Huu ndio mkataba unaomtesa Congo DR dhidi ya Rwanda na wakulimaliza hili ni Congo DR mwenyewe

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
295,752
749,993
Mapema usiku wa tarehe 16/3/1996 viongozi wa Rwanda, Uganda, Sudani kusini na Ethiopia pamoja na kiongozi wa AFDL Laulent kabila walisaini “Makubaliano ya mkataba wa Lemera”.

Mkataba huu ulikuwa na shabaha ya kuigawa nchi hiyo kubwa mikononi mwa Marekani kupitia usimamizi wa Rwanda, Uganda, Sudani kusini na Ethiopia, huku Kenya na Tanzania wakiwa ndio wenyeviti wa kuinjinia mkataba huo wa lemela.

Japo baadae Tanzania ilijitoa kuunga mkono kuigawanya Kongo baadala yake ikaunga mkono msimamo wa Laurent Kabila katika kukataa kuutekeleza mkataba wa lemela, ambao kupitia mkataba huo ilizalishwa operation maalum iliyoitwa "Operation Banyamrenge".

Operation hii ililenga kumuondosha madarakani Mobutu, kiongozi wa muda mrefu wa Kongo na kibaraka wa Marekani ambao mpaka kipindi hicho walikuwa tayari wamemchoka kutokana na mabadiriko ya siasa za dunia.

Katika Makubaliano hayo yalio fanywa kati ya Laurent Desire Kabila na mataifa hayo huku Kabila akiwa kama kiongozi wa chama cha “kuikomboa Kongo” aliyekuwa akitaka kuondosha utawala wa dikteta Mobutu Sese Seko alipewa masharti ambayo yalianishwa kwenye mkataba wa Lemera.

Ambapo moja ya masharti ilikuwa ni kishirikina na wapiganaji wa Kinyarwanda kutoka Rwanda, Uganda na watutsi walio kuwa na makazi mashariki mwa Kongo, na baadae ya mapigano atoe sehemu ya ardhi mashariki mwa Kongo kama shukrani kwa Rwanda na Uganda huku akiruhusu usalama wa taifa hilo kuwa mikononi mwao.

Makubaliano hayo yalifanyika kwenye vilima vya Lemera vilivyoko Kivu ya Kusini katika mji wa Uvira na kujulikana kwa jina hilo, la "mkataba wa lemera" makubaliano hayo yalitaka Kabila, baada ya kuwa rais wa Kongo, aruhusu mikoa miwili ya Kivu Kaskazini na Kusini kuwa makazi ya Wanyarwanda wa kabila la Kitutsi.

Laurent Desire Kabila alikuwa tayari amechoka Kwa takribani miaka 20 ya kupambana na utawala wa Mobutu Sese Seko hivyo aliona ni bora kukubali mashariti yeyote yale ya mkataba ili tu awezi kumtoa Mobutu madarakani,.

Ukweli ni kwamba pamoja na mkataba huo lakini bado Laurent Kabila alikuwa na hesabu zake kichwani ambazo alizipania kuwa geuka baada ya ushindi wa kumfurusha Mobutu ikulu ya Palace de la ñatíonaľ iliyopo Kinshasa, na inadaiwa kuwa baadhi ya mikakati baada ya ushindi aliwashirikisha TISS (shirika la kijasusi la Tanzania) ili wampe baraka za kuwageuka Rwanda na Uganda.

Baada ya makataba huo kusainiwa, ukainjinia operation maalum iliyopewa jina la "Operation Banyamrenge" operation hii ilisukwa vyema mjini Kigali, Rwanda kwa kuundwa kikundi cha wapiganaji waliojiita “wapinzani wa dikiteta Mobutu.”

Hawa walikuwa Wakongomani na Wanyarwanda kutoka Rwanda na wengine waliokuwa wakiishi mkoa wa Kivu Kusini, Mashariki mwa Kongo. Katika kundi hilo alikuwemo Mkongomani, Jenerali Andre Kisasi Ngando, askari mtaalam wa kusomea aliyefunzwa ukomando China, USSR na Cuba.

