Huyu ashitakiwe kwa kuongea uongo na kupotosha jamii

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
15,039
43,766
Mimi simjui huyu mtu ila mpaka media zinamwita kufanya naye mazungumzo bila shaka ni mtu maarufu katika jamii.

Anatoa uongo kwa manufaa ya nani?

Ni kweli sasa bodaboda wamekuwa wengi sana.

Kila kwenye stand ya daladala kuna stop ya bodaboda, kila kwenye soko, makutano n.k kuna stop ya bodaboda lakini kusema bodaboda zaidi ya 70 ni Masters na degree ni uongo unaopaswa kukemewa hadharani.

Hapa ninapoishi stand ya bodaboda wapo kama 50, wengi ni wahitimu wa std 7, wengine primary hawajamaliza.

Waliomaliza form 4 unawatafuta kwa tochi.

Huyu labda kafanya research kwa online drivers ambao wao ndio kidogo wasomi wapo wengi.

Lakini totally bodaboda na bajaji ni std 7, form 4 failure na wenye four za 32, 33. Diploma, degree na Master's wachache mno.

DSM pekee madereva wa bodaboda na bajaji wanaweza kufika milioni 1 au zaidi.

So , kwa takwimu za huyu mpotoshaji degrees na Master's zaidi ya laki 7 zinaendesha bodaboda Dar es salaam?

Anapotosha kwa manufaa ya nani?

Tanzania yote madereva wa bodaboda na bajaji wanaweza kufika milioni 5.

Haya hapo maana yake degrees na Master's zinazokimbiza upepo kwa bodaboda na bajaji zinazozidi milioni 3?
 
Kwa niliwaona pale udom wengi wana Degree/Masters, labda wale sababu Ni wa mitaa ya pale udom
 
Back
Top Bottom