Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 4,079
- 13,921
Ushahidi katika kesi Namba Cc.5866 /2024 inayomkabili Baraka Benedicto (23) anayedaiwa kumlawiti mtoto wa Kiume umehitimishwa rasmi Machi 7, 2025 baada upande wa Mshtakiwa kukamilisha utetezi wake.
Akizungumza mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni mara baada ya mshtakiwa kuhitimisha utetezi wake, Wakili wa Jamhuri ameiambia Mahakama kwamba wamefunga rasmi ushahidi, hivyo akaomba kesi ipangiwe siku ya hukumu.
Baada ya kueleza hayo Mahakama kupitia Hakimu Nabwike Mbaba amesema kesi hiyo itatajwa Machi 14, 2025, ambapo itakuja kwa ajili ya kutolewa hukumu.
Mshtakiwa alipopewa nafasi ya kujitetea kabla ya ushahidi kufungwa amekana kwamba hakutenda tukio hilo la kumuingilia mtoto kinyume na maumbile (ulawiti) na kudai kwamba tukio hilo ni lakusingiziwa.
Ikumbukwe mshtakiwa huyo alipandishwa Mahakamani siku chache baada ya Mwanachama wa JamiiForums.com kudai kwamba kulikuwepo na mazingira ya danadana ya kutomfikisha Mahakamani mtuhumiwa (Baraka) ambaye inadaiwa akiwa anatekeleza majukumu ya ulinzi alimfanyia ukatili wa kumlawiti mtoto wa kiume kwenye vyoo vya Parokia ya Bikira Maria Mama Mwokozi, Sinza – Dar es Salaam.
Andiko la kwanza la Mwanachama huyo aliliandika Februari 13, 2024 na mtuhumiwa akafikishwa Mahakamani kwa mara ya kwanza Machi 6, 2024.
Pia soma:
~ Mlinzi wa Kanisa (Sinza, Dar) aliyeshtakiwa kwa kumlawiti mtoto kwenye vyoo vya Kanisa, atupwa jela Miaka 30
~ Anayetuhumiwa kumlawiti mtoto katika Vyoo vya Kanisa - Sinza, asema “Sina lolote, naiachia Mahakama”
~ Anayetuhumiwa kulawiti Mtoto kwenye Vyoo vya Kanisa ashindwa kutoa Ushahidi, adai anaumwa, kesi yaahirishwa hadi Machi 3, 2025
~ Tukio la Mlinzi wa Kanisa Katoliki Sinza kudaiwa kumlawiti Mwanafunzi, Padri asimulia kilichotokea
~ Dar: Mlinzi wa Kanisa anayetuhumiwa kumlawiti Mtoto Muimba kwaya kwenye vyoo vya Parokia apandishwa kizimbani
~ Madai ya Mlinzi wa Kanisa Katoliki Sinza kumlawiti Mwanafunzi, mama wa Mtoto aomba Serikali imsaidie
~ Serikali imsaidie Mtoto huyu anayedaiwa kulawitiwa na Mlinzi wa Kanisa Katoliki Sinza