Huyu komando Ngado anadaiwa pia kupata mafunzo nchini Ujerumani na Bulgaria. Alikuwa akiongoza Wakongomani wapatao 600 katika kikundi hicho. Wakati kikundi hicho kinaanza vita kilimteua Laurent Kabila kuwa msemaji wao, baadae akawa kamanda mkuu baada ya kifo cha Kisasi Ngando.

Mwanzoni mwa vita ya kumg’oa Mobutu kikundi hiki kilijulikana kama cha Wanyamulenge. Dunia nzima ikaambiwa na kuaminishwa kuwa hayo yalikuwa “maasi ya Wanyamulenge.” Wanyamulenge ni watu wanaodaiwa kutoka kwenye vilima vya Mulenge vilivyoko wilaya ya Uvira katika jimbo la Kivu Kusini.

Makabila ya asili ya hapo ni Wavira na Wafuliro pamoja na wabwale hawa wanaojiita Wanyamulenge ni Wanyarwanda walio lowea huko nchini Kongo. Vita vilianza kwa propaganda kuu kwamba serikali ya Mobutu haitambui Wanyamulenge ambao walidai ni raia wa Kongo, inawanyanyasa na inawanyima uraia.

Haya yalikuwa madai makubwa sana yaliyovuta hisia kali na huruma kwa wapiganaji.

Wapinzani, chini ya Jenerali Laurent Kabila waliteka, kama mchezo, mji mkuu wa Kivu Kaskazini, Goma.

Hatimae Kabila alisonga mbele na hatimaye kushinda na kuingia ikulu ya Kinshasa akiwa na wapiganaji wa Rwanda, akiwemo aliyekuwa mkuu wa majeshi wa Rwanda.

Ambaye baadae akawa Waziri wa ulimzi wa Rwanda na sasa ni mshauri wa masuala ya kiusalama ya serikali ya Poul Kagame, kamanda huyu ni General James Kabarebe.

Baada ya kuingia ikulu, Kabila aliwasiliana na Mwalimu Julius K. Nyerere mjini Dar es Salaam chini ya uratibu wa TISS, chaguo la Tanzania lilikuwa nikuzuia uuzwaji huo wa ardhi ya Kongo.

Mashauriano yaliyochukua sura dhahili ya nguvu ya Tanzania katika ujasusi yalimpa nguvu Kabila na alipowarejelea wabia wake aliwageuka dhahiri shahiri, Ilikuwa baada ya miaka miwili ya urais, alitangaza, tena kwa jeuri, kuwa wageni wote waondoke nchini.

Aliongeza kwa kufafanua, kwamba Wanyarwanda warudi kwao na kusema anawashukuru kwa kazi waliyofanya.

Kabila alinukuliwa akisema kuwa hayo (Makubaliano ya Lemera) ni “makubaliano ya porini” na kwamba yeye hakuwa na madaraka ya kuuza nchi. Alisema hakatai kuwepo mkataba, lakini akataka hilo “lipelekwe kwa wananchi kupitia bungeni ili wananchi wenyewe waamue.”

Kilichomshangaza zaidi Kabila, baada ya kutangaza kuwa Wanyarwanda warudi kwao, ni kwamba aliyekuwa wa kwanza kuondoka na kukimbilia Afrika Kusini, alikuwa waziri wake wa mambo ya nje aliyeitwa Bizima Karaha (Bizimana Karahamuheto).

Katika mshangao na labda kejeli, Kabila alisema, “Kumbe nchi ilikuwa imevamiwa! Hata waziri wangu wa mambo ya nje alikuwa Mnyarwanda?” Hiyo ilifuatiwa na kufukuzwa kwa James Kabarebe aliyekuwa mkuu wa majeshi ya Kongo na kurudi Rwanda na kuwa mkuu wa majeshi ya Rwanda.

