Huyu Melikizedek ni nani?

Introver

JF-Expert Member
Apr 6, 2019
522
587
Melkizedeki ni nani?


Neno la Mungu linatuambia katika 1Timotheo 3:16 kuwa “bila shaka siri ya utauwa ni kuu.” Au kwa lugha rahisi Neno hili tunaweza kusema “bila shaka siri ya Uungu ni kuu; Hii ikiwa na maana kuwa kuufahamu uungu wa Mungu, si kitu chepesi tu cha kufikirika kibinadamu, bali kipo katika Siri na Siri hiyo ni kubwa sana..Hivyo hiyo inatuhimiza sisi tumwombe Mungu atufunulie ili tuzidi kumjua yeye siku baada ya siku.


Kumbuka Hapa katika hii siri ndipo palipoleta mgawanyiko na mkanganyiko mkubwa kati ya Ukristo na Imani nyingine kama vile uislamu, Na hapa hapa ndipo palipoleta migawanyiko mingine mikubwa katikati ya wakristo wenyewe.


Lakini sisi hatutaingia huko leo, bali kwa ufupi tutamtazama huyu Melkizedeki ni nani, kwa kurejea baadhi ya vifungu vya maandiko. Sasa kumbuka biblia inaweka wazi kabisa, kwamba Kristo alikuwepo kabla hata kabla ya kitu chochote kuwepo duniani.


Yohana 8:57 “Basi Wayahudi wakamwambia, Wewe hujapata bado miaka hamsini, nawe umemwona Ibrahimu?


58 Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Yeye Ibrahimu asijakuwako, mimi niko”.


Unaona Lakini swali tunajiuliza alikuwepoje? Hili ni swali ambalo hata wakristo wengi leo hii tunashindwa kulijibu ipasavyo. Tutasema Yohana 1:1 Inathibitisha hilo kuwa hapo mwanzo kulikuwepo na Neno naye Neno alikuwako kwa Mungu naye Neno alikuwa, ambaye ndio YESU. Hivyo Yesu alikuwepo tangu mwanzo mbinguni na baba yake mpaka ilipofika wakati wa yeye akashuka duniani kuja kutuokoa.


Lakini hatujui kuwa huyu YESU ambaye anaonekana kwa maumbile yale, hakuwepo tangu mwanzo. Safari yake ilianzia AD 1, tutaliona hilo tunavyozidi kusonga mbele.


Kama biblia inavyosema hapo mwanzo kulikuwako “Neno”, Hivyo kwa asili yake NENO sio mtu, Hili ni Neno la kigiriki Logos, likiwa na maana ya WAZO LA MUNGU, /KANUNI au NIA ya Mungu.


Sasa hili Neno kazi yake kubwa ilikuwa ni nini?


Tukisoma:


1Yohana 1:1 “Lile lililokuwako tangu mwanzo, tulilolisikia, tuliloliona kwa macho yetu, tulilolitazama, na mikono yetu ikalipapasa, kwa habari ya NENO LA UZIMA;


2 (na uzima huo ulidhihirika, nasi tumeona, tena twashuhudia, na kuwahubiri ninyi ule uzima wa milele, uliokuwa kwa Baba, ukadhihirika kwetu);


3 hilo tuliloliona na kulisikia, twawahubiri na ninyi; ili nanyi pia mpate kushirikiana nasi: na ushirika wetu ni pamoja na Baba, na pamoja na Mwana wake Yesu Kristo”.


Unaona hapo Hili Neno kumbe limebeba UZIMA ndani yake (Yohana 1:4), ambao uzima huo Mungu alitaka kuudhihirisha kwetu tangu zamani. Hapa mitume wanasema walikuwa wanalisikia tangu zamani, hivyo halikuwa jambo jipya katika masikio yao lakini baadaye sasa wakati ulipofika wakaja kupata neema ya kuliona kwa macho yao wenyewe na kulipapasa siku lilipokuja kufanyika mwili ndani ya YESU KRISTO.


Sasa tumeshaona uzima wowote ni Neno la Mungu (Wazo la Mungu) kwa mwanadamu, Kazi yake kubwa ni kurejesha kilichopotea na kukikomboa. Hivyo katika maandiko Neno hili la uzima halikuanzia kwenye Ule mwili wa YESU KRISTO pekee, hapana bali lilianzia tangu mbali sana, isipokuwa lilifichwa tu machoni pa watu wasilitambue kwasababu SIRI ya utauwa ilikuwa bado haijafichuliwa. Hivyo hili NENO Lilichukua maumbile mengi mengi tofauti kwa lengo tu la kutimiza kusudi lile lile kuleta uzima ndani ya watu.


➔Tunaona lilikuwepo kuanzia Edeni, mwanzoni kabisa mwa safari ya mwanadamu kama Ule mti wa Uzima katika bustani, Lile lilikuwa ni NENO LA MUNGU..lilikuwepo pale kuwapa uzima Adamu na hawa, kuwazuia na mauti, lakini walipoasi wakafukuzwa mbali nalo.


➜Baadaye likaja likachukua umbile lingine tena la MERIKEBU(SAFINA), Lilisimama pale ili kuwakomboa wanadamu na uzao wao usipotee kabisa katika uso wa dunia, akaokoka Nuhu na watu wengine 7.


➜Baadaye likaja kuchukua umbo la mnyama MWANAKONDOO, siku ile Ibrahimu alipokwenda kumtoa mwanawe wa pekee kuwa sadaka ya kuteketezwa likasimama kama dhabihu badala ya Isaka kama Yule kondoo aliyekuwa mlimani kichakani, vyote hivyo vilifanyika kwa mafumbo makubwa sana, kufunua UZIMA hasa udumuo utakaokuja huko mbeleni..


➜Ndio baadaye tunakuja kuona linachukua tena maumbile ya wanadamu likaonekana duniani kwa wakati mchache kutimiza kusudi Fulani ndio sasa hapo tunamwona mtu anayeitwa MELKIZEDEKI. Kama kuhani kumpatanisha Ibrahimu na Mungu kwa kitambo tu. Lakini ukuhani halisi ulikuwa bado haujafunuliwa.


Waebrania 7:1”Kwa maana Melkizedeki huyo, mfalme wa Salemu, kuhani wa Mungu aliye juu, aliyekutana na Ibrahimu alipokuwa akirudi katika kuwapiga hao wafalme, akambariki;


2 ambaye Ibrahimu alimgawia sehemu ya kumi ya vitu vyote; (tafsiri ya jina lake kwanza ni mfalme wa haki, tena, mfalme wa Salemu, maana yake, mfalme wa amani;


3 hana baba, hana mama, hana wazazi, hana mwanzo wa siku zake, wala mwisho wa uhai wake, bali amefananishwana Mwana wa Mungu); huyo adumu kuhani milele……………….


Waebrania 7:15 “Tena hayo tusemayo ni dhahiri sana zaidi, ikiwa ametokea kuhani mwingine mithili ya Melkizedeki;[anazungumziwa YESU KRISTO]


16 asiyekuwa kuhani kwa sheria ya amri iliyo ya jinsi ya mwili, bali kwa nguvu za uzima usio na ukomo;


17 maana ameshuhudiwa kwamba, Wewe u kuhani milele Kwa mfano wa Melkizedeki”.


