Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 126,599
- 241,417
Katika mwendelezo wa nyuzi zetu kwenye mwezi huu wa 3 , ambao unaitwa Mwezi wa Mungu , Hatimaye tumemfikia Ndugu Humphrey Polepole , Mjumbe wa kamati ya kuratibu Maoni ya Wananchi ya Mchakato wa katiba mpya au katiba ya Warioba , DC wa zamani wa Ubungo , Katibu wa uenezi na Itikadi wa ccm , ambaye sasa ametunukiwa ubalozi .
Huyu ni miongoni mwa vinara wa kuua Demokrasia Nchini Tanzania , ametajwa waziwazi kuhusika na kununua Madiwani na Wabunge wa Upinzani kwa kutumwa na Bosi wake , katika ule uchafu ulioitwa kuunga mkono Juhudi , Pole pole anatajwa kutumia vikosi vya Usalama wa Nchi kutisha wale waliokuwa wanakaidi kuunga mkono Juhudi zao hizo ( wako walioshughulikiwa )
Ni wazi kwamba Bwana Humphrey alitumwa lakini hiyo haiwezi kumuondoa kwenye orodha ya wauaji wa Demokrasia ya Nchi , kwa niaba ya serikali huyu akiwa mtendaji wa Chama cha siasa aliingia makubaliano ya hela na vyeo na Wahamaji , yaani unanunuliwa na unapewa cheo , mifano ni mingi mno , pichani hapo juu ni Polepole na Julius Kalanga aliyekuwa Mbunge wa Monduli kupitia Chadema , usiku wa manane alipokuwa anatangaza kuunga mkono Juhudi , ambapo inatajwa kwamba bei yake ilikuwa mil 600 tu za madafu ili alipe madeni anayodaiwa Benki .
Ukiacha haya ya kununua wapinzani , Polepole na genge lake likiongozwa na Jiwe waliwazuia Wanachama wa ccm kuchukua fomu za kugombea kwenye majimbo na kata zilizo wazi baada ya waliokuwepo kuunga Juhudi kinyume cha katiba ya chama chao, ili kulinda Makubaliano ya wasaliti waliounga Juhudi kwa kuwafanya wagombea tena kwenye majimbo hayo hayo kwa tiketi ya ccm , hii maana yake ni kwamba wanaccm walinyang'anywa chama chao na genge la watu wachache tena wa kuja wasio na historia yoyote kwenye ccm .
Viongozi wakuu wastaafu wa ccm na wa serikali waliufyata ili kuogopa kutukanwa ama kutekwa , huku wakionywa kwamba muda wao umekwisha .
NITASEMA KWELI DAIMA FITINA KWANGU MWIKO