Kufatia hatua hiyo ya Laurent Kabila kuwafurumusha Wanyarwanda Kongo na kuvunja makubaliano ya mkataba wa lemera kulipelekea kuibuka mgongano mkubwa baina ya Laurent Kabila na Marekani hasa kupitia mataifa ya Rwanda na Uganda.

Ambayo ndio yalitoa askari wake (military personnel) kwenye uwanja wa vita wakati wa kumfurusha Mobutu madarakani.

Hatua hii ikamfanya Laurent Kabila kuchukiwa na kufanyiwa mbinu ya kuondolewa madarakani, mkakati huu wa kumuondosha madarakani Laurent Desire Kabila ulipewa jina "Operation Kitona".

Hii Operation Kitona ilikuwa ni mkakati na mission ya kwanza kupangwa kuhakikisha Laurent Kabila anaondoshwa ikulu ya Palace de la Nãcíonál, mkakati huu kwa wakati huu uliinjiniwa na Rwanda kwa mipango na maelekezo kutoka Marekani.

Operation hii ilikuwa na malengo ya kumuondosha Kabila kutokana na kushindwa kutekeleza ahadi ya makubaliano ya mkataba wa lemera.

Chanzo cha Operation Kitona.

Ebu turudi mpaka mwaka 1994, Kiufupi tu ni kwamba baada ya vita ya kimbari 1994, majeshi ya kihutu yaliyopinduliwa na majeshi ya wanamgambo wa RPF yaliyo ongozwa na Kagame, yalikimbilia Mashariki ya DRC.

Hivyo utawala wa kagame uliona kama watapinduliwa saa yoyote kama hawato wateketeza mapema.

Kilichotokea ni Rwanda kuvamia makambi ya wahutu na kuwateketeza na waliokimbilia Katikati ya DRC walifuatwa hadi huko.

Na ndipo Mobutu akatoa order ya wavamizi hao kushughulikiwa hivyo vita ikabadilika malengo kutoka kuwamaliza waasi wa kihutu hadi kumpindua Mobutu, kama nilivyo eleza huko juu.

Kufikia May 1997 Majeshi hayo ya waTutsi yalifanikiwa kuondoa utawala wa Mobutu ambaye alifariki muda mfupi baadae huko Morocco.

Utawala mpya uliowekwa na watutsi ulishuhudia Rais Laurent Kabila akiteua wanyarwanda kwenye nafasi nyeti za serikali kama kulipa fadhila kwa majeshi hayo ya kigeni.

Lakini!! Ulipofika mwaka 1998 Kabila akaona hana kabisa mamlaka na utawala wake maana maamuzi yote mazito yanafanyika Kigali.

Ukizingatia Mkuu wa majeshi ya DRC alikua mnyarwanda pure Gen James Kabarebe hivyo unaweza ona alivyopokwa ushawishi wa kiutawala.

Mnamo july 13,1998 Kabila akaamua kutimua wanyarwanda na waganda wote kwenye serikali yake na kufikia tarehe 27 alitoa amri kuwa masalia wote wa kitutsi waondoke nchini mwake lasi hivyo watatolewa kwa nguvu.

Kiburi hiki kiliwakera sana serikali za kitutsi (Rwanda na Uganda, pia Burundi) hivyo wakadhamiria kumtoa madarakani ili waweke kibaraka mwingine atakayelinda maslahi yao.

Ndipo ikaamriwa kuwa Gen James kabarebe aongoze kikosi cha makomandoo cha kuiteka kinshasa na kumpindua Rais Kabila kwa spidi na ufanisi wa hali ya juu.

Ikumbukwe Jiografia ya DRC sio rafiki sana kwa logistics za kivita maana ni nchi kubwa sana iliojaa misitu na mito, na miundombinu ya usafirishaji ni migumu mnoo hivyo majeshi yakitoka Rwanda yatachukua miezi zaidi ya 6 kufika Azma yao ya Kinshasa.

