Zaki Khellaf huyu ni mmoja wa wasakata kandanda 'mahiri' zaidi kuwahi kutokea duniani. Ni mraibu wa soka anayetokea nchi ya Algeria anayefahamika kwa jina la Chouchaa(Shusha) maarufu duniani kote.
Choucha ni mchezaji wa 'ajabu' ambaye aliweza kutambulika kwenye mitandao kutokana na mapenzi yake kwa soka. Anajulikana kwa video zake zinazozunguka kwenye mitandao ya kijamii kama Facebook, Tiktok, Youtbe na Instagram.
Video zilizorekodiwa wakati wa uchezaji wake 'stadi' wa kandanda uwanjani hupokea maoni mengi zaidi ikilinganishwa na wachezaji wengi wa kulipwa. Wakati mwingi anapokuwa uwanjani huunda tabasamu kwa kila mtazamaji anayemfatilia.
Chouchaa ni mlemavu wa Afya ya akili lakini haruhusu ulemavu wake kumzuia linapokuja suala la msisimko anaotafuta katika soka. Kwa muda sasa, kijana huyo, anayethaminiwa sana na Waalgeria, amepata umaarufu mkubwa kwenye mitandao kutokana na video zake za soka ambazo zimewavutia watumiaji wa Intaneti.
Chouchaa ni shabiki mkubwa wa mchezo huu na anapenda kuufanyia mazoezi na marafiki zake na hasiti kuonesha vipaji vyake vya soka kupitia video zake. Amekuwa nyota halisi kwenye mitandao ya kijamii, na maelfu ya waliojiandikisha kwenye mitandao tofauti ya kijamii. Katika akaunti yake rasmi ya Facebook, Chouchaa ana wafuasi zaidi ya 400k, Instagram 768K na TikTok 555K.
Chouchaa anatoka manispaa ya Oum El Bouaghi ( أم البواقي) nchini Algeria, Kulingana na kitambulisho chake cha taifa alizaliwa mwaka wa 1982.
Wakazi wa kitongoji chake humuandalia mechi za kumfurahisha na kumtia moyo kiasi cha kumfanya
ajione gwiji la soka kuwahi kutokea Duniani. Kinachofanyika ni mahusiano ya kijamii hata kwa wale
wenye matatizo ya Afya ya akili. Jezi yake anayovaa ni namba 10 pamoja na kitambaa cha unahodha.
Anapocheza wote uwanjani huakikisha lazima afunge goli ili kumletea msisimko ambapo naye anapofunga
hushangilia kwa namna ambayo uwanja mzima hufurahi kwa kuanguka na vicheko.
Chouchaa ndio mchezji pekee Duniani anayesapotiwa na timu pinzani na washabiki wote uwanjani. Makipa wa upinzani wanaokuja dhidi ya Chouchaa wanamruhusu kuweka mpira wavuni badala ya kujaribu kuokoa.
Pamoja na kupewa mwanya huo wa kufunga hukawia kufunga bao kwenye eneo dogo karibu na Goli.
Kila anapofunga Goli anafurahia kukimbia kwa kasi katika uwanja na kujiviringisha(Kubinuka), na kuweka kidole chake mdomoni kwa maana ya kuwakata ngebe wapinzani wake. Mechi zake huandaliwa katika viwanja vidogo vyenye ubora mzuri ambazo hujumuisha wachezaji watano kila upande.
Inaelezwa ana mahitaji maalum hivyo jamii yake inamfanyia yote hayo ili ajihisi kuwa ni nyota wa Soka bora Duniani. Sapoti anayopewa Chouchaa inatufunza kuwathamini wenzetu wenye matatizo ya Akili kwa kuwapa moyo bila ya kuwatenga.
Unaweza kwenda kumuona kwenye akaunti zake za Instagram, TikTok na Facebook.

Login • Instagram
Welcome back to Instagram. Sign in to check out what your friends, family & interests have been capturing & sharing around the world.
www.instagram.com