Huyu mwandishi wa Mwananchi Juma Bakari kaamua kukopi uzi wangu kwenye JF na kuuchaopisha gazetini bila hata kusema kaitoa hiyo habari JF!

Synthesizer

Platinum Member
Feb 15, 2010
12,639
22,490
Wana JF, mnakumbuka uzi wangu hapa chini ambao wengi wenu mlinishukuru sana na hata mnasema hadi leo unawasaidia sana


Sasa kuna huyu Mwandishi anaitwa Jafari Juma katoa sehemu ya huu uzi kwenye gazeti la Mwananchi, halafu wala hata hajatoa message kwamba source ni JF, maana kwa kuwa mie natumia pseudo name basi angalau angewa-acknowledge JF.

Hiki ndio tunaita plagiarism.

Mie niliandika hivi;

Update 3; Kujiokoa ukitumbukia na gari majini; Muhimu sana!!!
Kutokana na matukio mengi ya gari kusombwa na maji wakati wa mafuriko, nimeona ni vema pia nikaongelea hili suala hapa. Ni muhimu sana kukumbuka kwamba kitu chochote chenye hewa iliyofungwa ndani kama matairi ya gari kitaelea majini. Hivyo, mara nyingi sana, hata kwenye maji yanayoonekana kuwa na kina kidogo, gari zinakuwa na mwelekeo wa kuelea kwenye maji mengi. Hii ni kwa gari zote, kubwa na ndogo. Hivyo ni muhimu sana kutojaribu kukatisha au kupita barabara ambayo imefurika maji, hasa maji yanayotembea. Huko nyuma ilishatokea basi nzima lililojaa abiria likiwa safarini toka Tanga kuja Dar kusombwa na maji lilipotaka kupita daraja ambalo maji ya mto yalikuwa yakipita juu, japo dereva aliona maji hayo kuwa na kina kidogo. Suala muhimu la kukumbuka ni kwamba tairi zimejazwa upepo, hivyo ukipitisha gari kwenye maji gari itakuwa ina mwelekeo wa kuelea, na itahitaji nguvu kidogo sana kuisomba na kuipeleka nje ya barabara.

Na pia, gari ikitumbukia majini mara nyingi milango inakuwa migumu kufunguka kutokana na pressure ya maji kwenye milango. Na pia ni vigumu sana watu kujiokoa kwa sababu ya kupanic. Ili uweze kufungua mlango ni vema usubiri maji yaingine ndani ya gari kwa kiasi fulani ili kubalance pressure ndani ya gari na nje, na milango itafunguka kirahisi. Kama vioo vilikuwa vimefungwa ni vizuri hata zaidi kwa sababu maji hayatajaa ghafla ndani ya gari, na kukupa muda wa kupanga jinsi ya kutoka na kujiokoa. Hivyo usipoteze nguvu nyingi kujaribu kufungua milango ikiwa pressure ya maji inakuzuia kufanya hivyo, kwa sababu utatoka nje ya gari wakati huna nguvu na pumzi ya kutosha. Ikiwa una kitu cha kuvunjia vioo, vunja vioo ili utokee dirishani badala ya kusubiri maji yajae ndani ya gari ili uweze kufungua milango. Unaweza pia kujaribu kufungua madirisha kwa kutumia power window au kidude cha kufungulia kioo. Kumbuka sio rahisi kufungua mlango wa gari iliyozama majini.

Gari ikizama majini jitahidi kuto-panic, jipe kama sekunde thelathini kutuliza akili na kupanga jinsi ya kutoka na kujiokoa, badala ya kutumia nguvu nyingi ambazo zitakuchosha kabla hata hujajaribu kutoka ndani ya gari na kuogelea kwenda juu. Pia watu hupoteza mwelekeo wa wapi ni juu na wapi ni chini wakizama na gari. Hivyo unaweza kufa kwa kuwa tu hujui uogelee kwenda wapi, hasa ikiwa gari ilitumbukia na kupinduka. Jambo la msingi ukizama na gari ndani ya maji, kabla maji hayajajaa ndani, ni kujipa muda kidogo wa kutulia, na kujua mwelekeo wa kwenda juu ni upi, kutegemea kama gari imegota chini au bado inaelea. Kama maji sio machafu na sio usiku, angalia mwelekeo wa mwanga uko wapi, huko ndio juu. Pia unaweza kuzifuata povu (bubbles) kwa sababu huwa zinaelekea juu. Ni muhimu sana ujue wapi ndio juu kabla ya kuanza kuogelea. Kabla hujatoka ndani ya gari ambako kuna hewa, vuta hewa nyingi, bana pumzi na kuanza kuogelea kwa kasi kwenda juu au kufuata mkondo wa maji.