Kwa kutathmini hili ikapangwa moja ya operation nzito katika historia ya Afrika ilioitwa Operation kitona ambayo ilikua na mpango wa kufikisha majeshi kwenye kitovu cha Kongo yaani Kinshasa kwa spidi ya mwanga wa radi na kumaliza mission yao haraka.

August 1998, wakitumia ndege za kiraia kabisa Boeing 727 walitua katika uwanja wa ndege wa Kitona pembezoni na jiji la kinshasa kwa usiri mkubwa na kuweza kuteka uwanja wa ndege na kufanikisha majeshi zaidi kufika hapo kujiandaa na uvamizi.

Mpango ni kuwa wakiteka jimbo maalum zaidi la Bas Congo (kwa sasa Congo Central) ambalo lina bandari na umeme mkubwa wa nchi unazalishwa pale basi ingekuwa ameparalayse nguvu yote ya serikali kujiendesha

Wakiwa na askari 800 pekee waliopo Katikati ya Kongo zaidi ya Km 1000 kutoka nyumbani kwao walianza safari ya kuuteka mji wa kinshasa na ikumbukwe kutoka Kitona hadi Kinshasa ni km 320 na ndani ya siku 5 walikuwa wamefika Kinshasa.

Serikali ya Kabila ikapatwa na shock kwa ''spidi ya umeme'' ya watutsi ikabidi aombe msaada kwa majirani ili kupata msaada wa kuikomboa serikali yake.

Ikumbukwe Kwenye 1st congo war ya kumtoa mobutu Angola ilisaidia majeshi ya Rwanda maana Mobutu alikuwa akisupport majeshi ya waasi wa Angola UNITA chini ya Jonas savimbi.

Hivyo Rwanda walitegemea kupata support tena ya Angola, lakini ambacho walisahau ni kwamba maadam maslahi ya Angola yaani waasi wa UNITA walikua hawana support tena ya DRC hawakuwa na haja ya kumtoa Kabila na ndio hapa vita ikapata sura mpya kabisa iliobadili historia.

Mnamo August 22 majeshi ya Angola, Zimbabwe na Namibia yaliingia kwenye uwanja wa vita kupitia kusini mwa Kinshasa hivyo majeshi ya watutsi 800 (yaliyoongezwa nguvu na askari 2000 wa zamani wa Mobutu ) wakazingirwa katikati ya Kinshasa.

Vita ikachachamaa na Zimbabwe walitumia ndege za kivita huku Angola ikiingiza vifaru na mizinga mizito (Heavy Altirelly) huku askari wa Rwanda wakiwa na silaha nyepesi bila msaada wa ndege au vifaru. Hivyo wakawa hawana namna zaidi ya kusurrender.

Gen. James kabarebe hakuwa tayari kusurrender ingawa alikua amezingirwa katikati akiwa hana pa kutoka. Akaja na uamuzi mzito wa kuvamia Angola kwa nyuma ili wapate nafasi ya kupumua na kurudi kwao kishujaa kuliko kupata aibu ya kushindwa vita.

Mnamo mwezi september 1998, Makomandoo wa kitutsi (Rwanda, UG na Burundi) walivamia Eneo la Zombo de maquela huko Angola ambapo walisambaratisha majeshi ya Angola ya eneo hilo na kuteka uwanja wa ndege wa jeshi.

Walipodhani wamepata mwanya wa kutorokea, changamoto ilioonekana ni kwamba uwanja ulikua mdogo sana kwa ndege kubwa kutua hivyo alihitaji walau wiki 3 wapanue uwanja ndio askari watoroshwe.

Bila uoga, wakiwa bado nchi ya kigeni walitengeneza safu ya ulinzi imara kiasi majeshi ya Angola yalishindwa kupenya kukomboa uwanja huo licha ya kuwa na silaha nzito, vifaru, ndege na ukubwa wa jeshi zaidi ya mara 10 ya wanyarwanda.