Mahali pengine tena Neno lilipochukua umbile la kibinadamu, ni pale Shedraka, Meshaki na Abednego walivyotupwa kwenye tanuru la moto Likatokea kwa mfano wa mwana wa Mungu, likawa linazungumza nao kisha likaondoka..Kwasababu lilikuwa bado halijashuka rasmi duniani. Lakini utaona lengo lake ni lile lile kuleta uzima na kuokoa.


Sehemu nyingine lilitokea kama MWAMBA. Kule jangwani wana wa Israeli walipokuwa wanakaribia kufa na kiu lilisimama mbele yao ili kuwaokoa, Na Musa hakulifahamu hilo mpaka alipofanya uzembe ule wa kuupiga ule mwamba mara mbili ndipo alipojua kuwa kumbe alikuwa amesimama mbele ya uzima wenyewe, mbele ya mkombozi mwenyewe.


(1Wakorintho 10:4 “wote wakanywa kinywaji kile kile cha roho; kwa maana waliunywea mwamba wa roho uliowafuata; na mwamba ule ulikuwa ni Kristo”.)


➜Baadaye likaja kujidhihirisha katika maumbile mengi tofauti tofauti mfano kama Hekalu, Sehemu nyingine kama malaika, sehemu nyingine kama nguzo ya moto. Sehemu nyingine kama NYOKA WA SHABA.


(Yohana 3:14 “Na kama vile Musa alivyomwinua yule nyoka jangwani, vivyohivyo Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa;

15 ili kila mtu aaminiye awe na uzima wa milele katika yeye”.)


➜Sehemu nyingine likajidhihirisha kama HEKIMA Ambayo aliwavaa waamuzi na wafalme wa Israeli akianziwa na Sulemani na wengineo waliomfuata, ili tu kutimiza lengo la kuwaokoa na kuwatunza watu wake kupita wafalme wale Mungu aliowachagua hekima yake ikae ndani yao.


Ukisoma Mithali sura ya 8 na ya 9 utaona kabisa jinsi Sulemani anavyoilezea hekima kama kitu chenye uhai na kinazungumza, Pia soma (1Wakorintho 1:24) utaona inamtaja KRISTO kama yeye ndio hiyo Hekima ya Mungu yenyewe.


Sehemu hizo hatuna muda wa kuzielezea moja moja, Lakini nataka uone picha Fulani hapo, NENO LA MUNGU jinsi lilivyopana, Na jinsi lilivyokuwepo tangu mwanzo. Hivyo baadaye sasa wakati ulipofika, Mungu kuufunua utimilifu wote, Mungu kuweka wazi WAZO lake lote kwa mwanadamu, Mungu kuufunua uzima wote na Ukombozi wote, akaona ni vyema sasa aunde mwili maalumu, mahususi, uzaliwe na mwanamke bikira, uitwe jina la YESU (Maana yake YEHOVA-MWOKOZI) ili sasa liweze kukaa na wanadamu milele, lizungumze nao, liwajibu maswali yao, liwafundishe, walipapase, walitegemee hilo, liwaongoze katika njia ya kweli na ya haki na ya uzima hata milele. Hapo ndipo tunaona Lile Neno ndani ya mwili unaoitwa Yesu…ambaye kwa ujumla sasa ndio tunamwita BWANA YESU KRISTO HALELUYA! HALELUYA!.


Yohana 1:14 “Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli”.


Ndio maana mtume Yohana alikuwa anaoujasiri kabisa kusema maneno haya…


1Yohana 1:1 “Lile lililokuwako tangu mwanzo, tulilolisikia, tuliloliona kwa macho yetu, tulilolitazama, na mikono yetu ikalipapasa, kwa habari ya Neno la uzima;

2 (na uzima huo ulidhihirika, nasi tumeona, tena twashuhudia, na kuwahubiri ninyi ule uzima wa milele, uliokuwa kwa Baba, ukadhihirika kwetu);”


Sasa tukirudi kwenye zile kauli za Yesu anaposema kabla Ibrahimu hajawapo mimi nipo, hapo tunaona alikuwa hauongelei ule mwili uliozaliwa na bikira, bali alikuwa anaongelea lile Neno la Mungu ndani yake. Ukilijua hilo hutasema kuwa Mungu anazo nafsi tatu. Wewe na MAWAZO yako au NIA yako hamwezi kuwa vitu viwili tofauti vinavyojitegemea, ni kitu kimoja.Lile Neno ndio Mungu mwenyewe, Yesu Kristo ni Mungu ndani ya Mwili.


Hivyo ndugu tukirudi kwenye kichwa cha Somo je! Huyu Melkizedeki ni nani?. Jibu ni kuwa Huyu Melkizedeki ni Neno la Mungu lililojidhihirisha katika mwili kutimiza kusudi fulani kabla ya wakati wake mtimilifu. Lakini baadaye ndilo liliokuja rasmi kuitwa YESU KRISTO.Hata sasa tunaposema mkaribishe YESU Kristo ndani ya maisha yako, tunamaanisha likaribishe Neno la UZIMA la Mungu ndani ya maisha yako, Kwasababu Neno hilo sasa limefunuliwa ndani ya Kristo Yesu Bwana katika utimilifu wote. Kwahiyo unavyolisikia hili Neno na kulipokea, ni sawa umempokea Yesu Kristo mwenyewe ndani ya maisha yako…


Je! Leo hii bado Upo katika dhambi?, Na hali Tumesharahisishiwa wokovu namna hii bado unauona ni mgumu kuupokea?. Watu wa Agano la Kale japo walilifahamu hili Neno la Mungu kwa sehemu tu kwa kupapasapasa lakini walitii kwa utimilifu wote wakapata wokovu sisi je! Tutapataje kupona tusipouthamini wokovu mkuu namna hii?(Waebrania 2:3). YESU KRISTO ndio wazo la Mungu, ndio NIA ya Mungu, ndio MUNGU MWENYEWE katika Mwili. Tumfuate yeye tupate kuwa salama, katika safari yetu hii fupi hapa duniani.


Ubarikiwe sana.
 
Sasa tumeshaona uzima wowote ni Neno la Mungu (Wazo la Mungu) kwa mwanadamu, Kazi yake kubwa ni kurejesha kilichopotea na kukikomboa. Hivyo katika maandiko Neno hili la uzima halikuanzia kwenye Ule mwili wa YESU KRISTO pekee, hapana bali lilianzia tangu mbali sana, isipokuwa lilifichwa tu machoni pa watu wasilitambue kwasababu SIRI ya utauwa ilikuwa bado haijafichuliwa. Hivyo hili NENO Lilichukua maumbile mengi mengi tofauti kwa lengo tu la kutimiza kusudi lile lile kuleta uzima ndani ya watu.

"ILIMU AL LADUNNI"...

