DOKEZO Huku Arumeru kuna jamaa wanavamia mabweni ya Wasichana (Shule ya Sekondari ya Nshupu) na kufanya uhalifu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Shule ya Sekondari ya Nshupu iliyopo Kijiji cha Nshupu, Wilaya ya Arumeru, Kata ya Nkoaranga Mkoani Arusha haina milango na katika baadhi ya majengo ikiwemo yale ambayo wanaishi Wanafunzi wa kike wa shule hiyo.

Kutokana na hali hiyo kumekuwa na matukio ya wahalifu kuvamia na kufanya uhalifu ikiwemo kuiba na kuwafanyia ukatili Wanafunzi hasa Wasichana.

Taarifa nilizo nazo ni kuwa hivi karibuni kuna Wahalifu waliovamia shuleni hapo na kuingia kwenye bweni la Wasichana na kufanya yao, hali hiyo imesababisha baadhi ya Watoto waanze kuondoka kwenye shule hiyo kwa kuwa wanahofia usalama wao.

Jamaa wanaovamia, wakiingia ndani ya shule hiyo wanazima umeme kisha wanaendelea na uhalifu uliowapeleka

===UPDATE====

JamiiForums ilipomtafuta Mwenyekiti Mtendaji wa Kijiji cha Nshupu, Geoffrey Mungure amesema:

Suala hilo lipo chini ya Mkuu wa Mkoa, Afisa Elimu wa Wilaya, Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya, pia sio kwamba hakuna milango, ipo lakini kitengo cha laboratory huwa hakiwekewi madirisha ya chuma kwa sababu za kiusalama.

Kuna vijana watatu walivamia kwa kupitia laboratory, kuna Wanafunzi wakawaona wakapiga kelele, wale wahalifu wakakimbia lakini baadaye walikamatwa na maelekezo mengine yapo chini ya Wakubwa.

Wale vijana waliingia hakuna kitu walichogusa, walikuwa karibu sana na mabweni ya kike, tukawa na hisia labda wanataka kuwabaka wale Watoto au vipi.

Wale vijana walipokimbia waliacha kofia wakati wanakimbia, hivyo wakahisiwa na kuanza kufuatiliwa na kisha kukamatwa.

Sababu ya kupitia Laboratory ilikuwa kama njia ya kuelekea kwenye mabweni ya Wasichana.

Mambo mengine yapo chini ya Mahakam ana ngazi nyingine za usalama. Tunao Ulinzi Shirikishi ambao wanalinda usalama.

Hili ni tukio la pili, nilisikia sikuwepo, walivami vilevile katika bweni la Wasichana, inawezekana walikuwa na mambo yao.
 
Mkoa wa Arusha umekuwa wa hovyo.

Ukatili ni mkubwa.

Hapo jana nimesikia wahuni walimvamia mama ima wakambaka na kupora.

Ma ima mwimbaji na mtumwa wa Bwana, amefariki, atazikwa Monday.

Mheshimiwa Makonda hebu angalia mkoa wako, uko hovyo.
 
Kukusahihisha tu hiyo shule ni Day haina mabweni kilichofanywa ambacho ni hatari ni wanafunzi wa madarasa ya mitihani form iv na ii kutenga madarasa kufanya mabweni. Shule haina uzio wala miundombinu ya kulaza watoto humo. Tuchukue hatua madhubutu kujenga miundombinu ya kuwasaidia hao watarajiwa wa madarasa ya kufanya mitihani kuliko njia hii hatarishi inayotumika kwa sasa.
 
Back
Top Bottom