Hukumu zenye utata kama hii ya Askari Morogoro huwa zinasababishwa na nini?

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,550
22,097
Kuna kesi ya askari magereza aliyekuwa na tuhuma za kubaka mtoto huko Morogoro.

Alipelekwa mahakamani na ikathibitika pasi na shaka kwamba alitenda kosa hilo na hakimu msomi akaitolea hukumu ile kutumikia kifungo cha maisha jela. Hiki ni kifungo cha kikatili ambacho lazima kusiwe na chembe ya mashaka ya ushahidi.

.Kama kulizingatiwa ushahidi basi ushahidi wake naimani ulikuwa active kwa muda huo kutokana na mazingira, vielelezo na hata vipimo vya matabibu.

Baada ya mtuhumiwa kukata rufaa hukumu ile;

Miezi sita baadae mahakama ya rufaa imekuja na hukumu nyingine ya kutengua hukumu na kumwachia huru mtuhumiwa baada ya kujiridhisha hakubaka.

Kama kulizingatiwa ushahidi katika rufaa hii basi walitumia vielelezo vilivyopo ambavyo kutokana na muda mrefu kupita huenda vikawa na majibu tofauti na ya awali, kama ni damu inaweza kuwa imekauka, kama ni bikira inaweza ikawa imerudi maana kuna bikra za michongo kurudisha bikra, n.k.

Hivyo kwa maoni yangu bikira haifai kutumika kama kielelezo kwasababu kwanza inatengenezeka siku hizi, pili ni hatari kwa mtuhumiwa kwasababu zinaweza tokea tuhuma za ubakaji kwa mbakwaji ambaye hana bikira, yamkini anakuwa kashatolewa na watu wengine kabla!

Je, wataalam hawaoni wanaweza mfunga mtu maisha kimakosa kwa kielelezo cha ubikira?

Je, katika kesi kama hizi mahakama ya awali hadi kumfunga mtu maisha huwa wanatumia ushahidi upi, na wanaokuja kubatilisha hukumu huwa wanatumia ushahidi gani?

Tunashukuru askari kaachiwa huru katika rufaa lakini watuhumiwa wangapi wamefungwa maisha kwa style yake?
 
Askali!!!? Ndiyo maana ameachiwa Angekuwa Askari asinge achiwa. Kwenye rufaa hakuna ushahidi mpya unatolewa Bali wanaangalia kama Mahakama ya Chini ilikosea katika kufikia maamuzi husika iwe kisheria au Kwa fact.
Sasa kama walikosea hukumu nzima kiasi cha kufutwa hauoni hilo ni hatari wangapi watakuwa wamefungwa maisha KIMAKOSA?
 
Report ya Dr ni kielelezo muhimu sana kwenye kesi za ubakaji sasa jiulize huko hospitali Huwa wanapimwa vipi? Ukigundua jibu bas utakuwa umejijibu
Sijaongelea report ya Dr, nimeongelea definition ya kubaka. Kwa mfano mtu akagusisha uume wake juu ya uke wa mwanamke bila kumuingilia kabisa, je atakuwa amebaka?
 
Kuna kesi ya askali magereza aliyekuwa na tuhuma za kubaka mtoto huko Morogoro.

Alipelekwa mahakamani na ikathibitika pasi na shaka kwamba alitenda kosa hilo na hakimu msomi akaitolea hukumu ile kifungo cha maisha jela. (Hiki ni kifungo cha kikatili ambacho lazima kusiwe na chembe ya mashaka ya ushahidi)

(Kama kulizingatiwa ushahidi basi ushahidi wake naimani ulikuwa active kwa muda huo kutokana na mazingira, vielelezo na hata vipimo vya matabibu)

Baada ya mtuhumiwa kukata rufaa hukumu ile;

Miezi sita baadae mahakama ya rufaa imekuja na hukumu nyingine ya kutengua hukumu na kumwachia huru mtuhumiwa baada ya kujiridhisha hakubaka.

(Kama kulizingatiwa ushahidi katika rufaa hii basi walitumia vielelezo vilivyopo ambavyo kutokana na muda mrefu kupita huenda vikawa na majibu tofauti na ya awali, kama ni damu inaweza kuwa imekauka, kama ni bikira inaweza ikawa imerudi maana kuna bikra za michongo kurudisha bikra, n.k)

Hivyo kwa maoni yangu bikira haifai kutumika kama kielelezo kwasababu kwanza inatengenezeka sikh hizi, pili ni hatari kwa mtuhumiwa kwasababu zinaweza tokea tuhuma za ubakaji kwa mbakwaji ambaye hana bikira, yamkini anakuwa kashatolewa na watu wengine kabla!

Je, wataalam hawaoni wanaweza mfunga mtu maisha kimakosa kwa kielelezo cha ubikira?

Je, katika kesi kama hizi mahakama ya awali hadi kumfunga mtu maisha huwa wanatumia ushahidi upi, na wanaokuja kubatilisha hukumu huwa wanatumia ushahidi gani?

Tunashukuru askali kaachiwa huru katika rufaa lakini watuhumiwa wangapi wamefungwa maisha?
Ngja nikusanue, Kesi nyingi za ubakaji huwa na makosa mengi sana ya kisheria kutokana na matukio jinsi yalivyo..Hali hii hupelekea mahakama za chini kufanya maamuzi under pressure kutokana na mobb psyhology ya jamii husika...hivyo kutenguliwa baadayee inakuwa rahisi. Kesi nyingi sana za ubakaji kuchomoka katika mahakama za wilays ni ngumu sana. Mf mwalimu katuhumiwa kubaka Kesi dizain hii inavuta hisia kubwa, ghafla, mwl anaachiwa usalama wa mwl na Hakimu unakuwa mdogo.. hivyo solution ni rufaa...
 
Back
Top Bottom