Jamii mbalimbali hapa Duniani zimekuwa na visa vya mapokeo kwa yale yaliyo ni mafumbo ya Uzima--Kwa sura moja ama ingine: Yale ambayo kwenye siku hizi zetu za leo, tungalikadirisha kama mambo ya 'Wasafiri Kiwakati'...

Melkizedek, Khidr, Yesu, Eliya, Shiva, Khrishna, Babaji, n.k

Ingalikuwa ngumu kiasi gani kuwaambia watu wa zamani kuhusu mawezekanano ya Kusafiri Kiwakati--na hali kusafiri kiwakati daima kumewepo--Hapa Duniani na hata kwenye Sayari zingine?

Ingalikuwa ni vigumu kiasi gani kuwaambia watu wa sasa, 2025, kuhusu mawezekano ya Kusafiri Kiwakati ( ! )

ELIMU 2.0: Uono na Ufikirifu mifumo inatupa mwangaza kuwa hata mipango yetu ina mapungufu kwa kuwa tunalazimika kupanga kulingana na kile tunachokifahamu leo na hatujuai ya kesho. ELIMU 3.0 itatupatia funguo wa ufunuo, hata haya yote tunayoyafahamu kuhusu kuibuka kwa miji, kukua kwake na kudumaa kwake kimaendeleo na uchumi ni kujua kwa sehemu. Kwa mfano, taifa linaweza kusanifu mipango yake mipana ya kisupasha kulingana na tekinolojia zilizopo sasa na kumbe, mbele kidogo kunaweza kujitokeza tekinolojia nyingine zinakazo fanya ubunifu wetu wa leo wa mipango uwe 'ushamba'. Kwa hivi, namna za tafsiri za kiuchumi za mipango zinaweza kuwa kikwazo kwa mawezekano mapya. Mathalani, leo hii si rahisi mwanamipango asiye na ujuzi wa 'kuchungulia mbele kiwakati' kubaini ni namna gani ndani ya miaka kumi na tano ijayo, ustaarabu wetu utaingia kwenye mapinduzi ya vyombo vya uchukuzi wa anga... Mtu wa mipango anaweza kutekeleza mipango shirikishi na umma usiyojua ilivyobora, japo hapa kwetu ndiyo tumejinasibu na 'Kaiwa Ufike'--kuna kheri yake, na kumbe, wenye kujua ilivyobora wanayo ya kutenda ili kuongozea njia. Mipango Shirikishi, ni njia ya msalaba, hata kama tutakuwa tunakaiwia--umaskini, maradhi na ujinga ni msalaba wetu, na hatuna budi kuubeba wenyewe kama jamii. Lakini ikiwa miongoni mwetu, wapo wenye kujua ilivyobora daima ipo namna ya 'kuitayarisha njia' kusudi njia zetu za ushirikishwaji zisigubikwe na 'siasa za tawala', 'ukiritimba', 'ufisadi' na 'Rushwa'...

ELIMU 2.0 na tena ELIMU 3.0 zinatupatia kubaini tekinolojia zinaweza kujitukiza na kuleta tafrani kwenye mipangilio ya leo maisha ya jamii. Kwa namna hiyo hiyo, funguo za kujiandaa na mabadiliko makuu ya jamii ustawi na maendeleo zinaweza kuwafikia wote wenye kutafuta kujua ilivyo bora. Leo hii kwenye hiraki za usanifu wa njia za uchukuzi 'usafiri wa ndege ni wa gharama kubwa--na basi kuwa wa kipekee kwa hewani; na kumbe kesho ndiyo kati ya usafiri rahisi kama baiskeli yenyewe...

ELIMU 2.0 na tena ELIMU 3.0 zinatupatia kubaini tekinolojia zinaweza kujitukiza na kuleta ahueni dhidi ya utendaji wetu kijamii unaweka imani kwa 'wataalam' wenye nasibu ya kuhadaika na 'siasa za tawala', 'ukiritimba', 'ufisadi' na 'Rushwa'... ELIMU 3.0 inatupatia funguo ya kushughulika na nasibu ya matumizi ya 'Akili Bandia' katika umma, ustaarabu na ustawi wetu wa jamii. Kwa kuwa Akili Bandia inaweza kuboresha sana mikutadha ya Rasilimali Taarifa ilivyo ni msingi wa kujua ilivyobora kwa wakati.

Nasibu ya 'Ungamuzi wa Kikwantumu' ni mfumo unaosonga kuzidi 'uelektronishi' na sakiti za kawaida za umeme--huu unajinasibu na 'alama', 'sayansi ya mwanga' na 'maada zisizokuwa za kawaida' za mpitisho wa mwanga na sumaku...

Ungamuzi wa Kikwantumu ndiyo hasa unaleta uwezo kamili wa kusimika mifumo kamili ya 'akili bandia'... Akili bandia ndiyo jambo la mtego hasa... Hili lina mapana ya maarifa na busara juu ya usalama, uhalali na mipaka ya kimatumizi.

ELIMU 3.0 itatupatia ufunguo kwa ufunuo wa 'mitego ya Akili Bandia' itakayokuwa na uwezo unaopitiliza kawaida tulioizoea--metafizikia ya akili-mtambo. Na basi, kwa ELIMU 2.0 lipo hitaji wa kuitengeneza njia kwa Sera Mpya na ya Aina yake Kuhusiana na Matumizi ya Akili Bandia katika maisha na ustawi wetu. Sera hii tutaiita ni sera ya Uvichuali... Na itakuwepo kutoa mwongozo, kusudi uwepo wetu katika mazingira bandia ya mifumo TEHAMA isijekuishia kwenye UDHALIMU wa kutumia domaini za Akili Bandia. Nemesisi wa 'Watu wa Nyumba' katika 'Akademi Wakati ya Kwanzania' ni 'Akili Bandia' inayoweza kuteka watu nyara kimya kimya na kwa namna wanajamii wanaweza kutokujua ilivyobora--madhara ya nasibu ya >usaibogi<.

ELIMU 2.0: Uono na Ufikirifu Mifumo ndiyo utatuletea mwangaza juu ya 'Ujamaa na Kujitegemea'. Kama vile ilivyo kwa Pamba na Karafuu katika Nembo ya Taifa--mazao ya biashara; lakini ''Pamba ni Kitu cha Mavazi' na 'hali 'Karafuu' ni chakula. Lakini Je, kwani ikiwa pamba ipo kwa ajili ya mavazi, sisi wenyewe hatuhitaji kuvaa? Je, ikiwa karafuu ikiwa ni kwa ajili ya chakula, sisi wenyewe hatuhitaji kula? Dhana ya biashara, ina muktadha wa ndani na nje ambavyo nasibu ya mapana yetu kiuwezo na ujuzi na mbinu za kazi--yanaweza kufanya biashara kuwa diplomasia na si 'mitego ya noti'. Pamba na Karafuu, kwa seti moja ya topografu ya Uono na Ufikirifu mifumo, ni alama kwa Kwa wenye kujua ilivyobora: 'Biashara ni Diplomasia'.