Uwanja uliendelea kupanuliwa katikati ya risasi na mabomu kurindima na baada ya wiki kadhaa Rwanda ikaanza kutuma ndege kuokoa wanajeshi wake na taratibu wakatolewa wote huku askari waliobaki kulinda uwanja kwa zaidi ya km 100.

Inaelezwa walikua wanaacha malindo yao wakikimbilia ndege ya mwisho hivyo askari wakawa wametolewa wote kisiri siri.

Kiukweli hii vita ni ushujaa wa hali ya juu wa majeshi ya Rwanda licha ya kuwa na namba ndogo na silaha chache huku wakiwa maelfu ya Km kutoka kwao bado waliweza Pambana na majeshi ya nchi 5 kubwa na hawakusurrender mpaka mwisho.

Operation Hii ilimpa Gen James Kabarebe heshima kubwa kwenye historia ya kivita kama Mkuu wa majeshi wa nchi mbili kwa mafinikio makubwa.

Mpaka leo operation hii ni moja ya operation iliyofanywa na majeshi ya nchi za Afrika yenye kuheshimika sana, pamoja na mambo mengine operation hii imeipa jeshi la Rwanda kuwa moja ya majeshi yenye moyo wa mapambano katika mazingira magumu.

Japo kuwa wachambuzi wengi huiona operation hii Kama sio chochote kwa Rwanda kutokana na kupokea usaidizi kutoka mataifa ya Marekani na Israel.

Pia wakosoaji wengi hupinga kuipatia heshima operation hii kwa kukosoa kwamba, haiwezi kuwa operation kubwa kwakuwa ilifanyika katika nchi changa, kwa kusema kuwa Kongo is a dyfunctional country, No system, no functional government, nothing for avery things.

Pia husema kuwa Rwanda iliweza kuzihimili nchi tano kwakuwa Rwanda alikua amewekwa mbele kwa maslahi ya United States of America, msaada wote ni USA, akina Kagame walikua ni foot soldiers wa USA.

Pamoja na yote hayo bado operation hiyo ni moja ya operation zinazo heshimiwa ndani ya jeshi la Rwanda la RDF, kitu kilichopelekea chuo cha maafisa wa juu nchini Rwanda kilichopo mji wa Musanze (zamani ukiitwa Ruengere) kupewa jina la Kitona military college, hiyo yote inaonesha kiasi gani operation hiyo inaheshimika nchini humo.
 
Nachokiona kwa miaka mingi viongozi wakuu wa Congo hawako kupigania maslahi kwa ajili ya maisha wa wacongomani lakini wengi wako kwa ajili ya maslahi yao tu.
IMG-20250130-WA0041.jpg
 
🙏🏾
 
"Mapema usiku wa tarehe 16/3/1996 viongozi wa Rwanda, Uganda, Sudani kusini na Ethiopia pamoja na kiongozi wa AFDL Laulent kabila walisaini “Makubaliano ya mkataba wa Lemera

Sudani Kusini mwaka 1996?
Nice observation Sudan kusini 1996 wakati John Garang bado sana na harakati zake za kupigana msituni uhuru wa sudani kusini 2013? Au ni lini hio?
 
"Mapema usiku wa tarehe 16/3/1996 viongozi wa Rwanda, Uganda, Sudani kusini na Ethiopia pamoja na kiongozi wa AFDL Laulent kabila walisaini “Makubaliano ya mkataba wa Lemera

Sudani Kusini mwaka 1996?
Umewaza vema.. Ngoja nifanye fact checking
 
Vita vilianza kwa propaganda kuu kwamba serikali ya Mobutu haitambui Wanyamulenge ambao walidai ni raia wa Kongo, inawanyanyasa na inawanyima uraia.
Hii harufu ilisikika miaka fulani Tabora, Kigoma na Katavi au Ngara kama sikosei
 
Back
Top Bottom