Huu unyonyaji wa Bayport mbona haukomeshwi?

Mwakikusi

Senior Member
Jan 14, 2014
102
24
Hivi ndugu zangu nimekuwa nikiwaza kila siku kuhusu hii taasisi ya kijambazi ya kukopesha pesa watumishi wa serikali ni ya nani na kwa nini inaendelea kuishi wakati inawanyonya wafanyakazi kwa kutoa mikopo yenye riba kubwa kinyume na makubaliano yaliyofanyika na mteja?

Unapoomba mkopo maelewano yanakuwepo kuliko pale tu utakapoanza kukatwa kupitia mfumo mf ukikopa milion 3 riba yake ni zaidi ya milioni 4 kwa nini wapo hivi na wanaachiwa?Natamani wafanyakazi watakaoripoti nipate muda niwape semina wasikope fedha hizo hata siku moja yasije yakawakuta yaliyonikuta mimi.
 
Hahaha hataree, hiyo taasisi ni noumer. Mi sijawahi kukopa ila kuna waliokopa milion 3 wakalipa milion 9 huku mbeya.
 
Mmmh
 
Mbona kila siku mnaambiwa hao ni wezi lakini hamsikii ukitaka kukopa uwe mfanyakazi/mjasiliamali nenda Tanzania Postal Bank(TPB),NMB na CRDB
 
Mbona kila siku mnaambiwa hao ni wezi lakini hamsikii ukitaka kukopa uwe mfanyakazi/mjasiliamali nenda Tanzania Postal Bank(TPB),NMB na CRDB
NILIINGIZWA CHAKA NINAPOANZA KAZI 2011 LILE DENI MPAKA LEO MIKATABA HAWANA NA KILA KITU HAWAJAKIWEKA KTK KUMBUKUMBU NZURI LAKINI WANAKATA TUUUUU NA UKIENDA WANAKWAMBIA ALIYEKUSAINISHA HAYUPO
 
acha kulalamika fuata sheria ukiona deni kubwa nje ya mkataba uliojaza nenda ofisini kwao waombe mkataba uliojaza wakisema haupo basi nenda kwa mkurugenzi muelewa, etc tatizo lako mkurugenzi anauwezo kumuamrisha afisa utumishi asitishe makato yako na hii inawezekana iwapo hao Bay port watakuwa hawana mkataba wako ambao umejaza na upo nje ya makubaliano yenu

Tatizo watumishi wengi huwa hamsomi mikataba kwakua una shida ya pesa basi unajiripua tu at the end unakutana na haya mashwaibu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…