satong
JF-Expert Member
- Sep 18, 2016
- 260
- 311
Mke wangu mtarajiwa (sijui uko wapi sasa), nafahamu uko sehemu salama na ukivuta muda na 'jamaa' mwingine kabla hatujaoana kwa nderemo na vifijo..., Lakini kabla sijakuweka ndani kuna yenye kutoka moyoni kwangu machache ya kukueleza LAAZIZI...
1. My dear future wife, Jiandae kuwa mother of my beloved family wala sio "mom material" .., usipaniki!!! Nitakuelewesha maana yangu mke wangu mtarajiwa...
Mke wangu mpendwa mumeo, nitakuwa 'father' wala sio 'daddy' kwa watoto wetu, usishangae nitawalea watoto wetu katika malezi ya tamaduni za kiafrika zaidi, hivyo kwa hilo ntakuwa conservative na sio liberal.
Ningependa kukuona ukiwa 'MAMA' wala sio 'MOM' ukiwalea watoto kwa tamaduni za kigeni, wewe ndie utakuwa msingi wa maisha ya familia yangu.., natambua kabisa, utapaswa kuishi katika misingi ya mumeo mimi...
2. My future dear wife, nitakuoa kutokana na uzuri wa asili uliojaaliwa na Mungu, hivyo basi usitarajie kupata wasaa wa kujipachika kope na kucha za bandia wala mawigi (nywele za marehemu)..., wewe ni nani hadi ujichafue na mikorogo..? Hakuna kutafuta uzuri nje ya uzuri wako wa asili..
3. My future dear wife, huko uliko ni vyema ukaanza kujifunza kuendesha biashara na kusimamia, mumeo siamini katika kuajiriwa Bali kujiajiri.., nimeajiriwa, nikakimbia ajira.. Sitaki kuwa mtumwa wa kiumbe mwingine.., napenda na wewe usiwe mtumwa wa mtu mwingine.. Anza kujifunza huko, boss of your own metaphor.
4. My future dear wife; Siku tutakayokula kiapo kanisani mbele ya Kasisi, nyuma wazazi wetu wakitabasamu, tutafanywa kuwa mwili mmoja, hivyo basi, nisingependa baadae kutenganishwa na password kwenye simu zetu (no passwords).., simu ina password zaidi ya lango la white house au pentagon..
5. My future dear wife; madhehebu yote mchana kweupeeeee yanakiri kwamba MUNGU ni mmoja tu, muumba Mbingu na nchi, hivyo basi nisingependa kukushuhudia ukihama madhehebu mbalimbali kutafuta ushuhuda usiotimia. Usihangaike na madhehebu, simama katika imani. Mungu wetu ni mmoja.
6. My dear future wife; kilichopo ndani ya uwezo wangu utapata., nitakupa kwa moyo wa dhati, nitakupenda kwa dhati ya Moyo wangu.., nitakupa heshima yangu yote.. sitapenda kuona mke wangu ambae hawezi kuniheshimu mimi na wazazi wangu.. Ukimpenda Mungu, utaipenda na kuheshimu familia yangu..
MY FUTURE WIFE, msalimie sana huyo mnayevuta nae muda kwa kwenda Samaki Samaki, Club84, Hyatt, Jembe ni Jembe, sijui kwenye live band huko NK mara Villa Park, Nyama Choma festival, Fiesta, sijui White Party, mara birthday na huko katika marriage festival.., na makasheshe mengine yote ya usiku mjini hapa..
Mimi nitakupeleka kanisani na kukuweka ndani ya nyumba yangu, utakuwa mke.., nitakuoa na kukupa watoto, utaniita mume na utakuwa mke wangu, mama wa watoto wangu.., nitakupenda na Mbingu na ardhi zitaimba na kusifu..
(just thinking positively.. But what do i know).., sijui sasa hivi 'wanakuviringa' wapi kipenzi changu.. Aisee!! LIFE!
Ndimi; Mumeo tarajali...