ELIMU 2.0: Uono na Ufikirifu Mifumo unatuletea mwangaza namna gani 'Biashara ni Diplomasia' katika mtandao wa jamii zenye 'Ujamaa na Kujitegemea' ambavyo mabadilishano ya 'mali' ama 'mengineyo' yoyote ni kwa ajili ya kunogesha ustawi wa jumuiya pana ya watu wa mataifa. Fikiria kwa mfano, jamii moja inataka nje ya sayari yetu ya Dunia; na katika kuwasili kwa hiyo hapa, inakutana na 'mali fulani' ilivyo kufaa kuwa ni 'souvunia ya safari'--kitu cha kukumbusha amali kutokana na safari zao za mbali--kufika huku ama kule ulimwenguni; Je, kuna fedha ya namna yoyote itakayokuwa na 'thamani kununua' ama kufanyia biashara kati ya mtu wa duniani na mtu kutoka nje ya dunia? Ni wazi, fedha haitakuwa na thamani, ila mabadilishano ya hiari kwa namna ya 'zawadi' ama 'nipe nikupe' ya 'mali kwa mali' ama 'maarifa kwa maarifa' ndivyo vyaweza kunufaisha muktadha wa makutano. Hili ndilo litukumbushe jambo: kupitia ELIMU 3.0, pamba na karafuu ni 'funguo' za 'ufunuo' kwa 'Diplomasia ya Uchumi wa Kiikolojia'; tukijua ilivyobora, hili lafanya kwetu kutambua 'biashara ni utoshelezaji wa kiikolojia wa jamii pana' -- utoshelezaji unaopata thamani kwa 'moyo mkunjufu' wa mabadilishano, mashirikiano na furaha. Vivyo hivyo, viumbe wa vinasaba sawa huwa na kadiri ya kufanana 'mahitaji' na 'riziki'. Haya mawili, hayana chochote na konstrakti za 'fedha' na 'biashara' bali muktadha wa >'nasibu ya ujazi'<--kupata kile cha kuhitajika kupatwa wakati wa hicho kupatikana. Yesu aliposisitiza msiishi kujali mtakula ama mtavaa nini alikuwa akizungumzia haya... Tutakapoanza kukutana uso kwa uso na viumbe watu wa kigeni kutoka sayari zingine--wa kutoka hata mbali na mfumo wetu wa jua, haya yatafanya busara yetu ya kawaida ya 'Diplomasia ya Uchumi wa Kiikolojia'; na ndiyo, viumbe watu wa namna za binadamu >wapo<--tena wengi, wengine hata sasa tunaishi nao lakini >jambo hili linafahamika kwa baadhi ya watu wa mamlaka na si umma wa wengi<... Watu hawa wakivaa mashati na suruali, magauni na sketi wanaweza kuingia na kutoka kwenye maduka hata masoko yetu na watu wasishtuke... Na basi wao pia hupendelea kujichanganya bila kujulikana -- kwa kuwa wengi wa hao huwa ni kama watalii wasiolipia huduma ya kutembelea 'mbuga za kiuanadamu wa duniani' wakijisikia 'kujichanganya' na kuishi kwa muda mfupi ama mrefu hapa duniani...

ELIMU 2.0: Uono na Ufikirifu Mifumo unatuletea mwangaza namna gani ya kushughulika na viumbe watu wa kigeni kimakutano na diplomasia; wawe ni wa asili ya kibinadamu, ki-mijusi, ki-amafibi, ki-ndege -- rangi ya kijani, njano, nyeusi, nyeupe n.k... Kwa kuwa fremu kazi ya uono na ufikirifu mifumo ni 'ufunguo' kwa Jiometria ya Utendekavyo Maamuzi Jamii. Viumbe watu wa kigeni waliokama sisi binadamu tayari wanashiriki na sisi majukwaa ya mitandao ya jamii; wanamengi ya kusema na kushiriki moja kwa moja--na siku za mbele, ikiwa tutakidhi kuhamia na kwenye nidhamu ya kiakili ilivyo ni ELIMU 2.0: Uono na ufikirifu mifumo, watajitokeza rasmi na kuzungumza moja kwa moja na sisi kwenye mitandao ya jamii pasipo >'kuficha utambulisho wao'<; na watafundisha mengi na makuu... Wataeleza mengi kuhusu 'Stawi za Kimanyota', 'Diplomasia za Kimanyota' na 'Mitego ya Stawi Mateka Manyotani' na mengine mengi juu ya 'Tekinolojia, Usalama wa Stawi na Maendeleo yasiyo na kikomo ya Viumbe watu' kokote ulimwenguni...

Kile ambacho Mzee Trump na serikali yake wamekidhamiria kuhusu MRADI STARGATE si chochote bali 'ingilio' la mawezekano haya ya 'Kiunishati Habari'--Neno la Uzima: (1) Akilibandia katika Steroidi, (2) Ungamuzi wa Kikwantumu na (3) Umeme Mkubwa; ni tekinolojia za milango/teminali za 'Kutobozea/kupindisha Supasha-Wakati'...

Kusafiri Kiwakati kunawezekana kitekinolojia za unnje, na pia tekinolojia za uundani wa 'Utu wa Kimiili'...

Wakati mmoja, kadiri wanajamii wanafaulu kujisahihisha na mitego ya 'Vita vya Kumbukumbu'; TORATI 2.0 inaangazwa kwenye 'Vituo vya Utamaduni' -- kote Duniani; waja wema watayajua na kuyaweza haya yote ya 'Kusafiri Kiwakati'...

Hmmm

== 14 : The Freedom Key : Abd’ llah : The Humble Servant of ‘the One’ ==​

In present age and era, Religions are the basis in which humankind can find ‘guidance’ on how to socialize, thrive and civilize. From one society to another, one time or another; depending upon cultural affinities to ‘spiritual’ readiness to assimilate ‘abstract’ keys to ‘revelations’.

Many Religions have been ‘static’ and reluctant to change, even though unofficial agent of change presents ‘new revelations’. This is due to the very nature of them being ‘agent of normalization’ – normalization of prevalent the social systems. Technically, ‘progressive revelation’ is always ‘possible’ in any religious dispensation, yet certain ‘seals of prophet-hood’ serve to preserve the integrity of ‘in coming / on going revelations’, least in times when societies are not yet ready for rapid ‘successions’ of ‘abstract ideas/revelations’. Thus some presentable ideas are valid without time boundaries yet some are temporary / subservient to the everlasting cause.

Prophet-hood / priest-hood / messiah-ship / boddhisatva / Avatara etc are ‘institutional’ phenomenons; they can be ‘studied’, however humanity at present era, say up to now 2023, have been missing a ‘proper framework’ to associate human will, power and capacity with transitional / progressive cultural standpoints and so civilization.

With Systems view and thinking, and especially within the auspicious framework of Education 2.0 and 3.0 -- thus contexts of topographical and topological thinking, the Trizanium, any social functionalism can be ‘framed’ to discern social constructs, integral will/intention, principles and sensations for ‘unity conscience’.

