Huyu mwanaume ni wa aina gani?

Rasterman

JF-Expert Member
Feb 24, 2015
33,894
44,097
Jamani wanajamvi, habr za wikendi.
Kuna wanaume mamburula sijawahi kuona.
Kuna wanaume mambuzi hadi wanakera, kuna wanaume sijui wana wadaudu kichwani.

Yaani kuna wanaume sifa za kuitwa wanaume hawana kabisa na si shauri kabisa mdada kuwa na mwanaume kama huyu.
Mwanaume Punga.kabisa hadi nakereka kwa huyu mwanaume mwenzangu.

Stori iko hivi, nilihamia sehemu fulani hapa dar, nikawakuta wapangaji wengine, kuna mama alitaka kunizoea mara naomba sh mia tano mara kesho sijui nini? Ni mzuri kiasi fulani na nikamgundua anataka kunizoea nikawa namkwepa sababu nina mchumba wangu.
Kumbe huyu dada alikuwa anaishi na mume ambaye sijawahi kumwona mchana kutokana na shughuri zake.

Basi maisha yakaendelea, bidada akapata serengeti mtaa wa tatu hivi, akawa anaenda kugegedwa huko anarudi home kwa mme wake, ilifika kipindi bidada analetwa na gari la mshikaji home kwake na mume wake anashuhudia.

Hali ilizidi kuwa mbaya sana kwa mwanaume huyu, mke wake alianza kuja na nguo za mchepuko wake kwenye begi na kufua ilihali mme yupo, huyu mwanaume alikuwa anajua kila kitu, na aliweza kulala na mke wake ili hali akijua dhahiri kuwa anatusuliwa na another guy in the street.

Wanawake wenzake hapa walimshauri sana kuwa anachomfanyia mmewe sio kitu kizuri lkn mwanamke huyu aliweka pamba masikioni akaendeleza uasherati wake.

Pamoja na hayo mme alikuwa bado anakaa naye.
Siku moja (wiki iliyopita) mke huyu alikaa kwa serengeti wake siku tatu mfurulizo usiku na mchana, alivyorudi tu mme akafanya maamuzi mimi nayaita ya kijinga.

Akatuita wapangaji wenzake wote( kumbuka mimi nikikuwa simfahamu kipindi chote hicho) kila mtu alishangaa tunaitiwa jambo gani. Basi akasema wapangaji wenzangu naomba nimwize mke wangu mbele zenu,.

Akamwuliza, hivi mama angel nimekufanyia kosa gani kwa haya yote unayonitendea? Mama angel mke wake kimya!

Basi akagwuka upande wetu akasema jamani ndugu na jirani zangu mimi nawaaga naondoka namwacha mke wangu afanye yoote anayoyataka lkn dunia itamfunza, kwahelini kabeba mabegi na vilago vyake akasepa.

Wanawake waliokuwepo hapa walisikitishwa na hatua ile ya mke mwenzao, wengine walimsuta sana lkn huyu mwanamke hakuwa na soni wala aibu.

Cha ajabu ilipita kama siku tatu yule mwanaume akarudi eti anamtaka mke wake warudiane mke aende huko makao mapya.

Nikajisemea moyoni huyu mwanamke anaakili sana, hata mimi simshauri akae na mwanaume punga kama huyo, mwanaume asiyejielewa.

Wanawake muwe makini na wanaume mnaoolewa nao la sivyo mtaishia kuchepuka nakuonekana nyie ndio wabaya kumbe waume na mapoyoyo.
Karibuni kwa stori ya mtaani kwetu
 
Kuna kitu hujui wewe ndoa ndoano

unafikiri kwa nini jamaa aliamua kuondoka badala ya kumfukuza ??

inawezekana huyo mama ndio kichwa cha familia na siyo huyo baba ndio maana maamuzi ya mwisho anayo mama

pia inawezekana jamaa mgonjwa kitandani hoi

pia inawezekana ikawa kwa sababu yako
 
Jamaa ana busara sana na inawezekana amelimis penzi la mkewe. Unajua wakati mwingine penzi linatia ukipofu ndo unaskia mtu anasema siwezi kuishi bila yeye so mapenzi ya wawili achana nayo
 
Mh utakuwa hujui ndoa ni nini kama umeoa bado hujakomaa kiakili kama baba.
Hebu fikiria mwanaume wa kweli anaweza poteza muda wake kuandika haya uliyoandika?
We we na akina mama wenye vitambi wote saw a tu
 
Mwanaume bwege tu huyo, kama alifikia maamuzi ya awali mpaka akadiriki kuhama ya nini amrudie.
Sijui ndo Shuntama tayari inafanya kazi au #Lukomolo (kwa wasukuma wenzangu).
 
Bora huyo mwanaume ,kuliko aliyeandika mada hii,maisha ya mtu binafsi yanakuhusu vp au ww ni Rita mlata from Singapore???
 
au ulikuwa wewe ndiye unatosha aut huyo mke wa mtu si alikuwa anakuombaga vihela halafu kumbuka umepost taarifa wanasoma wenye akili ni wewe mwenyewe ndiye uliyekuwa unamzunguka mshikaji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…