Huyu Mwanamke ananikatisha tamaa ya kumtunza mtoto

Black poison The Factor

JF-Expert Member
May 31, 2020
1,330
1,896
Wakuu kwema? Baada ya salam niende kwenye mada.

Ipo hivii kuna single mother nimezaa nae, m nilimkuta ana watoto wawili namimi nikabandika mmoja wakawa watatu.

Kipindi cha mahusiano yetu ugomvi ulikua hauishi ani ilikua ni kama walevi wa mataputapu. ni mgomvi balaa, anapenda kelele vibaya mno. na hapo kila mtoto ana baba yake. Sasa wale wengine mfupa uliwashinda wakatelekeza na watoto mazima.

Stori ni ndefu mno ila ngoja niweke kipande kifupi tu kwa Leo.

Leo alimpeleka mtoto home kwetu kwa mama maana m sipo home nipo mkoani.

Baada ya kufika akamkuta mama pale wakakaa baadae akataka kuondoka mama akamuuliza vp mtoto bado ana sukari?

Ili kama imeisha nitume hela pamoja na mahitaji mengine.

Akajibu kwamba kwani huyo mtoto wako anatambua kama amezaa namimi?

Mama akamuuliza kwanini unasema hivyo? Akasema sioni umuhimu wake.
Kwa mshituko mama akamuuliza unasemaje wewe? akasema ndo hivyo

Mama akamuuliza kwani ni lini ilitakiwa hela na hajatuma, hakujibu akakaa kimya.

Akasema unga wa uji umeisha, mama akampa hela ili akanunue ulezi akagoma tena kwa dharau zaidi akasema siendi

Ikabidi mama ampgie muuzaji simu akaleta mpaka home maana yey anaumwa hawezi kwenda. Akauchukua akaondoka Sasa hapa natakiwa nitume hela ya mchele,karanga na maharage akamsagie unga wa uji.

Nimejikuta nimekata tamaa kabisa maana hata huo uji ukisagwa wanakunywa watoto wake wote watatu alafu ananiona sina maana wala situnzi mtoto dah. inauma sana

Mbaya zaidi mtoto wake wa pili nmemlea Mimi maana baba ake alitema mchongo akiwa ana mwezi na nusu tu.

Wakashindwana alichoma vitu vyote alivyomnunulia moto akamwacha hana chchte kile, sababu ikiwa ni dharau na kelele.

Jamaa akamwambia yule mtoto amempa zawadi yeye alee tu

Hapa mi mwenyewe nilitaka niteme cargo ila mama amenisihi sana kwamba niende nae hivyohivyo tu mpaka mtoto akue kidogo maana saivi ana mwaka na nusu.

Kuna mda anasingizia mtoto anaumwa nikituma hela anaenda kushona zake nguo.

Nilikua Nina mpango wa kumuoa ila mpango ulikufa.

January baada ya kuniambia maneno ya dharau sana tena vibaya mno, akasema kwanza hategemei hela zangu wakati huohuo kila baada ya siku mbili tatu napigwa mzinga. ani nimlee yeye watoto wake wale wawili pamoja na huyu wangu mzigo ulikua mzito ila nilijikaza kiume lakini haridhiki hata kidogo ni lawama tu.

Baada ya kugombana hiyo January Ikabidi nimpige chini. Hata simu sipigi wala sms situmi, nayeye ameuchuna nikasema safi sana behewa limejikata lenyewe hapa mzigo umepungua na hela nikawa situmi kwake bali natuma kwa mama alafu anaenda kununua mahitaji anapeleka kwao.

Ila napo naona nataka kuacha kabisa maana kama natoa kila kitu bado tu haoni umuhimu wangu. Je mtoto akikua si atamwambia kwamba mi baba hewa,sijamsaidia lolote lile?

Dah ni mengi sana lakini kwa leo naishia hapa.
 
KATAA NDOA, LINDA UHURU WAKO.
KATAA NDOA, LINDA UCHUMI WAKO.
KATAA NDOA LINDA MAISHA YAKO.
FB_IMG_17077430848893304.jpg
 
Mkuu na wewe ni nouma. Yaani unataka kuoa single mother mwenye watoto wawili + wakwako?
Halafu kitu kingine jifunze ukauzu, ni bora amlete huyo mtoto ukae naye maana huyo ni kibaka mzoefu. Otherwise utakufa mbwa wewe. Halafu oa uache umalaya.
Kumleta anakataa mkuu c anajua ndo pakuchulia hela. Nikimchukua hatapata matumizi tena
 
Kumleta anakataa mkuu c anajua ndo pakuchulia hela. Nikimchukua hatapata matumizi tena
Basi temana naye. Mwache kama mwezi kusikilizia. Kuna mawili hapo; atabadilika au atamleta mtoto. Asipofanya hivyo we jilipue serikalini wakupe kiwango cha matumizi kwa mwezi na uwaambie mtoto akifikisha miaka Mitatu unamchukua kwa hati ya serikali. Atakuua huyo.
 
Back
Top Bottom