Mmea Jr
JF-Expert Member
- May 20, 2016
- 738
- 1,732
Habari zenu wanajamii forum. Huku niliko, mimi ni mzima wa afya, na natumaini huko mlipo ni wazima pia kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu.
Leo, katika pita pita mtandaoni, nikakutana na post ya bwana James ambayo kwa namna moja imenivutia sana na kunifanya nije hapa kuianzishia uzi, pengine tukapata lolote la kujifunza toka kwake kuhusu namna ya kutumia mitandao ya kijamii katika kulitangaza taifa letu la Tanzania.
Bwana James ameieleza Afrika na dunia juu ya kile kinachofanywa na jirani yetu, Kenya. Amesema kuwa, "Kenya imekuwa ikirangua parachichi kutoka Tanzania na kuyasafirisha nje ya Afrika, hali inayopelekea taifa hilo kutambulika kama wazalishaji na wasafirishaji wakubwa wa parachichi barani Afrika na duniani kwa ujumla. Hili limekuwa likifanyika pia katika uzalishaji wa nyama na maziwa."
Baada ya kupitia maelezo haya, nilishuka moja kwa moja sehemu ya maoni na nilifarijika sana na maoni ya mfanyabiashara mmoja wa parachichi kutoka Afrika Kusini ambaye alishukuru sana kwa taarifa hii, akidai kuwa imemfungua macho. Alikuwa akirangua parachichi kutoka Kenya na kuziingiza nchini Afrika Kusini, hali iliyompelekea kuingia gharama kubwa sana, ila sasa anatizamia kuanza kuzirangua kutoka Tanzania.
Ombi langu ni hili: Wote tumeona jinsi mtu mmoja alivyoweza kumvuta mfanyabiashara mmoja kuja nchini kwetu. Je, kila Mtanzania akitumia nafasi yake kufanya hivi, tungeweza kuvutia wawekezaji au wafanyabiashara wangapi?
Pia, kizazi cha Z, kizazi cha taarifa, kizazi cha sayansi na teknolojia, kizazi cha mitandao ya kijamii, badala ya kuingia huko na kufuatilia habari za WCB, Mwijaku na wengine, jamani tumieni nafasi hiyo pia kuandika chochote juu ya mazuri ya nchi yetu. Kama inakuwa ngumu, basi tumeni hata picha za Mlima Kilimanjaro. Kwa namna moja au nyingine, tutakuwa tumeitangaza nchi yetu na siyo kuiachia serikali pekee.
Asanteni.