Hukumu ya Wachina majangili wa tembo sasa Machi 18

Daniel Mbega

JF-Expert Member
Mar 20, 2013
338
180
Hukumu ya raia wa China wakiokamatwa na meno ya tembo sasa itatolewa Ijumaa ijayo Machi 18 baada kuahirishwa leo.
Akiahirisha kesi hiyo, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Kisutu Cyprian Mkeha, amesema tayari hukumu hiyo imekamilika lakini bado hajamalizia kuiandika kutokana na kuugua, hivyo akawataka radhi upande wa mashtaka na utetezi.
"Hukumu iko tayari lakini nimeshindwa kuikamilisha kuiandika kutokana sababu zilizo nje ya uwezo wangu. Sikutaka kabisa kuahirisha shauri hili lakini nitaisoma Ijumaa mapema asubuhi," alisema Hakimu Mkeha.
Raia hao wa China, Huang Qing na Xu Fujie, walikamatwa Novemba 2, 2013 katika mtaa wa Kifaru, Mikocheni B jijini Dar es Salaam wakiwa na shehena ya meno 706 ya tembo ambayo ni sawa na tani 1.8 yenye thamani ya shilingi za Kitanzania 5,435,860,000.
Upande wa mashtaka uliongozwa na wakili wa serikali mkuu Faraja Nchimbi akisaidiana na mawakili Paul Kadushi, Simon Wankya na Salim Msemo.
Washtakiwa walikuwa wakitetewa na wakili Chuwa pamoja na Nehemia Mkoko.
 

Attachments

  • 1457682223649.jpg
    41.6 KB · Views: 26
  • 1457682249428.jpg
    39.6 KB · Views: 24
  • 1457682343070.jpg
    32.6 KB · Views: 22
Yetu masikio tunasubiria hiyo hukumu mana kwa tz wanaweza kufungwa miaka 5......wakti hao adhabu yao na ili iwe fundisho kma watuhumiwa wenzao wa ujangili kule simiyu kifungo halali ni miaka 161
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…