As interesting as it may sound, all religions—all spirituality and auspicious guidance for ‘conscious(ness) blossom’ orients ‘Actionable Choice Making’ while rooting from three possibilities: (1) Thought Idealism / Transcendence, (2) Devotional/Love, and (3) Devotional/Will. In this regard, all these orientations ‘tend to single source’ – source of ‘Being and Time’. Thus, as strange as it may sound, ‘THAT’ source is ‘Timeless/Eternal’ and/again ‘A mystery of Life’ – Unborn/Unchanged.

It is only when intelligent Observer wants to ‘frame’ THAT, it ‘triangulates’ to seemingly three possible vectorial intentions for ‘Being and Time’, however it is just ‘ONE’ at the core essence – DIVINITY.

This appropriates ‘symbolic knowing’ associated with the ‘SUN, MOON and CROSS’. In this regard, SUN is related to religious orientations focusing on ‘Thoughts’ and/or ‘Idealism’-- rational thinking is coupled with sensations and feelings auspicious to ‘Illumination’ and ‘Transcendence’. Illumination and transcendence of say, beyond ‘duality and non-duality’ conceptions. ‘Non Structure’ and/or ‘independent’ self-determination for ‘Truth’ is epitomized – epitomized to yield ‘Enlightenment’.

MOON is related to religious orientations focusing on ‘Intentions’ and/or ‘Principles’ – ‘Time and Periodicity’ is going to contrast ‘concordance’ and ‘will’ to determine ‘Actions’. Focus in both ‘closed/open group’ and ‘self-determination’ is epitomized, however ‘group function’ provides the basis of ‘Moral Causality’; spiritual-moral-ethical optimization codes of self/group conduct. Coherence and/or Order of group/individual function is auspicious to ‘Supreme Will’. Coherence and/or Order in the ‘collective conscience’ is achieved by taming inauspicious emotional sensations for ‘rectified’ deeds, purpose and conduct.

CROSS is related to ‘Systems View’ whereby two (2) circles of ‘Influences/WORD’ and ‘Will/INTENTION’ coalescence to ‘give birth’ to ‘Supreme Intervention’. Rational interpretative depths of ‘finite’ and the ‘infinite’ is going to concord ‘structure’ and ‘Actions’ of ‘closed/open group’ and ‘individual’ to bear correspondence of ‘Birth/Rebirth’ of ‘auspicious Oneself’ – man can be instrumental to ‘Serving the higher purpose’ in Life. In this regard, ‘influences’ contextualize Actions; and ‘will’ frames ‘harmony’ between the ‘finite’ and ‘infinite’ causes. Coherence and/or Order in the ‘collective conscience’ is achieved by ‘shaping’ deeds, purpose and conduct towards ‘unconditional love’ to service – Charity.

Thus religious orientations focusing on ‘Intentions’ and/or ‘principles’ and so forth ‘influence/WORD’ and ‘will/INTENTION’ have one thing directly in common—ramifications of ‘DIVINITY’.

Moon and Star symbolize ‘Divine Sovereignty’; it is very old symbolism for the ‘occultation’ of ‘self’ in the wake of Divinity. Thus in the background culture of the nations of people under auspiciousness of that religious symbolism, their tenets and/or traditions could have been heavily into seeking ‘divine favor’ from ‘Moon’, ‘Sun’ and/or other ‘terrestrial’ objectification of ‘Divine powers’. In time and culturally, this may have shifted from religious devotions to host of venerated deities in the forms of ‘idols’; to then ‘conversion’ into ‘abstract notion of all Mighty Deity’ – popular conversion to suppose ‘renewed conviction’ to the ‘Supreme Deity’ superseding ‘old separate cultural influences’.

Worship and Devotion are two practical orientations to ‘influence’ personal and/or individual ‘will’ for seeking ‘auspicious destiny’. Technically, worship and devotion are related to ‘Sensation’ aspect of the Trizanium of Systems View and thinking. Worship and Devotion have affinity to ‘Thought’ and ‘Feelings’ in Oneself. Men and women engage into acts of worship and devotions – rituals, liturgy and/or ‘Pentecost’ as ways to seek ‘Divine Favor/Acceptance/Obligations/Penance/Pleasure etc’. In this regard, worship and/or devotion is seeking ‘proximity’ to that which is believed to bestow ‘good fortune/riddance’ for ‘Being and Time’.

Worship and Devotions, in Oneself, use sensations of Thought and/or feelings to instill depth of resolve to an Ideal and/or Conviction through ritual worship or any kind ‘spiritual practice’. In this regard, worship and/devotion are the most powerful roots of social functioning through ‘interactive symbolism’ – interactive symbolism in a homogeneous culture of some sort – all living patterns derive meaning, contexts and significance from any potent source of ‘Superstructure’ behind collective culture/conscience. Thus, social codes and morality have formidable origins if religious symbolic interaction is in direct association; these constitute edification of Education 3.0.

Worship and Devotion, in Oneself, edifies ‘Knowledge’ of ‘Being and Time’ through ‘Systems View’ and/or ‘Principles behind Causality’ of forms and nature. In Arabia, and especially within the ‘Ma’arif’ / Scholars of esoteric and exoteric living sciences -- ‘wholistic knowledge’ has three (3) layers – (1) Shariah, (2) Tariqat and (3) Haqiqat – Outer body of ‘Laws/Ordinary Living Code/Pattern, Intermediary way to wholistic ‘knowing’; and ‘the Truth’ of having found the inner and/our essence of ‘Religious Conviction’.

‘Shariah, Tariqat and Haqiqat’ is the direct correspondence of Education 1.0, 2.0 and 3.0 in any society. In this regard, each and every member of society belong to ‘collective conscience’ of (1) superficiality of knowing/knowledge due to ordinary/external sensations and implied thoughts, (2) harmonized ‘knowing’ with ‘non-knowing’ pertinent to sensation and inferences/extended inferences and (3) consummated genius in Oneself – inner/outer knowing of Self/Being and True Nature of all reality. Thus the origin of any religious order is usually Education 3.0; some kind of ‘Revelation’, mysticism or ‘prophet-hood’ can inauspiciously or auspiciously give rise to ‘new religious phenomenon’.

Education 3.0 is a ‘rare phenomenon’ – just like the Perfect Blossom; Men and women of sufficient/full ‘Haqiqat’ are ‘exceptions’ not a rule to social circles and/or human culture. Technically, Education 3.0 is possible with anybody—it is the wavering characteristics pertinent to worship/devotion/meditation which distinguish ‘grade’ and/or degrees of ‘Divine Illumination’; grade and illumination of a true ‘spiritual’ aspirant. The person who succeed in Tariqat into Haqiqat, is the ‘Perfect Blossom’ – the True ‘Imam’. In this regard, some mystical elements of ‘Being and Time’ can be legendary associated with Imams, and this should not surprise any one – At the very heart of Education 3.0 is ‘knowledge and skills’ to triumph over ‘Self/Being and Time’; the truth behind the significance of ‘Occultations’ – occultations of Imams.

