Francis12
JF-Expert Member
- Sep 30, 2016
- 7,533
- 22,278
Kama taifa wazee walipoanzisha harakati za kudai Uhuru na hatimaye tukaupata mwaka 1961 walikuwa na malengo.
Upo uwezekano mkubwa kwamba sisi viongozi wa sasa tumewaangusha ninyi raia katika kufikia malengo ya waasi wetu.
Msikubali kuangushwa na sisi wachache. Nyinyi ni wengi mamlaka na nguvu kututaka sisi kuwafikisha kwenye malengo ya Uhuru.
Ni jambo la hatari kwa taifa inapotokea viongozi wakakosea na kutoka nje ya malengo. wananchi wakakaa kimya na kuogopa kuonya, kushauri, kukosoa au hata kukemea sababu tu ya uwoga au hofu. Tutakuwa tunajenga Taifa la Raia waoga msiingiwe na woga juu ya Kudai Haki zenu na kututaka sisi viongozi kutimiza wajibu wetu.
Kwa kushindwa kwenu kutukemea au kutushauri tunapokengeuka sote tunaingia katika kundi moja la kuwakosea na kuwasaliti wazee wetu waliopigania Uhuru wa Taifa letu. TUJISAHIHISHE
Hussein Bashe
Mbunge ,Nzega Mjini