Hukumu dhidi ya KANU ya Kenya kunyang'anywa jengo la KICC, Iko siku itawakumba CCM.

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
20,932
39,766
Jaji Jacqueline Mogeni wa mahakama ya Ardhi Kenya, ametupilia mbali hoja ya chama cha siasa cha Kenya Africans National Union (KANU) ya kudai kuwa walinyang'anywa Jengo la Kimataifa la mikutano la Kenyatta (Kenyatta International Conference center-KICC) kinyume Cha Sheria.

Pia Jaji Mogeni amekataa ombi la chama hicho kikongwe Cha siasa Kenya, la kutaka kurejeshewa jengo Hilo.

Msingi wa hukumu ya Jaji Mogeni ulijikita kwenye hoja kwamba mchakato wa KANU wa kupata Ardhi lilipojengwa jengo Hilo, ulikuwa batili tangu kuanza kwake.

Nikiangalia jinsi CCM ilivyojimilikisha kiharamu majengo na Ardhi za umma, Iko siku mhamaniko na kutapatapa huku kwa KANU, kutawakuta na wao pia.
 
Viwanja vya mpira zipewe halmashauri na halmashauri ziboreshe view viwanja vya kisasa vyenye nyasi laini na za kuvutia
 
Back
Top Bottom