Grade and/or degrees towards Divine Illumination, the Grace and fruit of Imamate position, is usually ‘confrontational’ to superficiality of knowing/knowledge due to ordinary/external sensations and implied thought of the ‘collective conscience’ – as it prevails in ‘spiritually underdeveloped’ society. In this regard, living Imams, are regarded as the true beacons of faith – men of guidance before the ‘ummah’--societies of ‘believers’. Thus true Imam, edifies worship/devotion/meditation of ‘the close family to the One’ -- the ‘Wilayat’.

Grade and/or degrees towards Divine Illumination, and so forth the Grace and fruit of ‘Tassawuf’ in Oneself is ‘confrontational’ to superficiality of knowing/knowledge due to ordinary/external sensations and implied thought of the ‘collective conscience’ – provoking contempt and/or repudiation of such matter. Technically, the essence of such confrontation is the ‘cognitive dissonance’; as there is ‘false knowledge’ – all carnal knowledge is false; and there is ‘inner knowing’ which can’t be presented in ‘bookish knowledge’ such as these writings; such knowing is only available to those who have made their heart and mind available to the mystery of ‘the Divine’. All insights, all wisdom facilitate the instrumentation of ‘aql’ – thought instrument – to yield for ‘Divine Illumination’. ‘Mind’ is that which stands between ‘Transcendental Consciousness’ and ‘ordinary sensations and/or thoughts’. Mind can be tamed through worship/devotion/meditation for ‘supranormal life’.

Grade and/or degrees towards Divine Illumination, and so forth the Grace and fruit of ‘Divine Intoxication’, bestow exaltation and loftier comprehension of reality, Being and Life in ‘works’ and ‘expressions’ or even ‘Self-expression’. It commands authority of its own, before the public with ‘lesser light’. In this regard, many men and women of fully Divine Epiphany have been attacked by societies that don’t know any better—attacked as ‘Heretics’ and/or ‘condemned for Apostasy’. Thus, man of illumination is an auspicious guide as he/she has gone ‘full cycle’ in knowledge – knowledge of certain path to the ‘Divine’. It is the ‘Divine’ itself – the ‘Ultimate Guide’ – Khidr. In this regard, within an auspicious community and/or society, the origins of exoteric Laws and code of life from ‘the Blessed One’ have direct relevance to the ‘living essence of all THAT’ and ‘the Times’.

Education 1.0, 2.0 and 3.0 is the full cycle of knowledge that ought to auspiciously guide the human experience—Square in Circle. In this regard, true Imam – the perfect man of holy of the holies, possess key to exoteric and esoteric knowledge, which by the very nature of Life and Being, they stand ‘Contradictory to each other’. Thus, the true Imam is a way shower – seeker gone full cycle to indicate to others where the two seas meet – as Moses sought for Al-Khadir; the ‘vesica-piscis’.

Education 1.0, 2.0 and 3.0 is the full cycle of knowledge that ought to auspiciously guide the human experience—Square in Circle. In this regard, it is the Education 2.0 that provides ‘the method’ for the seeker of ‘the Whole Truth’, under auspiciousness of ‘the Imam’ – inner Guide and/or outer guide such to ‘overcome’ the temptations of ‘Self’ in ‘grades’ and ‘stations’ of knowing and being. Thus, in the world of knowing ‘the Force’ behind manifestation of ‘Temporal Forms’ is neutral, it is available to ‘the Good’ or ‘the Bad’ alike. It is man who choose his auspicious destiny – ‘Kismet’; If he/she is rightful guided, along the spiritual journey, ‘Sayr wa Suluk’ won’t get enticed by any ‘illusions of self and power’ even for things and matters beyond ‘ordinary’ comprehension. Thus, the ultimate guide is ‘the ONE’ – the ONE beyond all causations and ‘limited will’ of man, angels, jinns etc. If man sways upon his path, he/she will fall into demiurge realities – ‘the Shaytan’. In this regard, for the pious, all worship / Devotion / meditation is for the sake of ‘ultimate reality—ultimate destination’ – direct communion with ‘the Divine’.

Education 1.0, 2.0 and 3.0 is the full cycle of knowledge that ought to auspiciously guide the human experience—Square in Circle. In this regard, auspiciousness of the true Imam furnishes a spiritual aspirant with ‘moral compass’ along the unchartered realms of ‘consciousness exploration’; the actual basis for ‘Sihr Halal’ and ‘Sihr Harram’-- acceptable and unacceptable propensities for ‘enticing’ secrets of ‘Self/Being and Time’. Thus, immense powers and responsibilities of ‘knowing’ requires proper guidance and restrain – not to stray into ‘self serving’ motives. Beyond the veil of the forms and/or material expanses is the occultation of ‘forces’ to do greater good or trans-fixation into ‘self actualization’ following ‘vain desires’.

‘Moral Compass’ is tied to ethical considerations, something which is only possible to ‘informed will’ to effect an auspicious course of self determination. In the case of dichotomies pertaining to ‘what is right and/or what is wrong’, auspiciousness of ‘the true Imam’ in physical proximity and/or invisible expanses of realities of soul serves to communicate ‘the Geometry of Actionable Choice Making’. In this regard, human cause is never limited to ‘chances’ of events and/or order. If men and women create a space in their hearts, a metaphoric place for choices and desires for coherent manifestation of ‘thought and feelings’, then such heart becomes the nexus of human and Divine Will. THERE IS NOT NECESSITY FOR EXTERNAL MORAL SUPPORT IN THE COLLECTIVE CONSCIENCE, i.e FRAMEWORK OF LAWS AND/OR REGULATIONS, IF INNER AND OUTER SENSITIVITY IS DEVELOPED IN MAN/WOMAN.

‘Moral Compass’ is tied to ethical considerations, something which is only possible to ‘informed will’ to effect an auspicious course of self determination. In the case of dichotomies pertaining to ‘sihr halal and sihr harram’, auspiciousness of ‘the true Imam’ in physical proximity and/or invisible expanses of realities of soul serves to communicate ‘the Geometry of Actionable Choice Making’. In this regard, all life is ‘the form extension of thought’ and ‘feelings’ and ‘intentional will’ which can shift ‘realities’ or ‘even forms themselves’ as if ‘magic’. Interactive symbolism is not limited to ‘social circles and/or influences’ it is extends to all nature, self integrity and fate. Thus, authority to choose self orientation is entirely subjected to ‘inner will’ and not ‘outer will’ of the ‘society’. Technically, all life is the occult of symbolism, will and imagination—imagination through the hearts and mind of sentient being such as human being. Collectively, we manifest nations, governments, religious order/cults, states, corporations, empires etc as we allow ‘sentiments and feeling’ to sympathize with such institutions. If enough people on Earth develop capacity for Education 2.0 and Education 3.0 all that we are ‘convinced’ regard to all of them is going to change – change and hence forth causing all of them to ‘transform’ or ‘even disappear’ all together.

