Shule ya Sekondari ya Nshupu iliyopo Kijiji cha Nshupu, Wilaya ya Arumeru, Kata ya Nkoaranga Mkoani Arusha haina milango na katika baadhi ya majengo ikiwemo yale ambayo wanaishi Wanafunzi wa kike wa shule hiyo.
Kutokana na hali hiyo kumekuwa na matukio ya wahalifu kuvamia na kufanya uhalifu ikiwemo kuiba na kuwafanyia ukatili Wanafunzi hasa Wasichana.
Taarifa nilizo nazo ni kuwa hivi karibuni kuna Wahalifu waliovamia shuleni hapo na kuingia kwenye bweni la Wasichana na kufanya yao, hali hiyo imesababisha baadhi ya Watoto waanze kuondoka kwenye shule hiyo kwa kuwa wanahofia usalama wao.
Jamaa wanaovamia, wakiingia ndani ya shule hiyo wanazima umeme kisha wanaendelea na uhalifu uliowapeleka
===UPDATE====
JamiiForums ilipomtafuta Mwenyekiti Mtendaji wa Kijiji cha Nshupu, Geoffrey Mungure amesema:
Suala hilo lipo chini ya Mkuu wa Mkoa, Afisa Elimu wa Wilaya, Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya, pia sio kwamba hakuna milango, ipo lakini kitengo cha laboratory huwa hakiwekewi madirisha ya chuma kwa sababu za kiusalama.
Kuna vijana watatu walivamia kwa kupitia laboratory, kuna Wanafunzi wakawaona wakapiga kelele, wale wahalifu wakakimbia lakini baadaye walikamatwa na maelekezo mengine yapo chini ya Wakubwa.
Wale vijana waliingia hakuna kitu walichogusa, walikuwa karibu sana na mabweni ya kike, tukawa na hisia labda wanataka kuwabaka wale Watoto au vipi.
Wale vijana walipokimbia waliacha kofia wakati wanakimbia, hivyo wakahisiwa na kuanza kufuatiliwa na kisha kukamatwa.
Sababu ya kupitia Laboratory ilikuwa kama njia ya kuelekea kwenye mabweni ya Wasichana.
Mambo mengine yapo chini ya Mahakam ana ngazi nyingine za usalama. Tunao Ulinzi Shirikishi ambao wanalinda usalama.
Hili ni tukio la pili, nilisikia sikuwepo, walivami vilevile katika bweni la Wasichana, inawezekana walikuwa na mambo yao.