Hussein Bashe: Sukari ni chakula cha watu masikini

Bila bila

JF-Expert Member
Dec 20, 2016
22,045
38,952
Akijibu hoja ya Luhaga Mpina kuhusu uagizaji na uingizaji wa Sukari nchini, Waziri wa Kilimo Hussein Bashe hapo Jana bungeni alisema, "Sukari ni chakula cha watu masikini, ndo maana Wabunge mkienda kantini mnaulizwa, unataka Sukari?" Na huwa mnachagua asali Kwa sababu nyie si masikini.

Kwa namna ya pekee nichukue nafasi hii kumpongeza Waziri Bashe kwa kuwa muwazi na kusaidia kuthibitisha kwamba Wabunge wa Tanzania si Tabaka moja na wapiga Kura. Hivyo ni Wazi nchi imetengeneza Matajiri kuwa wawakilishi wa masikini.

ASANTE WAZIRI BASHE KWA SOMO ZURI.
 
Ametajirika leo anakuwa na kauli za dharau
 
Hakuna tajiri aliyeajiriwa miaka 5 tu.
Huko ni kujisahau. Hata asali inategemea inatoka wapi. Asali wanayotumia matajiri duniani imepimwa sio zetu za urambo zilizojaa nicotin za tumbaku unakuwa hauna tofauti na mtu anayevuta fegi au ugoro.
Na wakimaliza miaka mitano wanarudi kitaa kuombaomba
 
Akijibu hoja ya Luhaga Mpina kuhusu uagizaji na uingizaji wa Sukari nchini, Waziri wa Kilimo Hussein Bashe hapo Jana bungeni alisema, "Sukari ni chakula cha watu masikini, ndo maana Wabunge mkienda kantini mnaulizwa, unataka Sukari?" Na huwa mnachagua asali Kwa sababu nyie si masikini.

Kwa namna ya pekee nichukue nafasi hii kumpongeza Waziri Bashe Kwa kuwa muwazi na kusaidia kuthibitisha kwamba Wabunge wa Tanzania si Tanaka moja na wapiga Kura. Hivyo ni Wazi nchi imetengeneza Matajiri kuwa wawakilishi wa masikini.
ASANTE WAZIRI BASHE KWA SOMO ZURI.
Huo msitari wako wa mwisho una maana kubwa sana,mfundishe mwanao kuuzingatia.
 
CCM NI LAANA...SISI MASKINI TUNAHITAJI SBB HATUNA MBADALA YAKE.ASITUNYANYAPE.PIA YY NA CCM WAKE WAKAOMBE KURA KWA HAO MATAJIRI WALA ASALI
 
Akijibu hoja ya Luhaga Mpina kuhusu uagizaji na uingizaji wa Sukari nchini, Waziri wa Kilimo Hussein Bashe hapo Jana bungeni alisema, "Sukari ni chakula cha watu masikini, ndo maana Wabunge mkienda kantini mnaulizwa, unataka Sukari?" Na huwa mnachagua asali Kwa sababu nyie si masikini.

Kwa namna ya pekee nichukue nafasi hii kumpongeza Waziri Bashe kwa kuwa muwazi na kusaidia kuthibitisha kwamba Wabunge wa Tanzania si Tabaka moja na wapiga Kura. Hivyo ni Wazi nchi imetengeneza Matajiri kuwa wawakilishi wa masikini.

ASANTE WAZIRI BASHE KWA SOMO ZURI.
Masikini wanatumika kuhalalisha uhalifu wa hawa watu hoja ya Mpina haijajibiwa kupitia sukari kwa makusudi watu wanajinufaisha kwa kigezo na kisingizio cha dharula leo hii huyo waziri akiambiwa atake majina ya wote waliopatiwa vibali vya kuagiza sukari toka nje hapa kila mmoja wetu ataelewa anachokisema Mpina hivyo tusitumie masikini kuhalalisha uhalifu na wizi
 
Yupo sahihi kabisa.
Hata mimi nilishangaa mwili unakataa sukari na mafuta automatikaly.
Na unapenda supu na ndizi za kuchemsha asubuhi.
Mmchana ugali na nyamachoma mbuzi, kuku au Samaki, na juice.
Jioni tambi, mayai mchemsho na mbogamboga na juice isiyowekwa sukari.
And free sugar beer or dry wine before a sleep.
Yaani Hadi kimombo kinakuja automatikaly mdomoni.

Soda situmii kabisa na nikipewa kwenye vikao, moja siimalizi.

Bashe Yuko sahihi.
Matajiri wanapenda kahawa zaidi.
 
Back
Top Bottom