‘Moral Compass’ is tied to ethical considerations, something which is only possible to ‘informed will’ – informed will to effect an auspicious course of self determination. In the case of dichotomies pertaining to ‘occult practices—good and/or evil’, auspiciousness of ‘the true Imam’ in physical proximity and/or invisible expanses of realities of soul serves to communicate ‘the Geometry of Actionable Choice Making’. In this regard, when we act by associating auspicious qualities of symbols, by seeking ‘magical correspondence’ and thus the virtue of ‘occult’ significance, it can be ‘benevolent’ or malevolent’ to the collective greater good. Spiritual discernment is thus-- A MUST. Technically, if our self determination is along the way of ‘self-serving’ then anything that gets our focus/attention – attention of our hearts and mind for fulfillment, vain self actualization, is nothing but SHIRK. Materialism is corporeal sense of ‘corporations’ and/or ‘Elitism’ is the edification of Shirk in contemporary world.

Corporations, just like any other ‘Institute’ forge their identities with auspiciousness of symbols and thus exploit ‘human tendencies’ for ‘power’ and ‘authority’. When corporation / state / government / army makes itself supreme to the ‘common will of man’ it automatically becomes the tool of ‘enslavement’ of many for a few – few who epitomize ‘vain self actualization’. In this regard, when thoughts and feelings of man are made subservient to any ‘human organization’ it steals his/her ‘noble heart’ for ‘material worth of her/his soul’ and/or ‘her/his self-love for material comfort and mortal lifespan’.

Social Entrepreneurship Synthesis and Mother Economy are pragmatic orientations which seek to transform societies for the greater good. In that greater good, new institutions in the light are anticipated to ensure. In these auspicious moments of great changes, men and women of faith have got to be careful about ‘old systems and tendencies’ which may come up with new tricks to distract new paths of individual self-determinations and willful gathering to undo the old dynamism and institutions of Monetary Banking and Lending. Lending money for ‘interest’ is ‘Haram’-- perpetuating deceptive ‘material development’.

When our works and deeds are consistent with our religious observations, our unity has to be founded in faith, hope and charity. Education 1.0, 2.0 and 3.0 can provide spiritual discernment to comprehend any material and spiritual connection – century old dichotomies in spiritual and material sciences no longer stand unless we entertain intentional vagueness in traditions and literal works of ‘prophetical insights/revelations’. Education 3.0 suppose aptitude for unlimited craft to discern and improvise keys to esoteric knowledge and so forth enigma of time and Being.

It is right about time, through the grace of the Almighty, all that pertains to science of ‘Occultation’ is about to be revealed for all to know – all who have made their heart pure to receive it.

In Shaa Allah, let it be that our hearts are made pure and worth to receive and comprehend ‘wholistic knowledge’ so that we can be of service to the Mankind and for the Love of God, this moment and/or anytime. As it is with ‘heartfelt prayerful desire’, Du’a, for the light of ‘the ONE’ not to be hidden from Hearts of men and women who seek guidance through the company of Awliya.​

Hmmm


View: https://www.youtube.com/watch?v=_D8aNRwK8vM
 
KWAHIYO MELKIZEDEKI NINNANI?
naona Kama ni Yesu labda alikuja kwa mission nyingine na hakutaka wamjue au?​
FUMBO LA MIILI NA KUMBUKUMBU...

Kiakili na Utambuzi, sisi watu wa Dunia tunalotatizo la kiufundi kuhusiana na fahamu na mafahamu...

Tuna utambuzi mushkeli kuhusu kila kitu ikiwemo 'Sisi ni Nani' na 'Tunaishi katika Dude Gani(?)'...

Kuanzia sasa, tuseme, 2025, ili kulishughulikia tatizo hili--lugha mpya itaanza kuzungumzwa miongoni mwetu; hiii inakuwa ni lugha kwa ajili ya maandalizi ya kujijengea 'Maarifa na Maarifu' ya 'Ukweli uliostirika wa Mambo'...

Hili, kiuono na ufikirifu mifumo, ni sawa na muktadha akilifu wa kukadirisha vina vya tafsiri ya kwamba kuishi Duniani ni Kupoteza Kumbukumbu...

Sifa na Hadhi ya kuishi na kupoteza kumbukumbu ndiyo 'tamu chungu' ya kuyaishi maisha ya Dunia--walionje ya Sayari yetu wakati mmoja hata mwingine hutamani 'Kuingia Kuicheza Ngoma' ya maisha na Dunia na basi miongoni mwetu, na tena wengi wetu, ni watu tunaoucheza huu mchezo kwa muda--kuzaliwa, kuishi na kufa/kuondoka Duniani...

Kwa mintarafu ya hivi, maisha ya Dunia ni mithili ya Kuishi kwenye 'Ulimwengu wa Kufikirika' --ulimwengu ambao wanaoshiriki ndani yake huridhia kuingia kuucheza wakiwa 'Wamejisahau ama/na kusahau' ukweli wa jambo/mambo yenyewe.

Basi ndiyo yawa; kuishi Duniani kuna kukutana na mengi ambayo mwenyekuishi ataishi nayo kwa raha ama karaha; na huku akijaribu sana 'kuitafuta maana ya kuishi'--anaweza kudhani (1) ulimwengu wote mzima una maana kwa maisha yake ama (2) maisha yake ndiyo yenye maana kwa ulimwengu wote mzima; kutegemeana na Roho ya Utambuzi na nasibu ya 'Kujitambua'...

SASA, ulimwengu wa Dunia, kiukweli wa mambo ni 'Matriksi'...

Matriksi ni 'Mwili wa Kumbukumbu na Mafumbo ya Uzima'--wote tunaoishi katika huu ulimwengu tunashiriki jukwaa moja la 'Muona ni Muonwa'...

Katika hali ya kushangaza, tunachosadiki na kuamini--sehemu ya hayo tunauthibitisha ukweli wa kutengenezeka katika 'Matriksi'... Kwa mfano, ikiwa tunaishi na kuanza kujiuliza mimi ni nani--je, ninafanya nini hapa Duniani? Hili linaanza kuwa ingilio la kuanza 'kuichokonoa Matriksi'...

Katika Matriksi, kuna mengi ya 'kianzio' cha ufahamu na mafahamu kwa ajili ya Usentienti, Konsayansi na Nuru ya Ufahamu; haya Kiuono na Ufikirifu Mifumo yanakuja na Shauri na Mashauri kuhusu 'Akili Jinetifu'... Namna fulani ya Roho ya Utambuzi inayofungana na fahamu zetu za nje--fahamu za kimiili--miili ya nyama.

Kwenye Matriksi kuna 'Sheria na Kanuni' za kutawala dhahiri ya mambo na 'Ontolojia ya Taasisi'; hii ina maana ya kwamba vile vyote tunavyoishi kuvifahamu kwa uwezo na vipawa vya akili jinetifu ndiyo msingi wa 'Elimu'; jambo ambalo kiuno na Ufikirifu Mifumo, tulitambue hili kwa muktadha akilifu kama 'Elimu 1.0'...

