee na kaka yake au dada yake wamshauri kama hawezi kutegemea kukua kimaendeleo kwa mshahara tu au nibaki nalo? na nikibaki nalo nifanyeje?
Hawazi kujenga, hawazi kununua kiwanja, 2024 january nilimwambia tuweke kiasi cha fedha kwa ajili ya kununua kiwanja akaweka mwezi wa kwanza nadhani kwa kuwa nilimkalia kooni.
Baada ya hapo akawa hawezi kuna siku nikamuuliza akasema mi niache tu na hayo mambo. Nikaacha nikaendelea mwenyewe, ila peke yangu nguvu ni ndogo.
Naombeni ushauri jamani mimi ni mtu mzima nina 40+ nashindwa kuomba ushauri wa rafiki zangu mana ndo yataenezwa.
Nadhani ninaweza pata depression kama ningebaki navyo moyoni kichwa kinauma kwa kuwaza.
Naombeni ushauri tafadhali.