Jambo la msingi ni kuepuka kupita na gari sehemu yenye maji mengi, hasa yanayotembea, kwa sababu hewa kwenye matairi ya gari yanafanya gari iwe na mwelekeo wa kuelea na hivyo kusombwa kirahisi sana, hata kama gari yako ni four wheel drive. Yaani, kama ikibidi, basi toa upepo kwenye tairi ili uvuke sehemu yenye maji - kitu ambacho sidhani kama utataka kufanya.

Ikiwa unasafiri wakati wa mvua sehemu zenye kufurika kirahisi, huenda ni vizuri kuwa na na maboya ya kuogelea ndani ya gari, hasa kwa ajili ya watoto. Ni rahisi kumuokoa mtoto ikiwa amevaa boya la kuogelea.

Angalia yeye alivyoandika;


1570771441066.png
 
Wameiga tabia ya diva yule wa clouds,walishawahi pia ku-copy tena thread ya yule The bold akakomaa nao wakamtoa mpunga wakamalizana.

Bongo hatuna waandishi wa habari mostly kuna maripota,waandishi wenyewe ndio hawa walitupiwa hela na Uwoya wakazigombania kama hawana akili nzuri.
 
Dawa yao ni kuwa na haki miliki ya maandiko akikopi na kupesti akumbane na rungu la sheria.
Daah shida mlalalamikaji unakuta hautaki ujulikane real identity yako hapo ndio changamoto,hata kwenda kufuatilia huko kwny gazeti la Mwananchi ni changamoto.

Maana unaweza ukawa mpondaji mzuri wa awamu ya kujimwambafai then ukajikuta kucha na pumbu 1 wameng'oa arifu.
 
Wameiga tabia ya diva yule wa clouds,walishawahi pia ku-copy tena thread ya yule The bold akakomaa nao wakamtoa mpunga wakamalizana.

Bongo hatuna waandishi wa habari mostly kuna maripota,waandishi wenyewe ndio hawa walitupiwa hela na Uwoya wakazigombania kama hawana akili nzuri.
Wale waliogombania pesa siyo waandishi ni watu wenye njaa kwenye mifumo yao ya maisha.

Kuna waandishi kama pascal Mayala wanaweza kuandika kitu ukaona kweli kuna mtu mwenye taaluma ya uandishi wa habari kaandika.
 
Daah shida mlalalamikaji unakuta hautaki ujulikane real identity yako hapo ndio changamoto,hata kwenda kufuatilia huko kwny gazeti la Mwananchi ni changamoto.

Maana unaweza ukawa mpondaji mzuri wa awamu ya kujimwambafai then ukajikuta kucha na pumbu 1 wameng'oa arifu.
Waandishi wetu ni wale wa kukopi na kupaste japo ni kweli taarifa nyingi zipo mtandaoni kwa sasa wajaribu kuwa na angle nyingine siyo kubeba andiko zima zima.

Wanaona wakitoa credit wataonekana wapumbavu na kweli ndivyo walivyo.
 
Wale waliogombania pesa siyo waandishi ni watu wenye njaa kwenye mifumo yao ya maisha.

Kuna waandishi kama pascal Mayala wanaweza kuandika kitu ukaona kweli kuna mtu mwenye taaluma ya uandishi wa habari kaandika.
Na kwny tasnia ya jabari jiulize watu wa dizaini ua Pascal watakua wangapi?
 
Mara kibao member wa JF wanatoa content Mwananchi na kuzileta hapa JF
Ila mwandishi wa Mwananchi akichukua content JF hata mara moja tu inakuwa anatukanwa kiasi hiki? Mpumbavu, kanjanja, njaa kali n.k?
 
Mkuu msamehe bure tu huenda akawa ameokoa jopo kubwa la watu kumbuka humu tu hatupo million 1 ila Kuna watz mil 50+ huenda walikuwa hawalijui hili ila akirudia atiwe adabu
 
Back
Top Bottom