Huruhusiwi kuhoji maamuzi ya ZEC, NEC, Balaza la Mawaziri, Uchaguzi wa Rais Mahakamani

Tanzania Njema Yaja

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
3,042
2,417
Wakuu na hasa Wanasheria naomba msaada kwenye suala hili..... Wakati Mh. Raisi anaongea na wazee wa Dsm, alishangaa ni kwa nini CUF wasiende mahakamani wakati mahakama zipo na wao wanataka yeye aingilie kati Mgogoro wa uchaguzi Zanzibar .... alimalizia kwa kusema hataingilia na atakae leta fyoko fyoko nchi nzima, yeye kama Amiri Jeshi mkuu atamshughulikia....

Baadae nilisikia mwanasheria mmoja wa CUF akisema kuna kifungu cha
sheria ndani ya Katiba ya Zanzibar na
Tanzania kinacho zuia kwa njia yeyote ile kuhoji kazi na maamuzi ya ZEC na NEC mahakamani.... hapa ndo nimeshindwa elewa hii imekaaje? Mwenye kujua tafadhali anijuze....

Baadae niligundua kuwa hata maamuzi ya Baraza la Mawaziri huwezi yahoji mahakamani na kama
tunavo jua uchaguzi na matokeo ya Uraisi pia.....

Kimsingi Demokrasia maana yake nini? Si ni wengi wape na je hivi vizuizi ndani ya Katiba vipo kwa nini?

Nawakilisha.... Jazba hapana....
 
Halafu wanakimbilia kujitoa ICC Bara la Afrika ni laana tupu.
Mkuu hata sielewi..... maana kama maamuzi ya baraza la mawaziri hayawez hojiwa mahakamani maana yake ni maamuzi ya Raisi.... maana Raisi akiwa dictator na yeye ndo anachagua baraza maana yake maamuzi yote ya baraza yanaweza kuwa ya mtu mmoja..... tuombe haya yasitukute kwa kweli...
 
Yaaaaa. Kwa upande wa katiba ya URT ya Mwaka 1977 Ibara ya 74 kwenye Kifungu kidogo(Subsection) 12, imeweka wazi kuwa "Hakuna Mahakama yoyote itakayo kuwa na Maamlaka ya kuchunguza jambo lolote lilotendwa na Tume ya Uchaguzi katika kutekeleza madaraka yake kwa Mujibu wa masharti ya Katiba hii"
 

LAKINI KATIBA HIYO HOYO HAIKIPA TUME UWEZO WA KURUDIA UCHAGUZI WOTE AMA JIMBO PASIPO KULALAMIKIWA NA MAHAKAMA KUTOA MAAMUZI YA SHAURI HILO.
 

Do ahsante mkuu...... sasa hapo mkulu alitaka CUF waende vipi mahakamani au kuna nisilo
elewa hapa?
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…