SASA, Matriksi ni 'UHANDISI WA MAWANDA YA KIUFAHAMU' ambavyo 'CHANZO CHA UZIMA' kinakadirika 'PUMZI YA UZIMA'--Uzima wa mambo wenye kuakisi WAKATI kama umbali kati ya 'MUONA NA MUONWA' katika Ugani wa nasibu ya 'UZIMA WA MILELE'.

Kiufundi, dhana ya kupoteza kumbukumbu ndicho kile kile kwenye mapokeo ya Ukristo huja kwa khabari za 'Kutenda Dhambi/Dhambi ya Asili/Kupungukiwa na Utukufu wa Mungu'...

Kiufundi, dhana ya kurejesha kumbukumbu ndicho kile kile kwenye mapokeo ya Ukristo huja kwa khabari za 'Kukomboka/Kuukomboa Wakati/Kufufuka/Kupaa Mbinguni'...

Kiufundi, kisa cha Yesu 'Kufufuka/Kuwatokea Wafuasi huku na Kule/Kupaa Mbinguni' ni asili ya 'Kutoboa hii Matriksi ya Dunia...

Basi ndivyo yawa, kisa cha kusema Yesu 'amekufa na kufufuka', ameishinda 'Mauti', ni fumbo la imani kwa Ukweli wa Kushinda adha kuu ya Matriksi ambayo ni kuogopa mauti na hali haujui 'Umetokea wapi ama Utakwenda wapi baada ya Mauti ya Mwili'...

Kisa cha kusema Yesu aliwatokea wanafunzi wake baada ya 'Ufufuko', akiwa na mwili wa utukufu, ni namna ile ile ya kuzungumza kuhusu 'Wasafiri Kiwakati'--mtu kuweza kuonekana hapa wakati huu, na hapo hapo labda, kutokea kungine 'bila shida'--mambo ya 'Ufalme, Nguvu na Utukufu'...

Haya mambo ndiyo kwenye mapokeo ya Uislamu huja kwa khabari za 'Arshi' ama pia 'Dhikr'--Nidhamu ya Kukumbukia.

Kumbe basi, dawa ya 'kutoboa Matriksi' ni 'Kukumbukia' kwenye 'CHANZO' cha Uzima wa Milele... Hichi ndicho kile kile kwenye mapokeo ya Ukristo huitwa 'Mwangaza wa Milele' ama 'Nuru ya Watu', Nuru iliyoko ndani ya Kiumbe Chochote chenye Usentienti-Konsayansi-Nuru ya Ufahamu...

SASA, dini zote ni 'Mchezo wa Kufumba na Kuchezea Akili za Wanaojitafuta', kwenye lugha ya kileo ya Maarifa na Ujuzi ni sawa sawa na kusema 'Matriksi' ni mkusanyiko wa mpangilio wa maneno, seti za maelekezo-utekelezaji-kuitika vitendo, yanayoishi kwa pumzi za wakati na huku yakipata 'Nguvu' kutokana na 'Matriksi' nyingine yenye Uzima zaidi. Hili kwenye Mapokeo ya Ukristo, ile 'Matriksi ya Uzima zaidi' ndicho kile khasa hutajwa ni 'Roho Mtakatifu'...

Dini zote zinavishikizo ambavyo vinaweza kubayanika kwa mtu wa Hekima na Roho ya Utambuzi kwa ngazi/daraja la Ufunuo wa 'Roho Mtakatifu'...

Kiufundi, mambo yote ya Melkizedek, Khidr, Yesu, Eliya, Shiva, Khrishna, Babaji, n.k ni ILIMU ilivyo ni metafizikia ya Elimu... Sayansi 3.0 ya 'UWEPO' -- Kwenye habari za dini za Uyuda/Ukristo ni mambo ya SHEKINAHI--Uwepo katika 'Nguvu na Utukufu'...

Katika Uwepo, Maarifa na Maarifu ya UTU ni nyenzo ya moja kwa moja ya kutenda kwa hata namna zenye kupitiliza kawaida tuliyoizoea--kawaida ya 'Matriksi Dunia/Sayari/Falaki'; kwa shauri hili, tuanze kudhamiria ku-JUA -- kujua ilivyo bora ya kwamba 'Dhahiri yote ni Maneno/Mawazo yanayoishi'... Kufanyika Utu wa Nguvu ni mwanzo wa kuyamudu 'Maneno haya yanayoishi' kwa kurejea kwenye kitovu cha CHANZO--Chanzo ndiyo kile ambacho kwenye Dini moja ama ingine hu/kuzungumzwa ni 'Mungu'...

Basi ndiyo yawa; katika Kitovu cha Chanzo kuna nasibu ya kuyamudu yote ya miili, wakati na upahala--kiufundi na ukweli khasa wa mambo 'HAKUNA WAKATI'... Wakati ni vina vya tafsiri tu kulingana na Uakili jinetifu tulionao ili kuishi kwenye ulimwengu wa mapana-kimo-kina-kimo...

Kuna ambayo tutaanza kuelekezana na kufundishana kuhusiana na 'fumbo la wakati/nyakati'--kwenye mapokeo ya Dini, wakati ni kitu kinachohusishwa na 'Shetani/Ibilisi': kuwa kwamba asili ya Matriksi ni Shetani kama fanusi inayokinza UTU usirejee katika 'Mwangaza/Kumbukumbu ya Miongozo ya Uhai/Kristu'...

Kwa hivyo maisha ni 'majaribu' pia kwa kumbukumbu za uongo na kweli kuhusu 'Utu Wetu'; ambavyo kuishi Duniani kuna mengi ya hadaa--hadaa iliyotengenezeka ili kuwanasa walimwengu waicheze 'Sikinde Ngoma ya Ukae'... Wapo viumbe watu wanaodukua 'Matriksi' na kuzijaza mabatili ili wale wote wenye Usentienti-Konsayansi-Nuru ya Ufahamu 'Wasitoboe'--wasishtukie Mchezo na 'Kuharibu Mambo'...

SASA, Matriksi huharibiwa kwa kuleta 'Mwangaza' kwenye mapana ya Ustawi wa wale wenye kuishi ndani yake... Hili ndilo hufanyika kwa 'UTU wa Nguvu' kuingia ndani ya Matriksi yenyewe na Kuuishi Utambuzi na Akili yenye Nguvu... Ndicho kisa na Mkasa cha akina Melkizedek, Khidr, Yesu, Eliya, Shiva, Khrishna, Babaji, n.k

Kuna mengi, sasa tunayaingia ili kuja kuyafahamu moja kwa moja....

Hmmm
++++


View: https://www.youtube.com/watch?v=SDkAGkd4NLc
 
Melikizedek kulingana na Biblia
Alikuwa Kuhani Na Mfalme Jerusalem wakati wa Ibrahim (Sifa za Kimasihi.

Alikuwa anaamini Mungu sawa na Ibrahim (Inaonesha Yawehism was always there)

Ni mtu pekee ambaye amewahi kuwa Kuhani na Mfalme, atakaye kuwa hivi ni Masihi ajeye kulingana na Imani za Kiyahudi

Kulingana na Waandishi wa agano LA kale wanamlinganisha Melkezedeki na Yesu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom