The Palm Beach
JF-Expert Member
- Dec 30, 2015
- 2,173
- 4,711
Mchakato wa ndani wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wa kuchagua mgombea wa kiti cha Urais wa JMT
Mchakato wa kumpata mgombea u - Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndani ya CCM unafuata utaratibu maalum kulingana na Katiba ya chama na kanuni zake za uchaguzi. Kwa ujumla, mchakato huu unahusisha hatua zifuatazo:
1. Kutangaza Nafasi ya Urais
• Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) hutangaza rasmi fursa ya kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa kuwa mgombea wa Urais.
• Wagombea wanaotaka kuwania nafasi hii wanatakiwa kuchukua fomu na kujaza taarifa zao.
2. Uchukuaji na Urejeshaji wa Fomu
• Wanaotaka kuwania nafasi ya Urais hujitokeza na kuchukua fomu kutoka makao makuu ya chama.
• Hutakiwa kurudisha fomu ndani ya muda uliopangwa huku wakikidhi masharti yote yanayohitajika, ikiwemo kupata wadhamini kutoka mikoa 10 tofauti ya nchi nzima ikiwemo Zanzibar
3. Uhakiki wa Wagombea
• Kamati Maalum ya Uteuzi wa CCM hufanya uchambuzi wa wagombea waliorejesha fomu.
• Vigezo mbalimbali hutumika ikiwa ni pamoja na uadilifu, uanachama hai, uzoefu wa uongozi, na uwezo wa kushinda uchaguzi mkuu nk
4. Upigaji Kura katika Vikao vya CCM
Mchakato wa kuchuja wagombea hufanyika kupitia vikao vya chama kama ifuatavyo:
A. Kamati Kuu ya CCM
➡Hupitia majina ya wagombea na kupendekeza majina matatu yenye nguvu zaidi kwa hatua inayofuata.
B. Halmashauri Kuu ya CCM (NEC)
➡Hupiga kura ili kupunguza idadi ya wagombea na kupitisha jina moja litakalopelekwa kwenye Mkutano Mkuu.
C. Mkutano Mkuu wa CCM
➡Hiki ndicho kikao kikuu cha chama chenye mamlaka na uamuzi wa mwisho kinachojumuisha wajumbe kutoka nchi nzima.
➡Wajumbe hupiga kura ya mwisho ili kuthibitisha mgombea mmoja
atakayesimama kwa tiketi ya CCM kwenye Uchaguzi Mkuu wa Taifa.
5. Kutangazwa kwa Mgombea Rasmi
• Mgombea aliyepitishwa na Mkutano Mkuu wa CCM hutangazwa rasmi na kupewa dhamana ya kupeperusha bendera ya chama kwenye uchaguzi wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
SWALI: Samia Suluhu Hassan mwenzake mgombea mwenza wake Dr Emmanuel Nchimbi walipitia kwenye hatua na mchakato huu kweli..?