Humphrey Polepole aibuka upya, aongea mambo yenye utata!!

The Phylosopher

JF-Expert Member
Mar 11, 2015
1,963
2,945
Aliyekuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba leo ameibuka na kuzungumzia mambo mbalimbali yanayoendelea nchini kuhusu katiba.

Polepole amesema Katiba Pendekezwa ina mapungufu kuizidi hata ya mwaka 77 tuliyonayo, sasa hivyo anapendekeza kuwa badala ya kuipigia kura ya maoni, ni vema pawepo maridhiano kwani bunge la katiba liliipoka katiba ya wananchi na kuifanya katiba ya viongozi.

Kuhusu mgogoro wa Zanzibar, anasema ufumbuzi wake ulikua kwenye Rasimu ya Warioba, lakini katiba pendekezwa imeukuza sana huo mgogoro kuhusu yeye kuwageuka Ukawa amesema si kweli kuwa yeye aliwageuka Ukawa, isipokuwa ukawa walisaliti misimamo yao kwa kumkaribisha na kumpa nafasi mtu ambae yeye binafsi na wajumbe wenzie walimpinga hata akiwa CCM, kwani anaamini kuwa Lowassa hakuwa na uadilifu wa kumuwezesha kuleta mabadiliko chanya.

Kuhusu CCM na ufisadi, amesema CCM ndio chama pekee hapa Tanzania kuwahi kukiri kuwa kuna ufisadi ndani ya chama na sasa kimedhamiria kuukomesha, vyama vingine havijafanya hivyo ingawa kwao pia kuna ufisadi.
 
Hakutegemea kutoswa na CCM. Abaki hukohuko hatumhitaji
 


Huyu jamaa huwa anajuwa kila kitu hahahaha huwa nikimuonaga kwenye television huwa nahisi kama kutapika flani hivi
 
Huyu jamaa huwa anajuwa kila kitu hahahaha huwa nikimuonaga kwenye television huwa nahisi kama kutapika flani hivi
kwa sababu anaeleza mambo usiyoyafurahia ? vumilia kamanda hiyo ndio demokrasia! ! lazima usikie mambo unayopenda na usiyoyapenda maamuzi baki nayo rohoni mwako. huna haja ya kutusimulia
 
Polepole alikuwaga! alisigina mtaji wake mwenyewe kwa kubadilika kutoka mwanaharakati wa mabadiliko na kuwa kada mkereketwa "vululuvululu" wa chama cha majizi ccm! He lost his major asset; MORAL AUTHORITY & CREDIBILITY; he can go hang for all I care!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…